Major General Mhidze aliyekuwa MSD apelekwe kwenye Court Martial

Ndo ajenge kiwanda kwao???ata kama ni uzuzu huu uko kiwango Cha lami
 
Hata hizi protocol za mwenezi akiwa anatua na ndege au kupaa unakuta wanajeshi wamejipanga kumpokea au kumuaga.
Yote haya yamesababishwa na yule Punguwani kuweka Majeshi kwenye Taasisi
 
Shida hawa ma general...wakiharibu huna Cha kuwafanya,kazi za kiraia haziwafai
 
Ukisema hii serikali ukamate wote waliokula hela, si utashika viongozi wote. Ccm na serikali yake imejaa wezi wa pesa za umma.

Nasi wananchi tusisahau kuiba pesa za umma
Join ze cheni imekusanya shilingi ngapi
 
Awamu ya 5 watu walifanya kazi kwa nidhamu ya uoga tu.

Kuwawekea pale watu mtu mwenye gwanda muda mwingi kuwatia hofu haikua busara.

Yule dikteta aliamini kuogopwa ndio ufanisi.
 
Kwanini Serikali inunue eneo la kujengea kiwanda wakati karibia kila wilaya nchi Serikali imetenga industrial area?

Kwa hiyo Ile slogan ya 'Tanzania ya viwanda' kwamba kila wilaya itajenga viwanda 100, maana yake ni kuwa Serikali ingenunua maeneo kila wilaya? Ficha ujinga unapotoa mchango katika jukwaa kwenye watu diverse kama hii.
 
Nipo hatua fulani inafanya nisifichefiche ujinga tena, nauweka wazi ili watu wauumbue nibaki na kitu sahihi. Nafikiri inajenga pia😴

Tukirudi kwenye hoja nimesemaa hivii; ichunguzwe, penye makosa awajibishwe, penye mema apongezwee. Hili suala la kuiona nusu ya upande wa kilichokosewa tu inakuponza mwenyewe na inatuponza kama taifa nakuambia.
 
Utawala wa mama umeanza kuwashughulikia mmoja mmoja bila kelele, bila kuwadhalilisha, wote watapelekwa kwenye mikono ya sheria ifate mkondo wake.

Kuna mwengine kishatumbuliwa leo kupisha uchunguzi.

Mtayasikia kila kukicha, wakuu wa mikoa, mawaziri na sehemu zote zilizotajwa na CAG wakae chon wawe na justificstions za kum prove wrong CAG, la sivyo wameenda na maji.

Mama kama siyo yeye vile, ndipo nnapompendea hapo. Tartiiib, hana mapapara kama bwana yule alivyokuwa.
 
kwa hiyo huwezi kumchambua mama bila kumtaja hayati
 
Wanajeshi hawatufai kwenye kazi za kiraia.
Ninaposikia eti apelekwe mahakama ya kijeshi naona upekee wa kumpa haki yake kibaka!
Mwizi ni mwizi tu.
 
Awamu ya 5 watu walifanya kazi kwa nidhamu ya uoga tu.

Kuwawekea pale watu mtu mwenye gwanda muda mwingi kuwatia hofu haikua busara.

Yule dikteta aliamini kuogopwa ndio ufanisi.
Huyo aliyesema hakuwemo kwenye hiyo awamu?
Maneno mengine haistahili kutamkwa mbele ya umma kama mtu ulikuwa ndani ya mfumo nahukuchukua hatua
 
Watu wa shujaa hao, wote wako juu ya sheria

Ni kama Sabaya
 
Apelekwe ukrain huyo kupigana na rusia😇🤣😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…