Huwa napata mtihani sana kwani kituo changu cha daladala kinaitwa SAMAKI kiko hapa Mbezi Beach
Mara nyingi tukikaribia kufika utasikia konda anauliza Samaki wapo?
Dah, napata mtihani sana kusema TUPO...... (maana infwakiti mimi sio samaki ni mtu) BAHATI MBAYA ABIRIA WENGINE ILI ASIPITISHWE UTASIKIA SHUSHA SAMAKI
Je unajua kituo gani kingine ambacho ni "mtihani"?
Shinyanga kuna kijiji kinaitwa kagongwa lakini ina vituo viwili ndani yake,kagongwa mbele na kagongwa nyuma.......