Mwaka wa Mbele
JF-Expert Member
- Mar 5, 2026
- 1,013
- 3,017
unauliza "Unamsalimia marehemu kwenye swala?" kwa mshtuko kana kwamba ni jambo la ajabu, lakini ukweli ni kwamba NDIO, tunamsalimia, na hakuna kosa lolote kiakili wala kidini kufanya hivyo.
Inaonekana bado unachanganya kati ya "Kumsalimia mtu" na "Kumuabudu mtu."
- Kumsalimia mtu: Ni kumtakia amani na rehema kutoka kwa Mungu (kusema 'Amani iwe juu yako'). Hata wewe ukienda makaburini kumsalimia ndugu yako aliyefariki au ukimwombea dua haimaanishi kuwa unamuabudu.
- Kumuabudu mtu:
Ni kumsujudia, kumwomba yeye shida zako, au kuamini yeye ndiye anayeamua hatimani yako. Sisi kwenye swala hatumwombi Muhammad (S.A.W) atusaidie shida zetu; tunamwomba ALLAH ampe amani Mtume wake.
Maneno yenyewe tunayosoma kwenye Tahiyatu yanasema: “As-salamu ‘alayka ayyuhan-nabiyyu wa rahmatullahi wa barakatuh” (Amani iwe juu yako ewe Nabii, na rehema za Allah na baraka zake). Hii ni dua ya kumtakia amani kiongozi wetu aliyetufikishia ujumbe wa Mungu.
Mbona ninyi mkisema "Mungu amlaze marehemu mahali pema peponi" hamsemi mnamuabudu huyo marehemu? Mbona mnamwombea Mungu ampe amani?
Kumtakia mtu amani (kumsalimia) akiwa hai au amekufa ni amri ya Mungu, lakini Ibada nzima inabaki kuwa ya ALLAH pekee [Surah Adh-Dhariyat (51:56)].
Acheni kukariri hoja za kusikia vijiweni .
Sio tu Binadamu.Hiyo kauli ya kumtakia mtu Mungu amlaze mahali Sema peponi usifananishe na salamu kila siku mnayofanya kumsalimia marehemu Muhammad kwenye swala.
AI inaharibu uwezo wako wewe wa kujibu hojaAI inaharibu uwezo wako wa kuchanganua mambo.
Tatizo lako lipo kwenye nini hasa? maana hiyo attahiyat kaifundisha mwenyewe Mtume Muhammad (pbuh ) yungali hai kwani ni maelekezo ya Mungu ametaka sala iswaliwe hivyo. Na yeye ndiye aliyesema kuwa salini kama mnavyoniona nikiswali.Hiyo kauli ya kumtakia mtu Mungu amlaze mahali Sema peponi usifananishe na salamu kila siku mnayofanya kumsalimia marehemu Muhammad kwenye swala.
Hoja ni mna muabudu Muhammad ndomana lazima mumtaje kwenye swala zenu kila siku wakati yeye kashakufa na ni marehemu kama mngekua mnamuabudu Mungu wa kweli msingemtaja marehemu kwenye ibada zenu kila siku maana huo ni paganism.unaleta Ad hominem attack baada ya kushindwa hoja
Hiki kituko!AI inaharibu uwezo wako wewe wa kujibu hoja
Kwamba mungu anataka mohammad waswaliwe pamoja! huu mtihani sheikh.Tatizo lako lipo kwenye nini hasa? maana hiyo attahiyat kaifundisha mwenyewe Mtume Muhammad (pbuh ) yungali hai kwani ni maelekezo ya Mungu ametaka sala iswaliwe hivyo. Na yeye ndiye aliyesema kuwa salini kama mnavyoniona nikiswali.
Waislam hawakuanza kuswali baada ya kufa kwa Mtume Muhammad (pbuh) .
tuelezee kwa upana zaidi.AI inaharibu uwezo wako wewe wa kujibu hoja
tuelezee kwa upana zaidi.
Kivipi kumswalia mtume kunafuta madhambi yako kumi?.
Tatizo lako lipo kwenye nini hasa? maana hiyo attahiyat kaifundisha mwenyewe Mtume Muhammad (pbuh ) yungali hai kwani ni maelekezo ya Mungu ametaka sala iswaliwe hivyo. Na yeye ndiye aliyesema kuwa salini kama mnavyoniona nikiswali.
Waislam hawakuanza kuswali baada ya kufa kwa Mtume Muhammad (pbuh) .
ALLAH anasema hivi katikaKwanini mwenyezi Mungu na Malaika wanamswalia mtume?.
Mtume ﷺ amesema: “Atakayeniswalia mara moja, Allah atamswalia mara kumi, atamfutia madhambi kumi na atamuinulia daraja kumi.”
Maana yake ni kwamba kumswalia Mtume ﷺ, kama kusema “Allahumma salli ‘ala Muhammad”, ni ibada yenye thawabu kubwa. Allah humlipa mwenye kufanya hivyo kwa rehema, kufutiwa madhambi madogo, na kuinuliwa daraja.
Hata hivyo, madhambi makubwa yanahitaji toba ya kweli, na haki za watu zinahitaji kurejeshwa au kusamehewa.
Vitabu vya mchongo hivi😊😆
Devils work kwa ajili ya devilish cult.
Dawa yenu tunayo
View attachment 3683235
nimejibu swali lako hapo juuKwamba mungu anataka mohammad waswaliwe pamoja! huu mtihani sheikh.
kwani wewe unashindwa kitu gani ??Iweke na hii kwa AI.
Je Yeye ni mkosaji sana?..
Kwanini aliamuru kila muislam amswalie? .
Pia kwanini aliamuru Hadi anayemsamehe dhambi pamoja na malaika wake. Na wenyewe wamswalie?
Mm sijasema kumuabudu.ALLAH anasema hivi katika
Quran 33:56
"Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu."
Ngoja nikufafanulie maana yake kwa mujibu wa tafsiri ya wanazuoni kama Ibn kathir na As-saadi.
Neno lililotajwa katika aya ni "(Yusswalluna) ina maana wanamsalia.
Kwa mtu usiyejua lugha ya kiarabu lazima ujichanganye. Neno swala lina maana tofauti linapotumiwa na Mungu, Malaika na binadamu.
Mungu anapotamka kumswalia haimaanishi kuwa anamsujudia au kumpigia magoti Muhammad la hasha.
Hapa ana maana ya Kumsifu Mtume mbele ya Malaika wakuu, kumrehemu, na kumtukuza cheo chake.
Neno kumswalia Linapotumiwa na Malaika lina maana ya Kumuombea dua ya msamaha, rehema, na kumtakia heri Mtume Muhammad (s.a.w).
Neno hili tunapolitumia waumini wa kiislam lina maana ya Kumuomba Mungu amshushie amani na baraka Mtume wake.
Neno moja la kiarabu ila lina maana na matumizi tofauti. Kwako wewe usiyeijua hii lugha unaona kuswalia ni kumwabudu. Jambo ambalo si sahihi.
Mm sijasema kumuabudu.
Nashangaa tu kuwa allah nae anaungana na malaika wake kumuombea msamaha mohames kwa allah na malaika wake. 😎😎😎
Hauko serious kama unafikiri ntafungua hiyo Link.