Majina ya sura zote 114 za Quran Tukufu kwa Kiswahili


Wewe ni mwalimu mimi ni mchangiaji nakuhoji kwenye kitabu chako na imani yako ili nipate ufahamu.

Umesema Quran ni maneno ya Mungu.
Ni maneno ya Mungu kwa nini
a) Binadamu
b) Majini
c) Binadamu na majini
Weka aya
 
Kwa hiyo mtume hakuonana nao.
Walisilimishwa na nani au alisilimisha vitu ambavyo hakuonana navyo?
Weka maelezo vizuri ukiweka na aya itapendeza
Majini hauwezi kuwaona Kwa maumbo Yao Kwa hyo aliongea nao.ndo wakasilimu.
Unapata shida wapi?
 
Je kuna majini mema yanakaa ndani ya mtu mwema kama muislam mcha Mungu?
Maana naona unayaongelea hatika hasi wakati Quran inasema kuna majini hasi na chanya.
Kama hauna control na uadilifu wa majini. Kwa nini uamini vitu ambavyo hauna control navyo na huvioni. Hauoni ni busara zaidi katika visivyoonekana ubaki na Mwenyezi Mungu tu ambaye unauhakika naye kuliko kujihusisha na vitu ambavyo hujui kama vinadanganya au vinaigiza kusilimu

Huoni kama kuongeza majini kwenye imani yako ni kuhatarisha imani?
 
Nitasoma tena majibu haya ni mazuri sana.
Labda teacher nadharia twende kwenye uhalisia.

Wewe binafsi unarafiiki yoyote mmoja au kumi au millioni na jini/majini waislam wenzako ambao wamesilimu.
Hii itasaidia kukuhoji maswali halisi zaidi
 
Majini hauwezi kuwaona Kwa maumbo Yao Kwa hyo aliongea nao.ndo wakasilimu.
Unapata shida wapi?
Ngoja nirudie tena kusoma surat jin yote wenda nitapata picha.

Wewe umewahi kuongea nao kama mtume wakiwa wanasauti tu bila mwili wala kuingilia mwili wa kitu?
 
Takhbiiiiiirrrr
 
Ngoja nirudie tena kusoma surat jin yote wenda nitapata picha.

Wewe umewahi kuongea nao kama mtume wakiwa wanasauti tu bila mwili wala kuingilia mwili wa kitu?
Kwani hauoni hata kwenye movie watu wanaongea na majini?
Unadhani wachawi wanaongea vipi na viumbe visvyoonekana?
 
Kwani hauoni hata kwenye movie watu wanaongea na majini?
Unadhani wachawi wanaongea vipi na viumbe visvyoonekana?
Uliwahi kufanikiwa kuonea nalo moja mawili au milioni yakiwa katika free state. Na uliongea na majini matakatifu au majini madhambi?
 
Je kuna majini mema yanakaa ndani ya mtu mwema kama muislam mcha Mungu?
maswali yako yanazidi kuonyesha kuwa bado hujajua tofauti kati ya "Kuamini uwepo wa kitu" na "Kujihusisha nacho kijamii au kiibada." Naomba nikufungue macho kwa hoja hizi tatu zilizoambatana na aya zake:

Jibu ni HAPANA . Jini mwema, mcha Mungu na mwenye adabu, hawezi kamwe kuingia ndani ya mwili wa binadamu mwema wala mbaya. Kuingia ndani ya mwili wa mwanadamu na kumfanya apagawe, apoteze fahamu, au kuingilia faragha zake ni dhuluma kubwa na kosa la jinai kimaumbile.
Jini mcha Mungu anaijua Quran na anajua kuwa kufanya hivyo ni haramu na ni kuvuka mipaka. Kwa hiyo, majini yote yanayoingia miilini mwa watu (iwe wanajiita majini subiani, masharifu, au majini mahaba) yote ni majini mabaya, waasi, na waongo (mashetani), hata kama yatakuja yakijifanya yanasoma Quran au yanataja majina ya kitajiri. Jini mwema anaishi katika ulimwengu wake kwa amani na anafanya ibada zake huko huko bila kubughudhi wanadamu.
 
Kwa nini uamini vitu ambavyo hauna control navyo na huvioni. Hauoni ni busara zaidi katika visivyoonekana ubaki na Mwenyezi Mungu tu ambaye unauhakika naye kuliko kujihusisha na vitu ambavyo hujui kama vinadanganya au vinaigiza kusilimu
hapa ndipo unapokosea kiitikadi. Sisi Waislamu hatujihusishi na majini, hatuombi msaada kwao, hatufanyi nao biashara, na wala hatuhitaji kuwa-control.

Uislamu unatukataza katakata kujihusisha nao! Sisi tunabaki na Mwenyezi Mungu tu kama ulivyosema.
Lakini, kuamini uwepo wao (kwamba wapo duniani) sio uchaguzi wetu wa kibinadamu; ni agizo la Mwenyezi Mungu aliyewaumba. Mungu mwenyewe ndiye aliyetuambia kwenye Quran kuwa amewaumba viumbe hao. Katika Surah Adh-Dhariyat (51:56), Allah anasema wazi kabisa:

"Nami kisha kuwaumba majini na watu ila waniabudu Mimi."
Sasa mkuu, kama Mungu aliyekuumba anakuambia: "Nimeumba na viumbe wengine wanaitwa majini lakini nimewaweka mbali nanyi, msijihusishe nao", wewe unakataaje uwepo wao?

Ukisema hauamini kama wapo, unakuwa unamwambia Mungu anadanganya, na hapo ndipo unapoharibu imani yako. Sisi tunawaamini kama tunavyoamini uwepo wa virusi vya Corona au wadudu wa bakteria—hatuwaoni, hatuna control nao, lakini tunajua wapo na tunajikinga nao kwa kufuata miongozo [Surah Al-Jinn (sura nambari 72)].
 
Huoni kama kuongeza majini kwenye imani yako ni kuhatarisha imani?
Sisi hatujawahi "kuongeza" majini kwenye imani (Aqeedah) yetu. Kwenye Nguzo za Imani za Kiislamu ziko sita:

(1) Kumwamini Allah, (2) Malaika wake, (3) Vitabu vyake, (4) Mitume wake, (5) Siku ya Kiyama, na (6) Qadari (Majaaliwa).

Hakuna nguzo inayosema 'Kuamini Majini'
.

Sisi tunaiamini Quran yote kama neno la Mungu lililonyooka. Ndani ya Quran kuna surah nzima inaitwa Surah Al-Jinn. Katika Surah Al-Baqarah (2:85), Allah anatoa onyo kali kwa watu wanaochagua kuamini baadhi ya vitu kwenye Kitabu na kukataa vingine, anasema:


sisi hatutafuti urafiki wa majini, hatuhangaiki kujua kama wanadanganya kusilimu au la, kwa sababu maisha yetu hayategemei wao. Sisi tunamtegemea Allah pekee. Kujua kuwa wapo kunatusaidia tu kujua jinsi ya kujilinda na mitego yao (uchawi na ushirikina) kwa kutumia Quran, basi!
 
Waongezee na hii Waislam wanamubudu Muhammad kwani kwenye swala lazima wamsalimie wanapochukua shahada.
hapo umeenda chaka kabisa na umeonyesha hujui hata maana ya neno "Kuabudu" (Worship).

Kwenye swala na kwenye Shahada, sisi hatumuabudu Mtume Muhammad (S.A.W), bali tunamshuhudia kuwa yeye ni Mtume na Mtumishi (Mja) wa Mwenyezi Mungu, na tunamtakia amani (salamu). Na ndio maana maneno yenyewe ya Shahada yanasema hivi:

"Nashuhudia kuwa hapana mungu anaepaswa kuabudiwa kwa haki ila ALLAH, na nashuhudia kuwa Muhammad ni MTUME wake."
Kama tungekuwa tunamuabudu, tungesema yeye ni Mungu. Lakini tunasema yeye ni Mtume.

Kumtakia amani na rehema kiongozi wako (kama unavyoweza kumwombea heri rais wako au mzazi wako) sio kumuabudu.

Katika Uislamu, ibada zote—kusujudu, kuomba, na kuchinja—ni kwa ajili ya Allah pekee [Surah Adh-Dhariyat (51:56)].

Mtume Muhammad (s.a.w) ni mwanadamu na kiumbe kama sisi, ila yeye kapewa utume wa kutuongoza. Usichanganye kumheshimu Mtume na kumuabudu Mungu!...Tumeelewana?




 
Unamsalimia marehemu kwenye swala?
 
Unamsalimia marehemu kwenye swala?
unauliza "Unamsalimia marehemu kwenye swala?" kwa mshtuko kana kwamba ni jambo la ajabu, lakini ukweli ni kwamba NDIO, tunamsalimia, na hakuna kosa lolote kiakili wala kidini kufanya hivyo.
Inaonekana bado unachanganya kati ya "Kumsalimia mtu" na "Kumuabudu mtu."
  • Kumsalimia mtu: Ni kumtakia amani na rehema kutoka kwa Mungu (kusema 'Amani iwe juu yako'). Hata wewe ukienda makaburini kumsalimia ndugu yako aliyefariki au ukimwombea dua haimaanishi kuwa unamuabudu.
  • Kumuabudu mtu:
    Ni kumsujudia, kumwomba yeye shida zako, au kuamini yeye ndiye anayeamua hatimani yako. Sisi kwenye swala hatumwombi Muhammad (S.A.W) atusaidie shida zetu; tunamwomba ALLAH ampe amani Mtume wake.

Maneno yenyewe tunayosoma kwenye Tahiyatu yanasema: “As-salamu ‘alayka ayyuhan-nabiyyu wa rahmatullahi wa barakatuh” (Amani iwe juu yako ewe Nabii, na rehema za Allah na baraka zake). Hii ni dua ya kumtakia amani kiongozi wetu aliyetufikishia ujumbe wa Mungu.

Mbona ninyi mkisema "Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi" hamsemi mnamuabudu huyo marehemu? Mbona mnamwombea Mungu ampe amani?

Kumtakia mtu amani (kumsalimia) akiwa hai au amekufa ni amri ya Mungu, lakini Ibada nzima inabaki kuwa ya ALLAH pekee [Surah Adh-Dhariyat (51:56)].

Acheni kukariri hoja za kusikia vijiweni .




 
AI inaharibu uwezo wako wa kuchanganua mambo.
 
Wewe ni mwalimu mimi ni mchangiaji nakuhoji kwenye kitabu chako na imani yako ili nipate ufahamu.

Umesema Quran ni maneno ya Mungu.
Ni maneno ya Mungu kwa nini
a) Binadamu
b) Majini
c) Binadamu na majini
Weka aya
swali lako sijalielewa naomba ulirekebishe ili nipate kukujibu inshaAllah
 
Hiyo kauli ya kumtakia mtu Mungu amlaze mahali Sema peponi usifananishe na salamu kila siku mnayofanya kumsalimia marehemu Muhammad kwenye swala.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…