Waw! Kumbe M23 wamejipanga. Hivi mkuu; itakuwaje ile deal ya DRC na Marekani wakianza utekelezaji??
Haiwezekani.
Na ikitokea imewezekana,
Maji na mafuta vitakuwa tayari vimeshakaa kila kimoja mahara pake.
Toka jana, ofisi ya raisi wa Angola, mpatanishi katika maswala ya mzozo wa DRC, ilitangaza kuwa rais wa DRC sasa yupo tayari kuzungumza na M23.
Ili jambo hilo lifanyike, ni kwamba plans zote za nje zinatakiwa zisitishwe, wanajeshi hao wa nchi mbali mbali, kwanza watoke( Hapa nisiende mbali, kama yeye sasa ndo anaomba mazungumzo na M23, subiri tuone orodha ya matakwa ya M23 ili ikae nae).
Kingine, kuwa rais hakumpi mamlaka ya kuuza nchi. Nchi haongozi raisi peke yake, ana kamati zake za ushauli. Hivyo wote hao hawawezi kuridhia kitu kama hicho, huku wanajua anaenufaika ni nani.
Na mbaya zaidi,kumbuka kuna wachina kwa makubaliano, Canada kwa makubaliano,USA kwa makubaliano(si kwamba hawapo). Russia ndo hivo. Hawa watu wote ukitaka wakae sehemu moja unategemea nini?
Tena kumbuka,DRC ina watu wana hela chafu. Na kwa sasa,M23 imekuwa na influence kubwa sana. Ukiangalia vitu vinavyoendelea kwenye maeneo yake,na ukiambiwa ni pesa za Congo, hawawezi kukubali michezo ya hivyo.
Matajiri hao,na wenyewe wana uwezo wa kuendesha migodi.
Kilichopo,huko Katanga, ni km60 tu kutoka ilipofika M23. Ndipo kuna mgodi wake. Je,anauachia hivi hivi uende? Japo haimaanishi atauendeleza! Ndo maana hapa subiri wazungumze ndo utajua inakuwaje.
Kumbuka tu kuwa wasaliti wa ile serikali ni wengi sana. Iwe upande wa jeshi na upande wa siasa. Jama kwa sasa nguvu ya ndani hana.