Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Mkurugenzi Mkuu wa EFM na TVE ambaye pia ni mdau mkubwa wa Muziki haswa wa Singeli, Majizzo amewaomba Watanzania kufuta kauli na Msimamo wa kugomea kusapoti Wasanii wa Tanzania kwa sababu eti walijihusisha na Siasa kwani wale ni watoto wa kimasikini ambao wanapambania ndoto zao hivyo kuacha kuwasapoti ni kuua ndoto zao.
Natoa pole kwa yote yaliyotukuta baada ya Uchaguzi wa Oktoba 29, kubwa zaidi wale waliopata misiba. Natambua maumivu yenu, Mungu mwenyewe awe mfariji kwenu. Pole kwetu sote.
Nimejiridhisha kwamba huu ni wakati sahihi kuja kwenu kuzungumza, lengo langu mahsusi ikiwa Sekta ya muziki na hasara tunayotengeneza kwa Watanzania wanyonge.
Ni kweli wasanii wanaathirika
Lakini athari kubwa zaidi, ipo kwa kundi kubwa linalotegemea hizo kazi za sanaa. Dancers wana kosa gani? Wapiga vyombo, Make up artists, Wauza Nguo, na wengine wengi? Familia zao vipi?
Moja vilio ambavyo tunalia wote, ni kilio cha ukosefu wa ajira, hivyo tusizipige teke hizi ajira kwenye kiwanda cha muziki kwa sababu kuna watu wachache wametukasirisha.
Ninaposema nimewahi kumchangia Sugu pesa sio kwamba alikuwa na shida binafsi, Sugu ni taita anayo pesa ya kutosha. Pesa ninayoongelea hapa ni ya kusaidia harakati za Muziki kupitia Bongo Flavour Honors.
Na namtaja Sugu kama mfano wa wengi ambao wametumia maisha yao yote kuukuza muziki wetu, hata wao walipochagua vyama hawakutengwa na watu wa vyama vingine. Sugu hakuwahi kusema wanachama wa CCM wasije kwenye show zake au wasisikilize muziki wake.
Nawaita kina Sugu na watu wengine, tusiruhusu muziki uanguke kwa sababu ya tofauti zetu za kiitikadi.