Mwaka wa Mbele
JF-Expert Member
- Mar 5, 2026
- 1,013
- 3,017
unauliza "Unamsalimia marehemu kwenye swala?" kwa mshtuko kana kwamba ni jambo la ajabu, lakini ukweli ni kwamba NDIO, tunamsalimia, na hakuna kosa lolote kiakili wala kidini kufanya hivyo.
Inaonekana bado unachanganya kati ya "Kumsalimia mtu" na "Kumuabudu mtu."
- Kumsalimia mtu: Ni kumtakia amani na rehema kutoka kwa Mungu (kusema 'Amani iwe juu yako'). Hata wewe ukienda makaburini kumsalimia ndugu yako aliyefariki au ukimwombea dua haimaanishi kuwa unamuabudu.
- Kumuabudu mtu:
Ni kumsujudia, kumwomba yeye shida zako, au kuamini yeye ndiye anayeamua hatimani yako. Sisi kwenye swala hatumwombi Muhammad (S.A.W) atusaidie shida zetu; tunamwomba ALLAH ampe amani Mtume wake.
Maneno yenyewe tunayosoma kwenye Tahiyatu yanasema: “As-salamu ‘alayka ayyuhan-nabiyyu wa rahmatullahi wa barakatuh” (Amani iwe juu yako ewe Nabii, na rehema za Allah na baraka zake). Hii ni dua ya kumtakia amani kiongozi wetu aliyetufikishia ujumbe wa Mungu.
Mbona ninyi mkisema "Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi" hamsemi mnamuabudu huyo marehemu? Mbona mnamwombea Mungu ampe amani?
Kumtakia mtu amani (kumsalimia) akiwa hai au amekufa ni amri ya Mungu, lakini Ibada nzima inabaki kuwa ya ALLAH pekee [Surah Adh-Dhariyat (51:56)].
Acheni kukariri hoja za kusikia vijiweni .
Umenifanya Nifikirie hii hoja.
Kwanini mwenyezi Mungu na Malaika wanamswalia mtume?.