Mkuu
Amavubi huko unakotaka kwenda kwenye mambo ya Anglicana,Lutheran ni kuleta mada mpya,kwanza kujadili mambo hayo inabidi uwe "umeiva" kiimani,usije "ukaasi" kanisa lako.
Kiufudi hizi dini ni "utamaduni",sisi Waafrika tuliletewa tu na wamisionari..lkn dini hutambulisha utamaduni wa mtu.Martin Luther alipoona nchi yake ya Ujrumani haitambuliki na Papa aliye Rome Italy anatoa amri ambayo mpaka wao Ujerumani wanaitii akaona ni kama "utumwa",ndio maana akasema lazima aondoe ile "Papacy Authority",kwamba kwanini kila kitu kitoke Vatican,yaani kwa lugha nyingine ni kuwa kwanini kila kitu atoe amri Mtaliano??Akaamua kuanzisha dhehebu lake na akalipa jina lake,yeye akiitwa Martin Luther basi kanisa lake liitwe "Lutheran" i.e "Of the Luther".Lengo ni kuondokana na mamalaka ya Vatican chini ya mtaliano na kukuza utaifa wao wa Ujeruman,na ndio maana makao makuu ya Lutheran yakawa Ujerumani...Ulutheri ni alama ya utamaduni wa Mjerumani,alihitaji "identity" yake na akaipata.
Mfalme George VIII wa Uingereza,akiwa muumini safi wa kanisa katoliki,akataka kuoa mke mwingine aachane na Catherine of Aragon,lkn sbb kanisa katoliki hurusiwi kuoa mke mwingine wakati mmoja yupo akakataliwa na Papa.Mfalme akaona Papa anamuingilia mpaka kwenye "ufalme" wake,akaamua kuanzisha kanisa akaliita "Anglican Church" toka neno "Anglo",maana Anglo= England,hivyo Anglican Church maana yake kanisa la England,akajitoa mikononi mwa "Papacy Authority" ili na yeye awe na kanisa lenye utamaduni wao.Anglican Church likawa kanisa la nchi,Mkuu wake ni malkia na kiongozi wake wa kiroho ni askofu wa Canterbury,hii ikawa ni alama ya Uingereza na utamaduni wao,ikawa kama wewe si Muanglicana basi huwezi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza,wakaweza kuanzisha kanisa la utamaduni wao...Dini ni utamaduni
Huku Afrika kuna watu walijaribu kaunzisha makanisa yenye ukristo wa kiafrika,maana waliona kabisa kuwa YESU WA AFRIKA ana tofauti sana na YESU WA ULAYA..kwamba inapswa tuwe na ukristo unaoakisi utamaduni wetu maana dini ni utamaduni,Congo ya Zaire akatokea mtu anaitwa SIMON KIMBANGU akaanzisha kanisa lake akaliita "KIMBANGUISM"...alifanya miujiza na kuponya watu na magojwa,kutibu ukoma na miujiza kibao,Kimbangu akawa na waumini wake lukuki walioukimbia Ukatoliki na Uprotestanti,hii iliwatisha wamisonary wakashitaki kwa serikali ya kikoloni,Simon akakamatwa na kushitakiwanbila kupewa nafasi ya kujitetea,kanisa lake likakuwa na kudidimiza "UKRISTO WA ULAYA" wa wakatoliki na protestanti.Waumini wake wakakamatwa na serikali ya kikoloni ya mbeligiji na wakateswa na wengine kupelekwa "exile" ili kuuwa mshikamano wao.Kimbangu alifia gerezani,dhamira yeke ilikuwa kama ile ya Martin Luther na Mfalme George VII,kuanzisha dhehebu linaloakisi utamaduni wake,yaani utamaduni wa muafrika..Isingekuwa fitna za Mkatoliki na mprotestanti kwa kushirikiana na serikali katili ya mbeligiji,leo hii Afrika nasi tungekuwaa na dini ya "YESU WA KIAFRIKA"....Kwa hiyo ndugu
Amavubi bhizi dini ni utamaduni...Umasikini wetu na nguvu za ukoloni zilituzuia kuimarisha dini zinazoendana na utamaduni wa kiafarika.Kwenye picha hiyo,Simon Kimbangu ni huyo aliyevaa shuka