15 January 2022
Taarifa toka makao makuu ya CCM Dodoma pia kutoka Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba na Afisi ya CCM Kisiwandui Unguja Zanzibar .
Wanachama wa CCM wanaotia nia kugombea nafasi ya uspika baada ya Spika Job Y Ndugai kujiuzulu
January 2022 ni hawa wafuatao :
- Andrew Chenge : mwanasheria mkuu wa serikali wa zamani
- Sophia Mathayo Simba
- Dr. Mussa Shafii Ngonyani
- Wakili Faraji Rushagama
- Rahmaddin Rashid Ismaili
- Hamisi Rajabu
- Festo John Kipate
- George Francis Nangale
- Barua Abdi Mwakilanga
- Zahoro Rashid Hanuna
- Thomas David Kirimbunyo
- Angelina Bello John
- Eng. Abdulaziz Jahad Hussein
- Dr. Tulia Ackson : Naibu spika chini ya Job Ndugai
- Dr. Thomas Kashililah : katibu wa bunge wa zamani
- Stephen Masele : naibu spika wa zamani Bunge la Afrika
- Mussa Azzan Zungu : meya wa zamani wa Ilala Dsm.
- Joseph Musukuma :
- Ezekiel Maige : waziri wa zamani
- Asia Juma Abdallah : mkuu wa wilaya wa zamani
- Dr. Titus M. Kamani : waziri wa zamani
- Tumsifu Mwasamale : Afisa Maendeleo ya vijana mkoa wa Dodoma
- Prof. Handley Mpoki Mafwenga : mtumishi wa serikali / umma
- Goodluck Mlinga : mbunge wa zamani wa CCM
- Prof. Norman Adamson Sigala
- Hatibu Madata Mjega :
- Dr. Linda Salekwa Ole Saitabau
- Emmanuel Simon Sindama
- Bi. Uwesu Msumi
- Hilal H. Seif
- Wakili Emmanuel Paul Mngare
- Athumani Mfutakamba
- Wakili Nduruma Majembe
- Mwenda Burton Mwenda
- Henry Erasto Kessy
- Josephat Malima
- Adam Nyanyavanu
- Eng. Stella Manyanya
- Andrew Kevella
- Luhanga Mpina
- Hussein Migoda Mattaka
- Dr. Godwin Maimu
- Mohammed Ali Mmanga
- Esther Stefano Makazi
- Comrade Amos Sollo
- Godwin Kunambi - mkurugenzi wa zamani wa jiji la Dodoma
- Goodluck ole Medeye
- Juma Hamza Chumu
- Baraka Omari Baibato
- Hamidu Chamani
- Fikiri Saidi : mkuu wa wilaya wa zamani
- Bi. Dotto Balele Mgasa
- Wakili Onyango Otieno
- Eng. Samuel Hayuma
- Merkion Ndofi
- Abwene Majula
- Patrick Nkandi
- ..
- ..
- ..
- ..
- ..
Toka Kumbukumbu mwaka 2015 :
waliogombea nafasi ya uspika toka vyama mbalimbali walikuwa wanane (8) tu
WALIOPITISHWA NA VYAMA VYA SIASA KUGOMBEA NAFASI YA USPIKA 2015
Jumla ya wagombea nane (8) wamejitokeza kugombea kiti cha Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Katibu wa Bunge, Dkt Thomas Kashilillah amesema, “nimepokea majina nane kutoka vyama nane vya siasa watakaogombea nafasi ya Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano .”
Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni, Mhe. Peter Leonard Sarungi kutoka chama cha Alliance for Tanzania Party (AFP), Mhe. Hassan Kisabya Almas kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Dkt. Godfrey Rafael Malisa kutoka Chama cha Kijamii (CCK), na Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wengine ni Mhe. Goodluck Joseph Ole Medeye kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Richard Shedrack Lyimo kutoka Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Hashim Spunda Rungwe kutoka CHAUMMA na Mhe. Robert Alexander Kasinini, Chama cha Democratic Party (DP).
Kwa mujibu wa Dkt Kashilillah, uchaguzi wa Spika utafanyika kesho tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mbali na kutaja majina ya wagombea wa Spika wa Bunge, Dkt Kashilillah amesema mpaka tarehe 16/11/2015 jumla ya wabunge 348 wamekwisha sajiliwa.
Aidha Dkt Kashilillah amesema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mkutano wa 11 wa bunge yamekamilika.
Katika mkutano huo wa kwanza wa bunge la 11, kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo kumchagua Spika, Naibu Spika na kuthibitisha jina la Waziri Mkuu
Source :
Parliament of Tanzania