Majina ya vituo vya daladala sehemu mbalimbali


Shinyanga kuna kijiji kinaitwa kagongwa lakini ina vituo viwili ndani yake,kagongwa mbele na kagongwa nyuma.......
 
Utasikia:

Vijana wapo? (Pale Vijana Kinondoni), na utasikia wazee na mvi zao wanaitikia: Tupo!
Pale Mbagala St. Mary's utasikia watu wakisema "Shusha kokoto".
 
Kuna vituo viwili barabara ya mazimbu moro... Kimoja ni kitimoto na kingine maziwa... Sasa ikiulizwa, ...maziwa mpo? au kitimoto mpo? dah... inakuwa noma
 
Buguruni kuna kituo kinaitwa malapa....basi gari ikikaribia kufika utamsikia konda anasema "malapa mpo? au anasema"wale wa malapa njooni mshuke",basi inakuaga balaa...
 
Kilometa Saba njia ya kwenda Amani kutokea Muheza, utamsikia konda anasema Kilometa mpo? Jamaa wanajibu shusha Kilometa.
 
Dodoma: kituo kinaitwa wajenzi. Basi konda anauliza "wajenzi wapo?", raia wanaoshuka utawasikia tupo; hata kama wao ni manesi, walimu, wazururaji n.k.

Dar: kituo kinaitwa madukani. Basi konda anauliza, "maduka mpo?" raia utawasikia tupo!!

Dar: kituo kinaitwa manyanya. Konda anauliza, "manyanya mpo?", raia wanaoshuka, utawasikia, tupo!!

Hivi itakuwaje pale muisrael atapotumia daladala kwenda kwa mwenyeji wake anayekaa Sinza Palestina?!? Ishu itakuwa balaa pale konda atakapouliza raia, Palestina hamshuki? Muisrael atasema shusha Palestina kweli?!
 
Njia ya mwenge-tegeta vituo vingi majina yake yanautata,utasikia konda akisema,Tanki bovu raia watajibu,shusha
makonde? Raia wanajibu:shusha
jogoo?
Samaki?
 
njia ileile kuna kwa mti mkavu na pia kuna kwa mchumia juani
 
mwananyamala kuna kituo kinaitwa KWA MAMA ZAKARIA[color]utaskia konda anaita kwa mama.....Mama zakaria mpo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…