Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Majirani wamemripoti jamaa kituo cha polisi kisa kazi yake haijulikani! Sasa anadai Milioni 500 kwa kuletewa usumbufu

Wakuu Kuna jamaa hapa mtaani alikua anahisiwa anafanya shuguli haramu sababu anamaisha mazuri ila kazi yake haijulikani anashindwa ndani akitoka jioni

Sasa Kuna majirani wawili wamemripoti polisi akaja kukamatwa. Sasa akiwa huko polisi akasema yeye kazi yake ni kubeti na analipa Kodi Kwa serikali kupitia mikeka yake anayoshinda na kweli kaonyesha mikeka anakula mamilioni ya pesa ni aina ya watu wanaoweka pesa nyingi sana kwenye mechi.

Sasa kingine kaenda mahakamani anawashitaki majirani zake hao wawili Kwa kosa la kumdhalilisha na kumpotezea mda wa kufanya mambo yake ya msingi na anadai fidia million 500 na ana mawakili wake kabisa wa 3

Hivi hii kesi anaweza kushinda huyu jamaa ishu ipo serious sana
Ishu ni serious sana.Na hao majirani lazima watandikwe Bakora 12 maana wanakosa adabu kabisa.Ndio maana TAIFA letu linazidi kuwa maskini.Na huyo Jamaa aache Kubeti.
 
Wewe
Ishu ni serious sana.Na hao majirani lazima watandikwe Bakora 12 maana wanakosa adabu kabisa.Ndio maana TAIFA letu linazidi kuwa maskini.Na huyo Jamaa aache Kubeti.
Unaweza kuacha kazi inayokuingizia pesa utakula nini Sasa au utakula mchanga
 
Hamna kesi hapo , ninachojua mimi kuna kosa la malicious prosecution .
Hii na hadi mtu apelekwe mahakamani mahakama imkute hana hatia .
Sasa kama ishu imeishia polisi, Polisi ndio watakuwa na makosa kwa nini wamtaje mtoa taarifa za siri
Sawa ngoja tuone
 
Hakuna kesi hapo,
Mahakamani wanahitaji ushahidi usio na shaka, jamaa ajipange kutoa uthibitisho wa kushiriki na kushinda hizo betting.
 
Hakuna kesi hapo,
Mahakamani wanahitaji ushahidi usio na shaka, jamaa ajipange kutoa uthibitisho wa kushiriki na kushinda hizo betting.
Ushahidi so upo kwenye simu yake ndio maana polisi wamemuachia
 
Wakamuulize huyo whistle blowe maarufu Snowden alivyonusurika.
Sheria mbele ya wabobez hainaga jibu la moja kwa moja. Inategemeana na vile unavyoitafsi na kuijua madhaifu yake in correlation to other situations. Kuna loopholea kwenye kila the so called sheria
Unachanganya vitu wewe. Snowden yeye alitoa siri za nchi kwa nchi za nje lakini majirani wametoa taarifa kwa Polisi ndani nchi na sheria ya whistle blowing ni ya Tz siyo ya Marekani.
 
Wakuu Kuna jamaa hapa mtaani alikua anahisiwa anafanya shuguli haramu sababu anamaisha mazuri ila kazi yake haijulikani anashindwa ndani akitoka jioni

Sasa Kuna majirani wawili wamemripoti polisi akaja kukamatwa. Sasa akiwa huko polisi akasema yeye kazi yake ni kubeti na analipa Kodi Kwa serikali kupitia mikeka yake anayoshinda na kweli kaonyesha mikeka anakula mamilioni ya pesa ni aina ya watu wanaoweka pesa nyingi sana kwenye mechi.

Sasa kingine kaenda mahakamani anawashitaki majirani zake hao wawili Kwa kosa la kumdhalilisha na kumpotezea mda wa kufanya mambo yake ya msingi na anadai fidia million 500 na ana mawakili wake kabisa wa 3

Hivi hii kesi anaweza kushinda huyu jamaa ishu ipo serious sana
Anaweza kushinda hata kwa fidia ya chini ya m500

Ila Betting 😡😡
 
Huyo jamaa nachoona ni kwamba, anajua kabisa hao majirani hawana huo uwezo hata wa kumlipa mil.5, ila anachofanya ni kama kuwapa somo la kuacha umbea na kufuatilia maisha ya wengine. Kutafuta pesa sio mpaka utoke nje ya makazi yako. Kuna wanaojipatia pesa kwa njia za online ikiwemo hiyo betting, cryptocurrency, Forex, freelrncing n.k. ila eengi hawajui wanaamini kutafuta riziki ni lazima utoke asubuh urudi jioni... So hapo atawasamehe ila atakuwa kawapa somo na hawatorudia tena hizo mambo ktk maisha yao..
 
Kushitaki ni kutoa ushahidi wa tukio la kihalifu..., kutoa taarifa ni kutoa hisia kwamba huenda kuna uhalifu, kutoa taarifa ndio polisi na vyombo vya kisheria vinashauri ufanye
Na ndio maana kuna Mabalozi wa mitaa, walitakiwa walifikishe kwa balozi kisha baloz ndo alifuatilie kwa hekima likimshinda ndio alipeleke polisi.
 
Huyu ndio ana invest kwenye kubet sasa sio sisi wazee wa mikeka team 20
 
Back
Top Bottom