Majina ya wanaCCM waliochukua fomu za Uspika

Majina ya wanaCCM waliochukua fomu za Uspika

Ni nini sababu za wanaCCM wote hawa kujitokeza mwaka huu 2022 kugombea nafasi ya uspika kupitia chama chao,

  • Je ni ongezeko la demokrasia ndani ya chama cha CCM ?
  • Kutoridhika kwa mwenendo wa Bunge kuburuzwa
  • Wagombea hawa 2022 katika makumi uspika ni dalili mtifuano ndani ya CCM kwa nafasi zote udiwani na ubunge 2025
  • Chama kimeshindwa kudhibiti nidhamu ya wanachama kujipima kikweli kweli wao wenyewe binafsi kuwa "wanatosha" kuwania uongozi ?
  • N.k
Kwa maoni yangu sababu zaweza kuwa;

1. Pamoja na uhuru uliotolewa ktk katiba bado umeacha mwanya mkubwa wa kukipa hadhi kiti cha Spika kwa vigezo/sifa za ziada mfano, kiwango cha elimu na nyanja ya ubebezi, umri, na uzoefu nk.

2. Kushushwa hadhi ya kiti chenyewe na Spika aliye jiuzulu hivyo Kila mtu kuona anao uwezo wa kuliongoza bunge maana alionekana nyakati nyingi akishindwa kufuata kanuni na kuwa kama mazoea.

3. Katika chama (ccm) inaonekana sasa ni fursa yao ya kuneemeka kwa kukusanya fedha nyingi kwa viongozi walio ktk idara ya siasa na uenezi na hii si kwamba ni demokrasia kama wanavyotaka kuhadaa watu maana ktk mchakato ndani ya chama wengi watakatwa bila kupiga kura wala maelezo ili kupata wawili/watatu wa kuzugia tu. Ndiyo maana inapigiwa promo sana ili wakachukue wengi na baadae watapigia debe kwa kuteleza kuwa huku chama kina hazina ya viongozi.

4. Baadhi ya vijana wapya wa ccm na wale waliosahaulika ktk teuzi mbalimbali wanatumia fursa hii kujitambulisha wakidhani kuwa kamati kuu/ halmashauri zitajisumbua kuwajadili jambo ambalo halipo maana tayari mteule wa kiti alishajadiliwa na kupitishwa hizi zilizobaki ni sanaa za kiitifaki tu.
 
Naunga mkono hoja
P
Tulia anafaa kwani ameshapata uzoefu
 
Ni aibu , hebu waweke mavyeti yanayohitajika ili uweze kuwa spika au ni sawa na ubunge hata ukiwa zuzu unakubalika ?
 
Washaingiza kama million57 za haraka haraka...

Wameruhusiwa kula ila wasivimbiwe...
 
Mwenda. Burton Mwenda alias Mwijaku
Ila jamani watanzania kupitia zoezi hili la kujaza nafasi ya uspika, tumeonesha jinsi tusivyokuwa serious na mambo yetu. Nafasi muhimu kama ya spika inafanyiwa utani wa kiwango kile, kupitia tukio hili ni dhahiri kuwa:

1. Mambo yetu mengi ya kitaaluma mtindo ni huu huu....... tunazalisha wasomi kwa vyeti lakini practically hamna wasomi
2. Uchumi wetu ni hoi, mbali na natuaral resources endowments zote tulizonazo...... tunaendelea kupambana na madawati na vyoo karne ya 21
3. Siasa zetu ni jokes, tuna sheria ya vyama vingi lakini nchi inaongozwa na chama kimoja miaka yote na opposition imejifia na haiwezi kujenga hoja
 
15 January 2022
Taarifa toka makao makuu ya CCM Dodoma pia kutoka Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba na Afisi ya CCM Kisiwandui Unguja Zanzibar .

Wanachama wa CCM wanaotia nia kugombea nafasi ya uspika baada ya Spika Job Y Ndugai kujiuzulu January 2022 ni hawa wafuatao :
  1. Andrew Chenge : mwanasheria mkuu wa serikali wa zamani
  2. Sophia Mathayo Simba
  3. Dr. Mussa Shafii Ngonyani
  4. Wakili Faraji Rushagama
  5. Rahmaddin Rashid Ismaili
  6. Hamisi Rajabu
  7. Festo John Kipate
  8. George Francis Nangale
  9. Barua Abdi Mwakilanga
  10. Zahoro Rashid Hanuna
  11. Thomas David Kirimbunyo
  12. Angelina Bello John
  13. Eng. Abdulaziz Jahad Hussein
  14. Dr. Tulia Ackson : Naibu spika chini ya Job Ndugai
  15. Dr. Thomas Kashililah : katibu wa bunge wa zamani
  16. Stephen Masele : naibu spika wa zamani Bunge la Afrika
  17. Mussa Azzan Zungu : meya wa zamani wa Ilala Dsm.
  18. Joseph Musukuma :
  19. Ezekiel Maige : waziri wa zamani
  20. Asia Juma Abdallah : mkuu wa wilaya wa zamani
  21. Dr. Titus M. Kamani : waziri wa zamani
  22. Tumsifu Mwasamale : Afisa Maendeleo ya vijana mkoa wa Dodoma
  23. Prof. Handley Mpoki Mafwenga : mtumishi wa serikali / umma
  24. Goodluck Mlinga : mbunge wa zamani wa CCM
  25. Prof. Norman Adamson Sigala
  26. Hatibu Madata Mjega :
  27. Dr. Linda Salekwa Ole Saitabau
  28. Emmanuel Simon Sindama
  29. Bi. Uwesu Msumi
  30. Hilal H. Seif
  31. Wakili Emmanuel Paul Mngare
  32. Athumani Mfutakamba
  33. Wakili Nduruma Majembe
  34. Mwenda Burton Mwenda
  35. Henry Erasto Kessy
  36. Josephat Malima
  37. Adam Nyanyavanu
  38. Eng. Stella Manyanya
  39. Andrew Kevella
  40. Luhanga Mpina
  41. Hussein Migoda Mattaka
  42. Dr. Godwin Maimu
  43. Mohammed Ali Mmanga
  44. Esther Stefano Makazi
  45. Comrade Amos Sollo
  46. Godwin Kunambi - mkurugenzi wa zamani wa jiji la Dodoma
  47. Goodluck ole Medeye
  48. Juma Hamza Chumu
  49. Baraka Omari Baibato
  50. Hamidu Chamani
  51. Fikiri Saidi : mkuu wa wilaya wa zamani
  52. Bi. Dotto Balele Mgasa
  53. Wakili Onyango Otieno
  54. Eng. Samuel Hayuma
  55. Merkion Ndofi
  56. Abwene Majula
  57. Patrick Nkandi
  58. ..
  59. ..
  60. ..
  61. ..
  62. ..



Toka Kumbukumbu mwaka 2015 :
waliogombea nafasi ya uspika toka vyama mbalimbali walikuwa wanane (8) tu

WALIOPITISHWA NA VYAMA VYA SIASA KUGOMBEA NAFASI YA USPIKA 2015​

Jumla ya wagombea nane (8) wamejitokeza kugombea kiti cha Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Katibu wa Bunge, Dkt Thomas Kashilillah amesema, “nimepokea majina nane kutoka vyama nane vya siasa watakaogombea nafasi ya Spika wa Bunge la Kumi na Moja la Jamhuri ya Muungano .”
Amewataja waliojitokeza kuwania nafasi hiyo kuwa ni, Mhe. Peter Leonard Sarungi kutoka chama cha Alliance for Tanzania Party (AFP), Mhe. Hassan Kisabya Almas kutoka Chama cha National Reconstruction Alliance (NRA), Mhe. Dkt. Godfrey Rafael Malisa kutoka Chama cha Kijamii (CCK), na Mhe. Job Yustino Ndugai (Mb) kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wengine ni Mhe. Goodluck Joseph Ole Medeye kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Richard Shedrack Lyimo kutoka Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Mhe. Hashim Spunda Rungwe kutoka CHAUMMA na Mhe. Robert Alexander Kasinini, Chama cha Democratic Party (DP).
Kwa mujibu wa Dkt Kashilillah, uchaguzi wa Spika utafanyika kesho tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi katika ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.
Mbali na kutaja majina ya wagombea wa Spika wa Bunge, Dkt Kashilillah amesema mpaka tarehe 16/11/2015 jumla ya wabunge 348 wamekwisha sajiliwa.
Aidha Dkt Kashilillah amesema kuwa maandalizi yote kwa ajili ya mkutano wa 11 wa bunge yamekamilika.
Katika mkutano huo wa kwanza wa bunge la 11, kutakuwa na shughuli mbalimbali zikiwemo kumchagua Spika, Naibu Spika na kuthibitisha jina la Waziri Mkuu
Source : Parliament of Tanzania
Utitili huu unaonyesha ni jinsi gani hadhi ya Bunge letu imeshuka na hasa kiti cha Speaker. Hivi kweli hata kama tuna demokrasia..watu zaidi ya 50 toka Chama kimoja wanaomba ridhaa ya kupendekezwa kugombea nafasi ya Speaker? Hii inaonyesha pia Chama husika kukosa mikakati ya kutengeneza viongozi na kujidhalaurisha.

Je Wanachama hao walio chukua form hawajui vigezo, sifa na uzoefu wa Kazi ya Speaker? Kwa kweli hii ni kuifanya nafasi ya Speaker ionekane ni very cheap na ni sehemu ya Ulaji, hasa ukizingatia mafao yaliyowekwa kwa nafasi hiyo akiwa kazini na akistaafu.

Labda ingalau kuwa na Bunge litakalo anza kujitambua, achaguliwe Speaker toka Chama cha Upinzani...na wapiga kula wenyewe ambao ni wengi ni kutoka chama kimoja, onyesheni mabadiliko kama wawakilishi wa wananchi. Msifuate Siasa za Uchama Bungeni, fuateni Siasa za maendeleo ya Watanzania kwa ujumla wake.
 
Kwenye hiyo list yako sijaona jina la Dr. Kasheku mzee wa wediwide open free viza.....
 
Mlinga na Mwijaku sasa huu ni utani, hawa wameionaje hii position ya Speaker? Hatari sana.
 
Ni nini sababu za wanaCCM wote hawa kujitokeza mwaka huu 2022 kugombea nafasi ya uspika kupitia chama chao,

  • Je ni ongezeko la demokrasia ndani ya chama cha CCM ?
  • Kutoridhika kwa mwenendo wa Bunge kuburuzwa
  • Wagombea hawa 2022 katika makumi uspika ni dalili mtifuano ndani ya CCM kwa nafasi zote udiwani na ubunge 2025
  • Chama kimeshindwa kudhibiti nidhamu ya wanachama kujipima kikweli kweli wao wenyewe binafsi kuwa "wanatosha" kuwania uongozi ?
  • N.k
Jibu ni lahisi sana, Ajira na mafao kedekede wakistaafu... ndio hilo tu ingawaje wanasisitza wengine wajiajiri ili hali wote hao wanataka waajiliwe na bunge...
 
Kampuni kama Ferrari au Lamborghini wana uwezo wa kutengeneza magari ya kumuuzia kila multi millionaire duniani.

Lakini kulinda brand zao ata model ambazo ni nyingi azizidi 9000 na hiyo unakuta kwa mwaka walikuwa wakitengeneza 1000 tu kusambaza duniani.

Kuna model zingine magari ayafiki 20 duniani na production imesimama bei ya gari $4.5 million na kuna watu duniani hiyo sio hela ya kuwanyima usingizi; lakini wakizitaka awapati. Brand protection ni muhimu.

Mradi katiba imesema speaker sio lazima awe mmbunge bali mtu mwenye sifa za kuwa mmbunge; achilia mbali hao kina Mwijaku bali kila mmbunge, msomi na mfanyakazi wa serikali anadhani anayo sifa ya kuwa mmbunge.

Nchi zilizoendelea ata kama na wao takwa la kikatiba kama letu, sahau kuwa speaker if you are not a seasoned house member.

Hata USA na U.K kumbe kikatiba kugombea nafasi za leader of their houses sio lazima uwe member; lakini tokea kuanzishwa kwa nyumba zao aijawahi tokea leader kutokuwa member of the house. Sasa tujiulize hizo houses zina miaka mingapi.

Na hizo nchi sio kwamba zinawasomi wa sheria waliobobea bali zinawahusika walioshape legal thinking duniani.

Leo kuna constitutional lawyers huko wameajiriwa ndani ya vyama vya siasa wanajua kanuni za kuendesha bunge na administration law za nchi yao kushinda house member yeyote, leave alone outsiders. Lakini wanajua leader of the house traditionally ni nafasi za seasoned house members.

CCM mnaaribu nchi na kushusha viwango vya hadhi ya nafasi muhimu serikalini. Kuna watu walitakiwa ata kuchukua form za speaker waogope kwa ukubwa wa nafasi yenyewe.
 
Back
Top Bottom