Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Ndio maana nadhani haujaelewa majukumu ya Wizara..., Jukumu la kuhakikisha gharama za uendeshaji ni rafiki ni nani ? na wakati mahindi yanashuka bei na kuozea mashambani huwa gharama za uendeshaji analipia nani...
Jukumu kubwa la Wizara ya Kilimo (ikiwa pamoja na Waziri) ni kutunga na kusimamia sera zinahlzohusiana na kilimo na chakula) ikiwa pamoja na kulinda maslahi ya mzalishaji. Haihusiki sana na mlaji kwasababu baada ya kuzalisha na kufikisha mazao sokoni, jukumu lililobaki linahusika pia na Wizara ya Biashara, usafirishaji nk.

Aidha, kutunga na kusimamia sera ni jambo moja na kufikiwa malengo ya utekelezaji wa sera hiyo ni jambo lingine. Hivyo sera ni lazima iweke mazingira ya kuvutia uwekezaji kwenye kilimo under open and free market system. Huenda si mara zote Wizara ya Kilimo inahusika moja kwa moja na bei ya mazao kwani kuna factors nyingi zinazohusika along the value chain ya kilimo.
 
Kwanini Vyakula vinapanda bei ? Kama vinapanda bei sababu ya supply huoni mzalishaji hajafanya kazi yake ya kuhakikisha supply ya kutosha kwa mwaka mzima ?

Na kama bei ya uzalishaji ni kubwa kutokana na jambo moja au lingine (nishati, usafiri, mbolea, pembejeo n.k.) Huoni ni kosa la mtu anayesimamia uzalishaji kwa kushindwa kwakwe kuhakikisha gharama ni rafiki ?
Aidha, kutunga na kusimamia sera ni jambo moja na kufikiwa malengo ya utekelezaji wa sera hiyo ni jambo lingine. Hivyo sera ni lazima iweke mazingira ya kuvutia uwekezaji kwenye kilimo under open and free market system. Huenda si mara zote Wizara ya Kilimo inahusika moja kwa moja na bei ya mazao kwani kuna factors nyingi zinazohusika along the value chain ya kilimo.
Jambo unaloshindwa kuelewa ni kwamba kutokea kwa mfumuko wa bei ni kosa kubwa la mtu anayesimamia uzalishaji huo kutokuona mbali na kufanya preparation ya kuhakikisha hizo bei hazifumuki...., issue sio bei zinapanda kiasi gani au nani auze au asiuze wapi..., issue ni kujua kabisa beforehand kwamba mzigo ukiwa mchache (uzalishaji) basi bei zitapanda na viceversa (sasa ili kupunguza hii seesaw ya kupanda na kushuka na kufanya betting kwenye kilimo) wizara hii kwa kushirikiana na wenzao wangekuwa na system in place ya kuhakikisha supply inakuwa constant throughout the year (kwa kutumia storage)

Ila tumetoka huko na kwenda kwenye mzalishaji kumshambulia mlaji kwamba ndio adui..., (na ili kuhakikisha mfaidika anakuwa ni peasant mwenye gunia moja au mbili kule kijijini inabidi kuhakikisha anafikiwa na cooperatives au anawezeshwa ili awe na cooperatives ili kupunguza / kuondoa middlemen...
 
Kwanini Vyakula vinapanda bei ? Kama vinapanda bei sababu ya supply huoni mzalishaji hajafanya kazi yake ya kuhakikisha supply ya kutosha kwa mwaka mzima ?

Kwanini Vyakula vinapanda bei ? Kama vinapanda bei sababu ya supply huoni mzalishaji hajafanya kazi yake ya kuhakikisha supply ya kutosha kwa mwaka mzima...
Kwani hoja yako ya msingi kabisa nini? Kwanini vyakula vinapanda bei au majukumu llya Wizara au Waziri wa Kilimo?

Kwanini vyakula vinapanda bei jawabu ni suala la demand and supply. Majukumu ya Wizara ya Kilimo nini, nilishakujibu. Sera sio bulldozer, kwamba sio suala la "kuwa then inakuwa". Nimekujibu utekelezaji wa sera ni pande mbili, mtungaji na mtumiaji. Ili pawepo na supply ya kutosha ya chakula si suala la kuwakamata watu wakalime ila ni suala la kuwawekea watu mazingira bora ili wenyewe wakalime.

Miaka ya mwanzo ya JPM tulishuhudia wakulima wakubwa akina Sumry wakilalamika mazao yao kukosa soko na kuharibika baada ya kuzuiwa kuuza katika masoko ambayo walidhani wangeuza kutokana na matakwa ya kisera. Baada ya kuvuna, wakazuiwa kuuza.

Je unatarajia mkulima atalayefanyiwa hivyo arudi tena shambani mwaka unaofuata? Umeona kilichotokea kwenye korosho? Tangu Serikali ilipoingilia, korosho haijaja juu tena hadi Sasa. Ndio maana Bashe anasema much as msomi anaamua elimu yake aajiriwe serikalini, private au nje ya nchi au ajiajiri mwenyewe, mkulima naye ainjoy fursa ya namna.
 
Kwani hoja yako ya msingi kabisa nini? Kwanini vyakula vinapanda bei au jukumu la Wizara au Waziri wa Kilimo nini?
Kwanini vyakula vinapanda bei jawabu ni suala la demand and supply. Majukumu ya Wizara ya Kilimo nini, nilishakujibu. Sera sio bulldozer, na sio suala la "kuwa then inakuwa". Nimekujibu utekelezaji wa sera ni pande mbili, mtungaji na mtumiaji.
Kama ukifuatilia jibu la JIBU lako utaona automatically hio Wizara inahusika na mfumuko wa Bei..., Twende Logically....

Kupanda bei kunategema Demand and Supply (hili hata wewe unajua let alone wizara) sasa kama wanajua kabisa kwamba kuna wakati demand inakuwa kubwa kuliko supply na kuna wakati demand ndogo wakati wa mavumo makubwa hadi wakulima kukosa bei nzuri na sio kwamba hatujangundua jinsi ya kuhifadhi nafaka utaona kwamba Wizara inayosimamia uzalishaji na kuwaangalia wazalishaji haifanyi wajibu wake.... (Jambo ambalo hata Egyptians na Mababu zetu huko karne za mbali walikuwa wanafanya) - Kutunza chakula wakati wa mavuno ili kuweza kufaidi wakati wa njaa......
Miaka ya mwanzo ya JPM tulishuhudia wakulima wakubwa akina Sumry wakilalamika mazao yao kukosa soko na kuharibika baada ya kuzuiwa kuuza katika masoko ambayo walidhani wangeuza kutokana na matakwa ya kisera.
Nani kasema wakulima wazuiwe kuuza ? Unaweza ku-niqoute ni wapi nimesema hivyo ? Am all for Free Market na wala sitaki mtu apangiwe bei ya kuuza kitu ambacho ametoa jasho lake na kama anaweza kupata pengine bei kubwa itakuwa ni uchizi kuuza kwenye bei ndogo...
Baada ya kuvuna, wakazuiwa kuuza. Je unatarajia mkulima atalayefanyiwa hivyo arudi tena shambani mwaka unaofuata? Umeona kilichotokea kwenye korosho? Tangu Serikali ilipoingilia, korosho haijaja juu tena hadi Sasa. Ndio maana Bashe anasema much as msomi anaamua elimu yake aajiriwe serikalini, private au nje ya nchi au ajiajiri mwenyewe, mkulima naye ainjoy fursa ya namna.
Narudia tena kugeuza hii kwamba ni vita ya walaji kutaka kuwanyonya wakulima ni Bashe na Wizara kujivua uwajibikaji kuhakikisha supply kubwa kila wakati..., kama tunajua kwamba soko la nje huwa lipo kwanini tusilitumia muda wote ? Na kama uwezo wa kulima hatuna sio hawa hawa waliosema Magereza na wengineo wasiingie kwenye Kilimo ili watu wafanye Biashara...

Yote hii ni kuangalia mambo kwa mafungu (reja reja) na sio kwa ujumla wake.....
 
Nimeamini wa Tanzania uwezo wa kufikiri ni mdogo sana.!

Bashe ni waziri makini sana tatizo vipele vingine kama akina Bashiru na mtoa mada ubongo kb...
"Vijana waache boda boda waende vijijini wakalime.."

Point yko ni ipi?

Wanaolalamika gharama za vyakula ipo juu ni bodaboda?
 
Nimeamini wa Tanzania uwezo wa kufikiri ni mdogo sana.!

Bashe ni waziri makini sana tatizo vipele vingine kama akina Bashiru na mtoa mada ubongo...
Katika hao wenye uwezo mdogo wa kufikiria na wewe pia upo na ndio maana unadhani hu mfumuko wa bei za nafaka wanafaidika wakulima wakati ukweli ni kwamba anayefaidika hapa ni mfanya biashara wakulima walishauza hizo nafaka tokea zipo shambani tena Kwa bei ya tshs 200 Kwa kilo Moja ya mahindi
 
Ukiona mtu anabishana na hili ujue kichwani ni mtupu kabisa
 
Katika hao wenye uwezo mdogo wa kufikiria na wewe pia upo na ndio maana unadhani hu mfumuko wa bei za nafaka wanafaidika wakulima wakati ukweli ni kwamba anayefaidika hapa ni mfanya biashara wakulima walishauza hizo nafaka tokea zipo shambani tena Kwa bei ya tshs 200 Kwa kilo Moja ya mahindi
Acha uongo, nipo Iringa hapa wilaya ndani chobi, boda boda zinapishana kutafuta mahindi kitaa debe moja la lita 20 wananunua kwa 18,000.

Hakuna mkulima aliye chukizwa na bei za mwaka huu, tena asikwambie mtu watu wamelima na Mungu bariki mvua inanyesha we subiri uletewe Dar mahindi kwa elfu 2 kg ya unga.
 
"Vijana waache boda boda waende vijijini wakalime.."
Point yko ni ipi?
Wanaolalamika gharama za vyakula ipo juu ni bodaboda?
Swali zuri, kimsingi ukiona supply ni ndogo kuliko demand ujue wazalizashaji wachache au waliopo wanazalisha kiasi kidogo.

Kwa utafiti wangu mdogo wasomi na wasio wasomi wanakimbilia kazi ndogo ndogo mfano hizo boda,vibanda vya kirusha nyimbo, n.k.

Kiuhalisia kama bei za mazao zitakua hivi zilivyo zitawavuta wengi kuachana na bahasha kutafuta ajira na badala yake watahamia Mashamban.

Kilimo lazima tukifanye kama ajira na biashara, na ndicho Bashe anajaribu kukiset.

Tuache kulalamika twende shambani.! Wazolee
 
Acha uongo, nipo Iringa hapa wilaya ndani chobi, boda boda zinapishana kutafuta mahindi kitaa debe moja la lita 20 wananunua kwa 18,000.

Hakuna mkulima aliye chukizwa na bei za mwaka huu, tena asikwambie mtu watu wamelima na Mungu bariki mvua inanyesha we subiri uletewe Dar mahindi kwa elfu 2 kg ya unga.
Point yako ni ipi hasa ?

Hivi unajua wakati bei zinashuka na mazao kuozea mashambani bado ni uzembe wa Wizara husika ? Huoni kipindi watu wanakosa masoko Serikali inge-step up na kuchukua mizigo na wakati huu bidhaa zimepungua ingefanya vice versa ?

Kwa logic yako kwanini na dawa za mahospitalini tusifanye kuzipunguza sokoni ili bei ipande zaidi na wenye pharmacy nao wachangamkie fursa ?
 
Swali zuri, kimsingi ukiona supply ni ndogo kuliko demand ujue wazalizashaji wachache au waliopo wanazalisha kiasi kidogo.

Kwa utafiti wangu mdogo wasomi na wasio wasomi wanakimbilia kazi ndogo ndogo mfano hizo boda,vibanda vya kirusha nyimbo...
Kwa utafiti wako mdogo uliofanya bei zitabakia hivi ? na hao wote Boda, vibanda vya nyimbo n.k. wakienda kulima (kubahatisha kwenye kilimo) unadhani bado bei itabakia hivi ?

Hakuna mtu ambaye anasema Kilimo kisiwe ajira (ingekuwa hivyo tusingesema kilimo ni uti wa mgongo) lakini kinachofanyika mpaka sasa bado ni siasa (majority ya wanaolima ni peasants) hakuna soko la uhakika na bado watu wanategemea mvua in short ni bahati nasibu na watu kuwa one step behind mwaka huu bei zikiwa nzuri mwaka kesho kila mtu analima bei zinashuka mwaka ujao wanaacha bei zinapanda wakati peasants wanauza mpaka mbegu na kukosa hata chakula chao wenyewe...,
 
Naam huenda usemayo ni kweli.., sasa ili wengine tuongeze ufahamu unaweza kuniambia jukumu la hii wizara ni nini na kama kuhakikisha kuna uwepo wa chakula cha kutosha sio moja ya jukumu lao...
Nimesoma mara kadhaa maelezo yako, kwa ufupi tukubaliane kwamba jukkumu la wizara ni ku set standard price ya mazao.

Lazima ifanyike tafiti uzalishaji wa ekar unagharimu inputs cost kiasi gani na output gain iwe kiasi gani kwa mkulima.

From there tunaweza kusema wizara ikawa imebalance pande zote na si kama tulivyo zoea KUMKANDAMIZA MKULIMA ambao ndo wazazi wetu vijijin.

Kumbuk pia kilimo kikiwa ni fursa itasaidia kutatua changamoto ya ajira kwa kiasi kikubwa refer mpango wa servikale block farms.

Kwa bei hizi za mazao acha ziishie hivi hivi maana by that time pembejeo zilikua juu sana mfano mfuko wa DAP ulifika laki na 40, leo unataka huyu aliyejitoa muhanga kubeba risk akuuzie bei chee, no haiwezekani.!
 
Nimesoma mara kadhaa maelezo yako, kwa ufupi tukubaliane kwamba jukkumu la wizara ni ku set standard price ya mazao...
Ku-set prices ni kazi ngumu sana ndio mwisho wa siku watu wataanza kushikwa kama walanguzi na wengine kuficha mizigo na kuuza kwa wizi....

Point kubwa ambayo nimesema kuepusha mazao kuozea mashambani wakati wa mavuno na ukizingatia Serikali ina wigo mpana wa kuweza kutafuta masoko nje na pia facilities za kutunza mazao.

Kwanini bei hii inavyokuwa ya kutupa kwa kumsaidia mkulima wasinunue at a reasonable price na kuyatunza ili wakati ambapo huwa bei zinapanda sana wakatoa mzigo sokoni ili bei zisipande maradufu?

Hii itamsaidia hata mkulima kuweza kupanga mikakati yake akijua kabisa angalau atapata kiasi fulani cha bei na sio hii bahati nasibu ya sasa....

Tena ili kodi zetu zisitumike kwa kununua mazao na kutoa ruzuku wanaweza wakawawezesha wakulima wakawa na storage za maana na waweze kupata mzigo mkubwa zaidi wa kuweza kuuza mwaka au hata miaka miwili.....
 
Ku-set prices ni kazi ngumu sana ndio mwisho wa siku watu wataanza kushikwa kama walanguzi na wengine kuficha mizigo na kuuza kwa wizi...
My friend huo ni mtihani mkubwa sana kwa serikali yako unataka kuipa.

Yaani inunue mazao ya wakulima mikoa yote itawezea wapi aisee.

Kuhusu mazao kuozea shamban labda mali mbichi hizi nyanya, viazi n.k.

Lakini kwa mazao ya nafaka yakiozea shamban ni vile mkulima kaamua kulingana na tumaini la soko halipo.
Ma ghala yapo nimeyaona yamejengwa sana huku kusini sijajua maeneo mengine.!
 
Nimeamini wa Tanzania uwezo wa kufikiri ni mdogo sana.!

Bashe ni waziri makini sana tatizo vipele vingine kama akina Bashiru na mtoa mada ubongo kb...
Angalia usivyokuwa na akili kuliko hao unaoona "hawana uwezo wa kufikiri".

Msimu huu mahindi yanakuwa adimu, vijana wanaacha bodaboda na kwenda kulima, msimu ukiingia mahindi yamejaa kila sehemu, hata huko nje bei ni ya kutupa, utafanya nini?
 
Sasa wewe ndo umeelewa somo una akili.

Sasa baada ya wengi kuingia kulima mpaka wasio na Kazi rasmi na kupelekea mahindi kutapakaa kama unavyosema, jambo la msingi Serikali ifungue mipaka yote na kusiwe na longo longo mipakani Kama kipindi cha mwendazake lkn pia serikali kitengo cha (nation food) kinunue mahindi mengi kwa bei nzur ili bei zilizopo zisishuke zaidi ya nusu ya bei ya sasa.
Umeelewa.!??
 
Hizo bei hazimgusi mkulima ni maalum kwa traders usidanganywe na viingereza
Mkuu, unamaanisha kuna sehemu wakaulima wanauza au wameuza mahindi kwa bei ya mwaka jana (Aftatu) ?

Suala jingine naona kama una ignore the role of "value chain"....

Sekta ya kilimo (kutoka shambani hadi mezani) ina wahusika (actors) wengi sana hapo katikati na wote wapo kihalali.

Ni kama ilivyo kwenye sekta zote zingine za kiuchumi (madini, utalii, uvuvi, mifugo, usafirishaji, n.k).

Kama mkulima anaendelea kumuuzia mfanyabiashara mahindi kwa bei ya mwaka jana, wakati gharama za uzalishaji zimepanda na pia bei ambayo mfanyabiashara anaenda kuuza hayo mahindi imepanda, huo ni uzembe wa mkulima.
 
Back
Top Bottom