Majinamizi yanayomaliza watu, hususani vijana na akina mama

Majinamizi yanayomaliza watu, hususani vijana na akina mama

Trainee

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
3,118
Reaction score
4,238
Ulevi
Kamari
Zinaa
Riba

Nimetaja kwa jumla sana hapo juu sasa ngoja nichambue kidogo.
Nyimbo siku hizi vitoto vyote vinaimba tena nyimbo zenyewe ni za kishenzi na kishetani haswa. Mbaya zaidi waliotakiwa kukomesha ndiyo kwanza wanaahidi kupaisha nyimbo hizo eti zienee na kutambuliwa ulimwenguni kote

Movie siku hizi ni bandika bandua na siyo zile za part 1 na part 2 za Kigosi kavaa kanzu anataka kuoa mke wa pili au Jenifer na stori ya Lipamba tena bali ni series za kishenzi shenzi. Kila mwanamama au kijana anawaza muendelezo wa filamu anayofuatilia unatoka lini

Mabenki kila siku yanakuja na mbinu mpya za mikopo na hapo ndo kila mtu anajikuta ana sifa na anastahili kuchukua mkopo. Taasisi za mikopo nazo ni kama uyoga huko mitaani. Kuna mikopo ya vitu nayo ni balaa mfano simu za mikopo "zinawaua" vijana na wamama vijijini

Kuna mikopo ya vyombo, nguo, vifaa vya ndani, biashara ndogo, pembejeo, na kadhalika yaani chochote unachotaka ni wewe tu. Mikopo hii kwa namna watu wanavyoichangamkia walahi litakufa jitu

Kamari sasa ndo imegeuzwa njia kuu kwa vijana kuingiza kipato. Kuna mabonanza ya wachina, kubeti makampuni kibao kwenye simu matangazo yao mpaka yanaboa, na madude mengine mengi ambayo yote ni pata potea

Kila siku kunabuniwa ulevi mpya au staili mpya ya kutumia vilevi utaona siku hizi sherehe zimekuwa nyingi kwelikweli na ili ionekane ilifana basi vilevi vya kutosha

Ni kama vile kuna mtaalamu ameviweka stoo vitu hivi anaachia kimoja baada ya kingine. Yaani bila kupaza sauti nchi na ulimwengu kwa ujumla unakwenda kuwa wa hovyo kabisa miaka ya mbeleni huko
 
Uchumi wa mabank kupitia Riba ni hatari sana..
1000146575.jpg
 
Back
Top Bottom