Kitaratibu ilikuwa malalamiko hayo yalikuwa yapelekwe UN, lakini si Marekani ambao ni taifa na wanakosa uhalali wa kuingilia moja kwa moja mambo ya nchi fulani, zaidi sana labda kuondoa misaada.
Pia wazungu wanatuchora sana na kujua akili zetu zimeishia wapi, sina hakika kama ni wazuri katika kuondoa matatizo ya namna hii katika nchi yoyote duniani kwa faida ya hyo nchi.
Swali; hv Uganda kuna demokrasia kuzidi Tanzania, vp uhusiano wake na Marekani. Tuamke, utatuzi sahihi wa matatizo yetu u mikononi mwetu watz, generally waafrika.
Jinsi barua ilivoandikwa juu ya utawala wa awamu ya tano mtu wa nje anaweza fikiri watz tulikuwa jehanamu, mi nasema ukikuza jambo lolote ama kwa chuki au malengo yako fulani, huja kudharauliwa hata kama ulikuwa na hoja za mantiki.
Marekani anajali maslahi yake, ukitishia maslahi yake mara moja unageuka dikteta hata kama sio.