Kwa ufupi tu ni raia wa Congo.
Alizaliwa huko Rutshuru, Kivu Kasikazini.
Miaka ya 1990, alijiunga na jeshi la chama cha RPF cha Rwanda, kipindi hicho wapo maporini kwa maandalizi ya kuikomboa Rwanda.
Badae aliamua kurudi kwao, na ndo kaamua aanzishe M23.(hiyo ni historia fupi)
Chanzo cha haya yote ni baada yaserikali ya zamani ya Rwanda kuzidiwa nguvu,ikiwa na msaada wa wafaransa, ambao walikuwa pete na kidole na Zaire, ambayo ndo DRC ya leo. Huko walikofika, waliendeleza mauaji ya watutsi kambini.
Lakini pia,kwa sababu Zaire ilikuwa na watutsi, na wauaji,ambao ndi FDLR ya leo, mazoezi ya kijeshi(walikuwa nakiingiza wanajeshi wapya) yalikuwa yakifanyika nje ya kambi. Hivyo, sehemu ya kupata huduma, ikawa ni uraiani.
Huko, kulikuwa na watutsi. Ndipo vitendo vya kuwaua na kubaka wanawake vikaanza.
Kuona hivyo, akaona hakuna haja ya kukaa kimya.