Tokyo40
JF-Expert Member
- Jun 16, 2013
- 2,065
- 1,925
Ngoja waje wazee wa vipedo wathibitishe
Siandiki kitu hapa bila ya kithibitisho.
Mara nyingine kuweka vithibitisho ni kujaza servers tu.
Lakini vipo vikihitajika, haina shida.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ngoja waje wazee wa vipedo wathibitishe
Waendelee tuu kuoana ili Obama na mfumo Kristo uendelee
Vyeti vya ndoa vinatolewa na Jamuhuri ya Tanzania na vinatambua mume mmoja kwa mke mmoja.
Vyeti vya ndoa Tanzania zina option ya Ndoa ya mke mmoja au wake wengi.Mkuu, Je na wale wenye wake zaidi ya mmoja?
Dini na mila mbalimbali Tanzania zinaruhusu.
Wake zao si wanatambulika na sheria za ndoa ya Tanzania?
Kuhusu uhalali wa nani wa kuoa, Wakristo na Waislamu wamefuata sana tamaduni zao za asili na za wale waliowaletea dini kuliko maandiko ya dini yenyewe!Sina data lakini ninawafahamu watu wengi wameoa binamu zao Tanzania, Kenya na Uarabuni.
Huu utamaduni ni kweli hatari kwa afya ya mtoto.
Kuna mmoja ameoa mke, baba zao ndugu, mama zao ndugu. Watoto wote wamezaliwa na afya duni na vichwa vikubwa kupita kiasi.
Sifahamu kama wanaoa/wanaolewa kwa idhini yao au wanalazimishwa/wanapangiwa na wazazi wao.
Elimu duni inahusika sana hapa.
Kuhusu uhalali wa nani wa kuoa, Wakristo na Waislamu wamefuata sana tamaduni zao za asili na za wale waliowaletea dini kuliko maandiko ya dini yenyewe!
Kwa mfano, kwa Waislam, wameorodheshwa wale ambao mtu haruhusiwi kuoa na ambao hawapo kwenye list inachukuliwa ni halali kama hao mabinamu kv hawamo ktk orodha ya waliokatazwa! Lakini pamoja na hayo, kuna jamii kadhaa za Kiislamu ambao hao kwao ni ndugu wa damu na katu huwezi kuoa. Hata hivyo, Waislamu hususani wa visiwani wao wanaoleana wao kwa wao simply because kule visiwani hawana tamaduni za Kiafrika! Wale wenye asili kabisa ya kule huwezi kumsikia kwamba kabila lake ni fulani... na kutokana na hilo unakuta majority tamaduni zao ni tamaduni za dini kv hawana tamaduni za kikabila.
Ukija kwenye Ukristo, nako wala hakuna tofauti na Uislamu coz' hakuna popote ilipokatazwa kuoa binamu kwa kuangalia orodha ya wale ambao biblia inakataza kuoa. Ukisoma Bible imeanza kwa kusema umekatazwa kuoa ndugu zako wa karibu. Baada ya mstari huo, ikaanza kutaja watu ambao huruhusiwi kuoa na katika hao binamu hawapo!
Lakini kv inawezekana waliotuletea dini ya Ukristo hata kabla ya dini kwao binamu ilikuwa ni nyama haramu, basi na baadhi ya Wakristo wa Afrika nao wakachukua utamaduni huo hususani wale ambao hata kwenye makabila yao, utamaduni huo ulikuwa tayari haramu since then sawa na baadhi ya makabila ya Waislamu ambao kwao binamu ni nyama haramu hata kama Quran binamu si moja ya watu ambao wamekataza kuoa.
Ulichosema ni sahihi kabisa... katika dunia ya leo ambayo secularism inazidi kushamiri ni ngumu sana kuishi vile dini zetu zinavyotaka! Kinachotokea hivi sasa ni ile tu kila mmoja kutekeleza wajibu wake japo kwa mdomo japo anafahamu practically wajibu anaouhubiri hautekelezeki!Mimekuelewa Mkuu.
Mimi binafsi nakubaliana na sheria za sayansi kuhusu athari za kuoa binamu yako (first cousin).
Kuna vitu ambavyo vinakataza katika dini tofauti lakini ni vigumu kuepuka navyo katika maisha ya leo: vidonge vya kuzuia mimba, kondom (inazuia mimba), kutoa mimba, riba ya benki, kuachana katika ndoa na pombe (kama dawa).
Sidhani kama inawezekana kuishi maisha ya leo kwa kufuata sheria za dini yoyote, hasa ukizingatia kuwa sheria za nchi nyingi zipo juu ya sheria za dini.
Nimetembea sana Asia na huko Indonesia, hairuhusiwi kuoa binamu yako, japo ni nchi ya Waislamu wengi duniani. Hata kutahiri, wanachelewa mpaka mtoto afike miaka 7 au 8 siyo kama sisi, tunatahiri akiwa mchanga.
(kuna baadhi ya makabila wanatahiri ukubwani Tanzania pia).
View attachment 325084
Mkuu Amavubi huko unakotaka kwenda kwenye mambo ya Anglicana,Lutheran ni kuleta mada mpya,kwanza kujadili mambo hayo inabidi uwe "umeiva" kiimani,usije "ukaasi" kanisa lako.
Kiufudi hizi dini ni "utamaduni",sisi Waafrika tuliletewa tu na wamisionari..lkn dini hutambulisha utamaduni wa mtu.Martin Luther alipoona nchi yake ya Ujrumani haitambuliki na Papa aliye Rome Italy anatoa amri ambayo mpaka wao Ujerumani wanaitii akaona ni kama "utumwa",ndio maana akasema lazima aondoe ile "Papacy Authority",kwamba kwanini kila kitu kitoke Vatican,yaani kwa lugha nyingine ni kuwa kwanini kila kitu atoe amri Mtaliano??Akaamua kuanzisha dhehebu lake na akalipa jina lake,yeye akiitwa Martin Luther basi kanisa lake liitwe "Lutheran" i.e "Of the Luther".Lengo ni kuondokana na mamalaka ya Vatican chini ya mtaliano na kukuza utaifa wao wa Ujeruman,na ndio maana makao makuu ya Lutheran yakawa Ujerumani...Ulutheri ni alama ya utamaduni wa Mjerumani,alihitaji "identity" yake na akaipata.
Mfalme George VIII wa Uingereza,akiwa muumini safi wa kanisa katoliki,akataka kuoa mke mwingine aachane na Catherine of Aragon,lkn sbb kanisa katoliki hurusiwi kuoa mke mwingine wakati mmoja yupo akakataliwa na Papa.Mfalme akaona Papa anamuingilia mpaka kwenye "ufalme" wake,akaamua kuanzisha kanisa akaliita "Anglican Church" toka neno "Anglo",maana Anglo= England,hivyo Anglican Church maana yake kanisa la England,akajitoa mikononi mwa "Papacy Authority" ili na yeye awe na kanisa lenye utamaduni wao.Anglican Church likawa kanisa la nchi,Mkuu wake ni malkia na kiongozi wake wa kiroho ni askofu wa Canterbury,hii ikawa ni alama ya Uingereza na utamaduni wao,ikawa kama wewe si Muanglicana basi huwezi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza,wakaweza kuanzisha kanisa la utamaduni wao...Dini ni utamaduni
Huku Afrika kuna watu walijaribu kaunzisha makanisa yenye ukristo wa kiafrika,maana waliona kabisa kuwa YESU WA AFRIKA ana tofauti sana na YESU WA ULAYA..kwamba inapswa tuwe na ukristo unaoakisi utamaduni wetu maana dini ni utamaduni,Congo ya Zaire akatokea mtu anaitwa SIMON KIMBANGU akaanzisha kanisa lake akaliita "KIMBANGUISM"...alifanya miujiza na kuponya watu na magojwa,kutibu ukoma na miujiza kibao,Kimbangu akawa na waumini wake lukuki walioukimbia Ukatoliki na Uprotestanti,hii iliwatisha wamisonary wakashitaki kwa serikali ya kikoloni,Simon akakamatwa na kushitakiwanbila kupewa nafasi ya kujitetea,kanisa lake likakuwa na kudidimiza "UKRISTO WA ULAYA" wa wakatoliki na protestanti.Waumini wake wakakamatwa na serikali ya kikoloni ya mbeligiji na wakateswa na wengine kupelekwa "exile" ili kuuwa mshikamano wao.Kimbangu alifia gerezani,dhamira yeke ilikuwa kama ile ya Martin Luther na Mfalme George VII,kuanzisha dhehebu linaloakisi utamaduni wake,yaani utamaduni wa muafrika..Isingekuwa fitna za Mkatoliki na mprotestanti kwa kushirikiana na serikali katili ya mbeligiji,leo hii Afrika nasi tungekuwaa na dini ya "YESU WA KIAFRIKA"....Kwa hiyo ndugu Amavubi bhizi dini ni utamaduni...Umasikini wetu na nguvu za ukoloni zilituzuia kuimarisha dini zinazoendana na utamaduni wa kiafarika.Kwenye picha hiyo,Simon Kimbangu ni huyo aliyevaa shuka
asante sana kwa udadavuzi
asante sana kwa udadavuzi
Mkuu Hv papa kumbe ana uwezo wakufuta madhambi ya watu?Jina lake siyo muhimu ila kinachofuatwa ni msimamo wa kile alichokuwa anakipinga dhidi ya Kanisa Katoliki:
The Ninety-Five Theses on the Power and Efficacy of Indulgences .
(Disputatio pro declaratione virtutis indulgentiarum)
Hajaanzisha kanisa lingine ila mwaka 1517, kachapisha kwa Kilatini "theses 95", moja wapo ni ya kupinga Papa kuwa na uwezo wa kufuta madhambi ya muumini, wakati huo, kwa kulipa fedha. Yaani, unanunua hati ya kusamehewa madhambi yako duniani.
Wale wanaofuata msimamo huo wa kupinga Theses 95 alizozibandika katika mlango wa kanisa la chuo chake ndiyo wanaitwa "Lutherans", kama wale wanaofuata msimamo wa siasa za Mao wa China wanaitwa "Maoists" na wa Lenin wa Urusi, wanaitwa "Leninists".
HV huu utamadun Wa kuuza hati ya msamaha Wa dhamb had Leo upo au?Wakuu,
Kuna kitu kimoja ningependa kueleza zaidi.
Ujerumani ilikuwa siyo nchi kama ya leo wakati wa Luther. Mipaka ilikuwa tofauti. Ujerumani ilikuwa sehemu moja tu ya "ardhi" iliyo chini ya "Roman Empire" , zingine zikuwa Uholanzi, Ubelgiji, Uswisi, Austria, Czech, Slovakia, baadhi ya sehemu za Ufaransa, Poland, Slovenia na Italy.
Ujerumani kama nchi ilianza mwaka 1648 katika ardhi chini ya Roman Empire iliyoifanya Empire kugawanyika katika Vita vya Miaka Thelathini (1616-1648).
Ujerumani ilianza hapo na Saxony, Bavaria na Prussia.
Nchi ikaungana zaidi na kuwa na nguvu chini ya Otto Van Bismark mwaka 1871.
Baadhi ya ardhi yake ikapokonywa katika vita dhidi ya Uiingereza, Urusi, Ufaransa na Marekani (1914-1918), baadhi ya ardhi yake ikawa chini ya utawala wa nchi nyingine kabisa.
Ilipokonywa makoloni yake pia kama Tanganyika.
Katika Mapunduzi ya Ujerumani ya 1918-1919, nchi ikaweza kuwavua haki ya kutawala familia za kifalme na Maaskofu katika miji tofauti ya Ujerumani na kuifanya nchi kuwa ya kidemokrasia ya Jamhuri ya Weimar.
Luther alipinga haki ya Papa kukusanya pesa mjini kwake. Papa alikuwa anauza hati za misamaha.
Aliamini kuwa misamaha inatolewa na Mungu, siyo mtu. Alichukizwa na Johan Tetzel, aliyotumwa na Papa kwenda Ujerumani kuuza hati za misamaha, ili achangishe pesa za kujenga Kanisa la St. Peter's huko Rome.
Akapinga haki ya kuchangisha hasa kwa wananchi masikini wakati Rome ni tajiri sana na kubandika sababu zake katika mlango wa kanisa la chuo chake. Hizo pingamizi ndizo zikajulikana kama "95 Theses".
Alikuwa hapingi utawala wa Rome kisiasa nchini kwake kwa kuwa Ujerumani ilikuwa siyo nchi kamili bali vitongoji tofauti na chini ya utawala wa kifalme, Maaskofu na Duke.
Alipinga tabia ya Rome ya kuchangisha pesa kwa kuuza hati ya misamaha ya dhambi za binadamu, duniani.
Kwahyo Mkuu huyu mfale George alfanikiwa kuoa mke wa pili na vp Anglicans wanaruhusu hil la kuoa wake wawil? Msaada wako mkuuView attachment 325084
Mkuu Amavubi huko unakotaka kwenda kwenye mambo ya Anglicana,Lutheran ni kuleta mada mpya,kwanza kujadili mambo hayo inabidi uwe "umeiva" kiimani,usije "ukaasi" kanisa lako.
Kiufudi hizi dini ni "utamaduni",sisi Waafrika tuliletewa tu na wamisionari..lkn dini hutambulisha utamaduni wa mtu.Martin Luther alipoona nchi yake ya Ujrumani haitambuliki na Papa aliye Rome Italy anatoa amri ambayo mpaka wao Ujerumani wanaitii akaona ni kama "utumwa",ndio maana akasema lazima aondoe ile "Papacy Authority",kwamba kwanini kila kitu kitoke Vatican,yaani kwa lugha nyingine ni kuwa kwanini kila kitu atoe amri Mtaliano??Akaamua kuanzisha dhehebu lake na akalipa jina lake,yeye akiitwa Martin Luther basi kanisa lake liitwe "Lutheran" i.e "Of the Luther".Lengo ni kuondokana na mamalaka ya Vatican chini ya mtaliano na kukuza utaifa wao wa Ujeruman,na ndio maana makao makuu ya Lutheran yakawa Ujerumani...Ulutheri ni alama ya utamaduni wa Mjerumani,alihitaji "identity" yake na akaipata.
Mfalme George VIII wa Uingereza,akiwa muumini safi wa kanisa katoliki,akataka kuoa mke mwingine aachane na Catherine of Aragon,lkn sbb kanisa katoliki hurusiwi kuoa mke mwingine wakati mmoja yupo akakataliwa na Papa.Mfalme akaona Papa anamuingilia mpaka kwenye "ufalme" wake,akaamua kuanzisha kanisa akaliita "Anglican Church" toka neno "Anglo",maana Anglo= England,hivyo Anglican Church maana yake kanisa la England,akajitoa mikononi mwa "Papacy Authority" ili na yeye awe na kanisa lenye utamaduni wao.Anglican Church likawa kanisa la nchi,Mkuu wake ni malkia na kiongozi wake wa kiroho ni askofu wa Canterbury,hii ikawa ni alama ya Uingereza na utamaduni wao,ikawa kama wewe si Muanglicana basi huwezi kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza,wakaweza kuanzisha kanisa la utamaduni wao...Dini ni utamaduni
Huku Afrika kuna watu walijaribu kaunzisha makanisa yenye ukristo wa kiafrika,maana waliona kabisa kuwa YESU WA AFRIKA ana tofauti sana na YESU WA ULAYA..kwamba inapswa tuwe na ukristo unaoakisi utamaduni wetu maana dini ni utamaduni,Congo ya Zaire akatokea mtu anaitwa SIMON KIMBANGU akaanzisha kanisa lake akaliita "KIMBANGUISM"...alifanya miujiza na kuponya watu na magojwa,kutibu ukoma na miujiza kibao,Kimbangu akawa na waumini wake lukuki walioukimbia Ukatoliki na Uprotestanti,hii iliwatisha wamisonary wakashitaki kwa serikali ya kikoloni,Simon akakamatwa na kushitakiwanbila kupewa nafasi ya kujitetea,kanisa lake likakuwa na kudidimiza "UKRISTO WA ULAYA" wa wakatoliki na protestanti.Waumini wake wakakamatwa na serikali ya kikoloni ya mbeligiji na wakateswa na wengine kupelekwa "exile" ili kuuwa mshikamano wao.Kimbangu alifia gerezani,dhamira yeke ilikuwa kama ile ya Martin Luther na Mfalme George VII,kuanzisha dhehebu linaloakisi utamaduni wake,yaani utamaduni wa muafrika..Isingekuwa fitna za Mkatoliki na mprotestanti kwa kushirikiana na serikali katili ya mbeligiji,leo hii Afrika nasi tungekuwaa na dini ya "YESU WA KIAFRIKA"....Kwa hiyo ndugu Amavubi bhizi dini ni utamaduni...Umasikini wetu na nguvu za ukoloni zilituzuia kuimarisha dini zinazoendana na utamaduni wa kiafarika.Kwenye picha hiyo,Simon Kimbangu ni huyo aliyevaa shuka
Ndio alioa mkuu,alifanya hivyo kwa "maslahi" yake tu ya muda,baadae ikawa ninmume mmoja kwa mke mmoja.Anglikani hawana ruhusa hiyo ya kuowa wake wawiliKwahyo Mkuu huyu mfale George alfanikiwa kuoa mke wa pili na vp Anglicans wanaruhusu hil la kuoa wake wawil? Msaada wako mkuu
Duu asante kwa kunifahamisha mkuuNdio alioa mkuu,alifanya hivyo kwa "maslahi" yake tu ya muda,baadae ikawa ninmume mmoja kwa mke mmoja.Anglikani hawana ruhusa hiyo ya kuowa wake wawili
HV huu utamadun Wa kuuza hati ya msamaha Wa dhamb had Leo upo au?
Duuuh, Mkuu kwel ndo maana wanasema dini nHaupo Mkuu, ila Wakatoliki wanaamini kuwa madhambi yao yanafutika wakitoka katika "confession" na Padri/ Askofu/ Papa.
Can the priest forgive all sins in the Sacrament of Penance (confession):
A. The priest has the power to forgive all sins in the Sacrament of Penance, but he may not have the authority to
forgive all.
To forgive sins validly in the Sacrament of Penance, two things are required:
1. The power to forgive sins which every priest receives at his ordination, and
2. The right to use that power which must be given by the bishop, who authorizes the priest to hear
confessions and pass judgment on the sins.
source:catholicnewsagency.com
Duuuh, Mkuu kwel ndo maana wanasema dini n
iman
Ndio alioa mkuu,alifanya hivyo kwa "maslahi" yake tu ya muda,baadae ikawa ninmume mmoja kwa mke mmoja.Anglikani hawana ruhusa hiyo ya kuowa wake wawili