Hapana..ila nakemea hiyo roho ya ubaguzi aliyo nayo mleta mada..tuwe wazalendo..ukiona mtu anakaa chini anaanza kukagua viongozi waliopo madarakani ni wa Kanda gani, kabila gani au dini gani..ujue huyo amejaa roho ya ubaguzi.tunaimani kwenye nchi yetu viongozi hawachaguliwi kwa misingi ya dini, kabila au ukanda..Bali uwezo wao kwenye kazi husika, uzoefu na elimu yao..Kama kuna mapungufu ya kibinadamu..Basi serikali iyarekebishe mapema
Ila ndugu zangu Watanzania tuache kuzungumza ukabila, udini au ukanda..hii mbegu ikiota itakuwa mbaya kwa mustakabali wa taifa letu