Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima.

Lakini ukiangalia kwa marefu na mapana hawa walaji sio kwamba wanasema mkulima apangiwe bei au pa kuuza bali wanalalamila bei zimepanda kuliko uwezo wao, kwahio nadhani Waziri atakuwa na myopic thinking kwa kudhani njia pekee ya kuzuia mfumuko ni kuzuia wakulima wasipate faida kubwa iwezekanavyo (ingawa nadhani hata hio faida wanapata walanguzi/ middle men na sio peasants ambao anajifanya kuwatetea)...

Kwa ufupi ukiangalia hili suala kwa ujumla wake ni kwamba amekosea/ tumekosea sehemu sababu kupata soko la nje sio vibaya bali ni baraka (kupata faida na watu kukuza uchumi wao) lakini kwa kuwa na demand kubwa kuliko supply kunaonyesha lack of long term planning kwa Wizara, na hapo ashutumiwe kwa kutokuwa na production ya kutosha kuweza kuuza nje na bado kubaki na mzigo wa kutosha ndani..., Mambo ya ukame tunayajua na yanatabirika kwahio ununuzi ungefanyika kabla na kuweka stock ya kutosha ili supply ikipungua waachie mzigo.

Na huko wanakotembeza bakuli hawashindwi kununua mahindi in volumes na kwa bei ya chini ili kuja kupunguza makali kwa kuongeza supply.

In short ni mengi ya kufanya kuliko kuendelea na mipasho (jambo ambalo sidhani kama ni moja ya majukumu yake)..., wananchi wanahitaji results na results ni bei ya chakula kuwa rafiki kulingana na kipato chao; kama wanashindwa kufanya hayo mimi kama mlipa kodi na bosi wao sioni umuhimu wa uwepo wao (tutaendelea kuuza nje na kulima na kulishana na hali itaendelea kuwa ngumu hivi hivi hata wasipokuwepo)
 
Ukiona unapendwa sana katika jamii yako basi tambua wewe ndie unaechukiwa kuliko wote katika jamii yako pia.

Sukama kete kwa uangalifu.

Vifijo huponza.
 
Nimeamini wa Tanzania uwezo wa kufikiri ni mdogo sana.!

Bashe ni waziri makini sana tatizo vipele vingine kama akina Bashiru na mtoa mada ubongo kb.

Acha mahindi yafike laki plastic ili vijana waache bodaboda waende vijijin wakalime, hivi mnafahamu hiyo mwaka jana mbolea wakulima walinunua mfuko sh ngap au mnapenda vya kunyonga tu!???

Mnafahamu hali ya mkulima daima ipoje vijijini?

Kwa nini bei hizi tusizifurahie zidumu ili mkulima nae anufaike ajenge nyumba ya simenti!??

Umekaa mjini huna kazi ya kueleweka nenda kijijin kalime mjini waache wafanyakazi wanaopata mshahara.
 
Nimeamini wa Tanzania uwezo wa kufikiri ni mdogo san.!
Naam huenda usemayo ni kweli.., sasa ili wengine tuongeze ufahamu unaweza kuniambia jukumu la hii wizara ni nini na kama kuhakikisha kuna uwepo wa chakula cha kutosha sio moja ya jukumu lao ?

Kumbuka hapa tunacheza na supply and demand na wenyewe kwa utashi wao, inteligensia yao inabidi wajue kabisa ni wakati gani supply ni kubwa ili waweze kujitayarisha wakati supply inapungua...
Bashe ni waziri makini sana tatizo vipele vingine kama akina Bashiru na mtoa mada ubongo kb.
Umakini wake unapimwa vipi ?, Bottom line ya kilimo na chakula ni nini kama sio watu kupata chakula mezani ?
Acha mahindi yafike laki plastic ili vijana waache bodaboda waende vijijin wakalime, hivi mnafahamu hiyo mwaka jana mbolea wakulima walinunua mfuko sh ngap au mnapenda vya kunyonga tu!???
Nimegundua unafikiria kwa mafungu na sio kwa ujumla wa jambo...., Okay tuseme yafike milioni mbili watu wakose chakula wengi washindwe kufanya shughuli za kila siku; vibaka wa kuiba mazao mashambani wazidi na wakulima kulala mashambani wakilinda mahindi yao..., unaona hio kama Jamii na nchi ni njia sahihi ya maendeleo ?!!!

Wakulima walinunua mbole kwa bei kubwa mwaka jana sawa hilo ni kosa la nani kama sio wizara husika ?!! Ndio maana nikasema hapa adui sio mlaji wala mtu yoyote mwenye busara hawezi kusema mkulima (mlanguzi / mfanyabiashara / dalali) asitafute bei kubwa na kupata faida kubwa iwezekanavyo bali point ni kwamba wizara inaweza kuhakikisha kuna supply ya kutosha at all times, ili kuepuka mifumoko ya bei....

Okay tusema gunia lifikie laki ili waendesha bodaboda waende wote wakalime mwaka kesho..., je demand ikiongezeka bado gunia litabakia laki moja au litashuka mpaka elfu 10 na watarudi tena mjini kuendesha boda ?!!! (Ndio maana nikasema ukipofikiri kwa mafungu bali kwa ujumla wake utaona kwamba vitu vinategemeana)
Mnafahamu hali ya mkulima daima ipoje vijijin???
Again kuhakikisha hali ya mkulima inakuwa nzuri ni jukumu la nani kama sio wizara ya Kilimo ? Hali ya mkulima ni mbaya na itaendelea kuwa mbaya hata mazao yakipanda maradufu sababu Tanzania majority sio farmers bali ni peasants....
Kwa nini bei hizi tusizifurahie zidumu ili mkulima nae anufaike ajenge nyumba ya simenti!??

Umekaa mjini huna kazi ya kueleweka nenda kijijin kalime mjini waache wafanyakazi wanaopata mshahara.
Again inaonyesha hata hukusoma ni hoja ipi ileletwa mezani...., nani kasema mkulima asipate bei kubwa iwezekanavyo ? Kwahio kwa logic yako hata wauza mafuta wapunguze supply ili bei zipande sababu ya demand ? Au na viwanda vipunguze uzalishaji wa Sukari, Cement na Vinywaji vyote ili bei ziwe nzuri zaidi ?

NARUDIA...., Wizara ikihakikisha hata supply ikiwa kubwa bado wakulima wanapata masoko (wanunuzi) na ikipungua serikali wanashusha mzigo walionunua wakati wa supply kubwa hence kupunguza mifumuko ya bei italeta predictability na fani ya Kilimo itaacha kuwa Bahati Nasibu...
 
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima...
Wameuza akiba ya chakula cha taifa alafu anakuja na viingereza vyake uchwara!
 
Trinity

Jibu lako lime-prove point yangu kwamba alichokifanya Bashe ni Divide and Rule na kuhamisha lawama; leo unamuona adui yako ni mlaji sababu anataka bei rafiki kulingana na kipato chake na sio Bashe mwenyewe na Wizara ambayo inafanya wewe mkulima kwanza upate mazao kwa gharama, mauzo yako ulipwe pesa ndogo kulingana na ugumu wako wa kufikisha mazao yako sokoni direct na vilevile kutokuwa na uhakika wa soko.., supply ikiwa kubwa hauna pa kuuza.

Ndio yaleyale yaliyofanywa kipindi fulani kwa Machinga kuona kwamba wanapendwa kwa kuendelea kubangaiza mchana kutwa na kupigwa jua barabarani eti tumeruhusiwa kufanya kazi kwenye mitaro na mazingira hatarishi

Kweli tuna safari ndefu sana.
 
Sisi wakulima tunamuunga mkono Bashe na Samia wake. Haiwezekani vi tecno vyenu muuze laki 5 halafu mchele wetu tuuze jero jero. Lazima ifike hatua thamani ya mkulima ijulikane ili kilimo kipate wawekezaji wa kweli.
 
Sisi wakulima tunamuunga mkono Bashe na Samia wake. Haiwezekani vi tecno vyenu muuze laki 5 halafu mchele wetu tuuze jero jero. Lazima ifike hatua thamani ya mkulima ijulikane ili kilimo kipate wawekezaji wa kweli.
Ndio maana nikauliza kazi ya Wizara ni kuhakikisha Bei inapanda maradufu? Kupanda kwa Bei kunasababishwa na nini? Kama ni supply na demand na wanajua lini demand inapanda kwanini sasa hivi kusingekuwa na supply ya kutosha kuuza popote pale?

Unadhani bei ikipanda maradufu zaidi hayo mahindi yako utauza au itabidi uongeze operational costs za kuyalinda shambani? Na kama operation costs zimepanda sababu ya mbole, umwagiliziaji na nishati kwanini wao kama serikali wasihakikishe operation costs zinapungua...
 
Nasubiri mchele ufike 4000 nipige hela, gunia zangu 300 endeleeni kupoa stoo. Kama mkulima Bashe kanikosha sana ila kama mlaji roho inaniuma. Ngoma droo
Wala kutunza ili uuze kwa wakati wako ndio the way to go wala sio brainchild ya Bashe (watu tulikuwa tunasema tangia enzi na enzi mkulima asipangiwe bei).

Ila ni uzembe wao ndio hata ulisababisha wewe kama mkulima kipindi fulani mazao yanaozea shambani kwa kukosa soko..., kwahio kama kila kitu kinaenda bora liende kuna umuhimu gani wa wao kuendelea kuwapo hapo na kula kodi zetu wakati mambo yanakwenda automatically?

Issue sio elfu 4 au nane issue ni watu kukosa income ya kutosha kuweza kukidhi mahitaji yao (basic needs) na hapo serikali as a whole imefeli
 
Ndio maana nikauliza kazi ya Wizara ni kuhakikisha Bei inapanda maradufu ? Kupanda kwa Bei kunasababishwa na nini ? Kama ni supply na demand na wanajua lini demand inapanda kwanini sasa hivi kusingekuwa na supply ya kutosha kuuza popote pale...
Natamani nikujibu kwa kirefu na ufafanuzi wenye tija ila muda nilio nao hautoshi. Tuko shambani mkuu tunaendelea kukuza mahindi ila elewa hivyo kuwa sisi wakulima tuko pamoja na Bashe. Bei zikishuka je nyie walaji mtatushushia na gharama za uendeshaji?
 
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima...
Hizo bei hazimgusi mkulima ni maalum kwa traders usidanganywe na viingereza
 
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima...
wacha wakulima wapate,ukiona bei ya vyakula iko juu nenda shamba kalime uuze kwa bei ya juu na wewe
 
Natamani nikujibu kwa kirefu na ufafanuzi wenye tija ila muda nilio nao hautoshi. Tuko shambani mkuu tunaendelea kukuza mahindi ila elewa hivyo kuwa sisi wakulima tuko pamoja na Bashe. Bei zikishuka je nyie walaji mtatushushia na gharama za uendeshaji?
Ndio maana nadhani haujaelewa majukumu ya Wizara, Jukumu la kuhakikisha gharama za uendeshaji ni rafiki ni nani ? na wakati mahindi yanashuka bei na kuozea mashambani huwa gharama za uendeshaji analipia nani ?

Issue kubwa sio kulazimisha watu wauze bei fulani, bali ni kwanini bei inakuwa kubwa hivyo unachofanya wewe ni kama kumshukuru mchawi kwa kula watoto wako wanne na kukubakishia mmoja.... wakati hata wale watatu hapaswi kuwachukua...

By the way unasahau kwamba hata mkulima pia ni mlaji.
 
wacha wakulima wapate,ukiona bei ya vyakula iko juu nenda shamba kalime uuze kwa bei ya juu na wewe
Nani kasema wakulima wasipate?, Hata kama kuna sehemu wanaweza kupata kwa milioni moja am all for that wauze huko...., ila hii beef imekuwa baina ya mkulima na mlaji na sio baina ya wananchi na wizara kwanini kuna mfumuko wa Bei (Hence Divide and Rule).

Au unamaanisha supply iendelee kuwa ndogo to infinity ili bei zipande ? Kama taifa tunahakikisha tulihakikisha vipi kwamba tuna storage ya kutosha?
 
Nani kasema wakulima wasipate ?, Hata kama kuna sehemu wanaweza kupata kwa milioni moja am all for that wauze huko...., ila hii beef imekuwa baina ya mkulima na mlaji na sio baina ya wananchi na wizara kwanini kuna mfumuko wa Bei (Hence Divide and Rule).
kwenye storage labda waziri atupitshe ktk ghala ya taifa
 
kwenye storage labda waziri atupitshe ktk ghala ya taifa
Na ukiangalia hapo ndio utaona kama Wizara wamefeli na walikuwa wanafeli:-
  • Always walikuwa wanafeli kwa kumpangia mkulima bei hususan katika soko huria
  • Walifeli zaidi kwa kushindwa kununua mazao ya huyu mkulima ambaye yakiwa machache wanampangia bei yakiwa mengi wanamuacha nayo na yanaozea shambani hence kupata hasara (wangeweza kununua na kutunza wakati supply ni kubwa
  • Wamefeli kutokuwa na hifadhi ya kutosha ili mzigo ukipungua waweze kushusha mzigo ndani ya nchi kupunguza makali (na hapo kumuachia huyu mkulima apate bei zake hata nje ya nchi)
  • Kama demand kwa majirani kubwa wamefeli kutokuongeza supply kwenye nchi yenye ardhi ya kutosha ili Kilimo ambacho ni uti wa mgongo kiweze kutusaidia kama taifa kwa kukuza uchumi wetu kwa ujumla
In short ni total failure ila siasa / cheap politics zinapelekea kupongezana kwa mediocrity...
 
Back
Top Bottom