Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hao wanaoana jinsia mbili tofauti lakini ulaya na Marekani wanaoana jinsia moja pia.
Mfumo Kristo bado mkubwa lakini upo katika ushindani mkubwa na mfumo wa Kiislamu na dini nyingine katika nchi magharibi.
Kila nchi zinavokuwa matajiri, watu wanapungua kuzaa na dini inapungua nguvu kwa kiasi fulani. Ukiangalia Spain, Italy, Marekani, Uiingereza au Ujerumani, hukuti watu wengi wanakwenda makanisani kwa mfano. Ni tofauti na Ufilipino au Wakristo wa Indonesia wanaojaza makanisa kila jumapili.
Wageni wengi wa nchi za Kiislamu wanaohama wenyewe au kutokana na vita ni wengi Ulaya na Marekani.
Ukienda Detroit, New York , London, au Toronto, utawakuta wengi tu.
Hao wanakuja na familia kubwa au wanazaa zaidi kuliko wazawa. Na dini ya Kiislamu inakuwa japo pia kuna watu wengi huko bado hawaamini Mungu (atheists).
Ukienda Toronto, New York au London, utakuta Waislamu wanaswali katika misikiti ambayo zamani yalikuwa makanisa.