Majohe: Zaidi ya Masaa 24 Bila Umeme, Tanesco Hamtoi Taarifa Wala Majibu, Tatizo Nini?

Saimony

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2015
Posts
469
Reaction score
542
Ninaomba kuwasilisha kero yangu kwa Tanesco kuhusu hali ya umeme katika maeneo la Majohe, Dar es Salaam.

Kwa muda sasa tumekuwa tukikumbana na tatizo la kukatika umeme mara kwa mara bila taarifa yoyote. Karibu kila baada ya siku mbili au tatu tunakaa siku nzima bila umeme, huku wananchi tukikosa maelezo ya tatizo ni nini na ni lini huduma itakaaa sawa.

Kwa mfano, jana umeme umekatika tangu saa tatu asubuhi mpaka leo saa mbili asubuhi hii ndio umerudi. Hali hii imekuwa ikiathiri sana biashara zinazotegemea umeme, pamoja na watu wanaofanya kazi za mtandaoni ambao wanashindwa kutekeleza majukumu yao.

Cha kusikitisha zaidi ni kwamba tangu jana asubuhi hadi muda huu wa leo, masaa 24 yamepita ndio umeme unarejea. Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa popote kuwa kutakuwa na katizo la umeme masaa 24 na hata tukijaribu kuwasiliana na wahusika mara nyingi hatupati majibu. (Page ya tanesco Instagram haijibi wakati mwingine page inawekwa sleep mode, kupiga simu huduma kwa wateja haipokelewi

Tunaomba Tanesco itoe ufafanuzi kuhusu chanzo cha tatizo hili na hatua zinazochukuliwa kulitatua. Wananchi tuna haki ya kupata taarifa sahihi na kwa wakati, hasa pale huduma muhimu kama umeme inapokatika kwa muda mrefu kiasi hiki.

Tafadhali vaeni viatu vya wananchi na wafanyabiashara wanaotegemea umeme kwa shughuli zao za kila siku. Hasara tunazopata ni kubwa na hali hii imekuwa ikijirudia mara kwa mara bila suluhisho la kudumu.

Tunaomba majibu na hatua za haraka.
 
Habari Saimony, pole na tunaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza.

Tafadhali tunapenda kukufahamisha kuwa inapotokea ukosefu wa huduma ya umeme tambua kuwa inatokana na matengenezo ya miundombinu yetu ambayo kwa kawaida hutangazwa mapema pamoja na maeneo yanayoathirika, na taarifa za dharura pia hutolewa inapohitajika.

Taarifa hizi husambazwa kupitia makundi ya WhatsApp na SMS. Ikiwa bado hujajiunga na makundi hayo, tafadhali pokea link ya group la TANESCO Majohe
8.B.26TANESCO HUDUMA MAJOHE. ^HN
 
TANESCO nnayoijua mimi nitofati na hii unayoilezea, huku kwetu tunapata taarifa za makatizo, ukipata changamoto jamaa wanapokea simu kwa wakati na wakiwa na matengenezo wanatujulisha mapema tena muda mwingine wanatukumbusha.
 
Habari, Ndugu Mteja. Tunashukuru kwa haya maelezo na tunajitahidi kufikia wateja wetu kwa wingi kuhakikisha wanapata taarifa mapema kupitia makundi ya WhatsApp ya Huduma kwa Wateja katika maeneo yao na kupitia taarifa fupi, yaani SMS. ^NM
 
Habari Saimony, pole na tunaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza.

Tafadhali tunapenda kukufahamisha kuwa inapotokea ukosefu wa huduma ya umeme tambua kuwa inatokana na matengenezo ya miundombinu yetu ambayo kwa kawaida hutangazwa mapema pamoja na maeneo yanayoathirika, na taarifa za dharura pia hutolewa inapohitajika.

Taarifa hizi husambazwa kupitia makundi ya WhatsApp na SMS. Ikiwa bado hujajiunga na makundi hayo, tafadhali pokea link ya group la TANESCO Majohe
8.B.26TANESCO HUDUMA MAJOHE. ^HN
Wa majohe walishaipigia kura CCM hapo October 29 japo walikufa kwa maksudi kabisa
Leo wanathamani Gani hata wapewe umeme wa uhakika?
Wameshakuwa toilet paper
IPO sikuk
 
Habari, Ndugu Mteja. Shirika letu linatoa huduma kwa Watanzania wote, hivyo tunakusihi ujiunge na kundi la WhatsApp tulilotuma ya Wateja wa Majohe ili uweze kupata taarifa mbalimbali kuhusu huduma za umeme kwa wakati.

Kila tunapotoa taarifa kuhusu huduma zetu, tunafafanua sababu zinazohusika na pia tunatoa nafasi kwa wateja kuuliza maswali na kutoa maoni yao ili kuhakikisha kunakuwa na uelewa wa pamoja na kuondoa mkanganyiko wowote unaoweza kujitokeza. Asante kwa ushirikiano wako. ^NM
 
Habari Saimony, pole na tunaomba radhi kwa changamoto iliyojitokeza.

Tafadhali tunapenda kukufahamisha kuwa inapotokea ukosefu wa huduma ya umeme tambua kuwa inatokana na matengenezo ya miundombinu yetu ambayo kwa kawaida hutangazwa mapema pamoja na maeneo yanayoathirika, na taarifa za dharura pia hutolewa inapohitajika.

Taarifa hizi husambazwa kupitia makundi ya WhatsApp na SMS. Ikiwa bado hujajiunga na makundi hayo, tafadhali pokea link ya group la TANESCO Majohe
8.B.26TANESCO HUDUMA MAJOHE. ^HN
Kwahiyo kila baada ya siku 2 mna matengenezo majohe maana tumeshinda nao jana na leo kesho laizma mtaukata tu au jumatatu na hiyo ni kama desturi yenu. Haya matengenezo mpaka lini?? Na sio mimi tu nalalamikia hili fuatilia thread zinaongelea umeme majohe
 
Habari, ndugu mteja. Tunakuomba radhi kwa kuchelewa kukujibu kuhusu suala lako.

Tunapenda kukufahamisha kuwa hatuna nia ya kusitisha huduma ya umeme kwa wateja wetu. Endapo huduma itasitishwa kwa zaidi ya siku moja, mara nyingi husababishwa na matengenezo au maboresho makubwa yanayofanyika kwa awamu ili kuhakikisha huduma inaendelea kupatikana kwa wateja wetu, au kutokana na hitilafu ambazo zinahitaji muda zaidi wa kurekebishwa.

Kwa matengenezo yaliyopangwa, huwa tunatoa taarifa kwa wateja wetu kwa kuweka wazi ratiba, muda wa kukatika kwa huduma, pamoja na sababu ya kufanyika kwa matengenezo hayo.

Tunashauri pia ujiunge na makundi yetu rasmi ya WhatsApp ili kupata taarifa kwa wakati na pia kuwa na fursa ya kutufikia kwa urahisi pale unapohitaji msaada. Unaweza kutuma ombi la kuunganishwa kupitia namba yetu ya WhatsApp ya Huduma kwa Wateja: +255 758 346 869, endapo utapata changamoto kutuma ombi kupitia jukwaa hii.

Asante. ^GK
 
Back
Top Bottom