Majina wanaopewa wanaume wasiofanyiwa tohara kwenye makabila mbalimbali nchini

Majina wanaopewa wanaume wasiofanyiwa tohara kwenye makabila mbalimbali nchini

Wadau hamjamboni nyote?

Naleta majina yanayotumika kwa watu ambao hawajafanyiwa tohara kwenye makabila mbalimbali nchini

Isemboo Kichaga
Warisyaa Kikurya
Isekaa Kimeru
Laiyok Kimasai
Akakata Kinyakyusa
Murajoni Kikaguru

Naomba utaje huko kwenu wasiofanyiwa tohara wanaitwaje

Niwatakie siku njema wapendwa
Kwetu hatufanyi huu ujinga ambao unapunguza raha!
 
Watani zangu Wajaluo na wasukuma hawawezi kutokea hapa maana ni jadi yao kutotahiriwa😆
Wahaya na makabila yote ya mkoa wa Kagera wanaotahiriwa ni waislamu tu, ila miaka ya karibuni kuanzia mwaka 2000 baada ya serikali kufanya kampeni maalumu kuhimiza wanaume kutahiriwa ndio wakristu wa mkoa wa Kagera wameanza na wao kutahiriwa.
 
Unahakika siyo lazima?
Wanachuoni Wana kauli tafauti juu ya jambo hili.
1. Kauli ya kwanza kutahiriwa ni lazima kwa wanaume na wanawake.
2. Kauli ya pili kutahiriwa ni Sunna kwa wanaume na wanawake.
3. Kauli ya tatu kutahiriwa ni Lazima kwa wanaume na ni Sunna kwa wanawake, na kauli hii ya tatu ndiyo inayoelekea kuwa na nguvu.
 
kwanini watu wasiofanyiwa tohara wapewe majina ya ajabu ajabu wakati kitendo hicho sio jambo la lazima, na hata mtu asipofanyiwa hapungui lolote
Pole sana Govinda, huku ndiko kupigwa na jiwe gizani.

Ubinadamu ni kazi/The humanity is a work.
 
Back
Top Bottom