The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 10,805
- 14,181
Hakina wa kikichukia ila hata huku Ccm hatutaki mnagiki wa hivi lowasa mkubwa weSijui ni nani aliyewaaminisha Watanzania kuwa ukiwa na tatizo la Kisiasa na Kidemokrasia Basi Kimbilio huwa ni Ubalozi wa Marekani au nchini Marekani.
Mna uhakika wa 100% kuwa na Wao Wamarekani huko Kwao hakuna Ukiukwaji wa Kidemokrasia na Masuala ya Siasa? Mbona huwa hatukimbilii Balozi za Uingereza au Urusi au Ujerumani na hata China ikiwezekana?
Kwahiyo Kukimbilia Marekani ( katika Ubalozi wao ) ndiyo mnataka Kuwalazimisha waende Mahakamani wakawe Mawakili na Mahakimu ili Kiongozi wenu atoke ( atolewe ) upesi?
Hivi kwa jinsi ambavyo sasa hivi Tanzania chini ya Utawala huu wa Rais Samia Suluhu Hassan imerejesha vyema Uhusiano wake wa Kidiplomasia na zile nchi ambazo Kipindi cha Hayati Dkt. Magufuli ulitetereka mnadhani mtasikilizwa na kuonekana wa maana au mna Hoja au sana sana mtasanifiwa tu na Kupuuzwa?
CHADEMA ni Watani zangu Kisiasa GENTAMYCINE nikiwa ni mwana CCM 'tukuka' kabisa ila mara kwa mara tena hapa hapa JamiiForums nimekuwa nikiwaambieni kuwa msipobadilisha 'Political Strategies' zenu mnapotea Kisiasa na Kidemokrasia na msipoangalia mnapoelekea muda ni si mrefu mtakuwa 'labelled Political Terrorist Group' ndani ya Tanzania na Chama chenu Kufutwa kabisa.
Najua kwa post yangu hii Kwenu leo mtanichukia na Kunitukana mno tu hapa, ila nawashauri CHADEMA rudini katika Misingi yenu, Jitafakarini na ikiwezekana Mjisahihishe kwa Ustawi wa baadae wa Chama chenu.
Ubalozi wa Marekani wala Balozi wa Marekani hakuna mwenye Mamlaka ya 'Kuishurutisha' Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais Samia Suluhu Hassan ifanye wanavyotaka Wao na niwaambie hili halitotokea hata Siku moja.
Mnaharibu wenyewe mnataka Msaada.