Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Kupanda kwa bei ya chakula ni jambo zuri kwa uchumi wetu. Zuri sana. Na hao 'walanguzi' walitokea sababu ya kuzuia kuuza mazao nje. Mpango huu wa Bashe utawamaliza
 
Haya mawazo ya kumtaka kila anayehoji kupanda Kwa bei ya chakula naye aende akalime ni ufinyu wa kufikiri. Mfano Walimu, maaskari, marubani, madaktari na wote walioajiriwa Ili wawahudumie hao wakulima Kwa namna moja au nyingine wote waende kulima? Chakula chenu lazima kiuzwe Kwa bei wanayoweza kuiweza, vinginevyo ni sawa na kusema hao wakulima wasitusumbue kuleta wagonjwa wao mahospitalini Ili siye pia tupate muda wa kulima kama mnafikiri hiyo ndiyo solution. Vivyo hivyo muwe na shule, magereza, vyombo vyenu vya usafiri wenyewe nk. Issue hapa ni kwamba lazima serikali itafute namna iliyo Bora na isiwe issue ya kutishana ati kila anayelalamika akalime. Familia Bora inapimwa Kwa utoshelevu wa vitu vya mhimu Cha kwanza ni chakula, ni sawa sawa na nchi.
Familia iwe chakula na chakula cha kutosha kwani umeambiwa chakula hakipooo.!?

Aliye kwambia manesi au wakalime ni wapi hapo ebu quote?

Wadau wamesema wasio na kazi maalumu ndo wakalime mfano, ukienda mijini utakutana na vyombo vya usafir mdogo mdogo utitili.
Well wamejiajir baada ya kutoka vyuo lkn kwa nyongeza tupendekeza serikal iweke mazira ya kilimo kuwa biashara inayolipa pia ajira kwa wasio na ajira rasmi.

Issue ya walimu, askari hao ni wateja wetu tunawapigania mishahara waongezewe daima ili mzunguko kwa mkulima na wafanyabiashar wengine wanufaike kupitia wao.
 
Katika hao wenye uwezo mdogo wa kufikiria na wewe pia upo na ndio maana unadhani hu mfumuko wa bei za nafaka wanafaidika wakulima wakati ukweli ni kwamba anayefaidika hapa ni mfanya biashara wakulima walishauza hizo nafaka tokea zipo shambani tena Kwa bei ya tshs 200 Kwa kilo Moja ya mahindi
Mkuu umesema kweli kabisa, nilishangaa nilikwenda fanya kazi mkoa fulani, nikakuta wakulima wameshauza mahindi yaliyoko shambani. Nilipodadisi wakaniambia ni kawaida ingawa huko nyuma haikuwa hivyo kwa kiwango hiki. Wenye mahindi kwa sasa ni wafanyabiashara wenye warehouses, au wanaokodi warehouses, na wametengeneza pesa nzuri tu.
 
Acha uongo, nipo Iringa hapa wilaya ndani chobi, boda boda zinapishana kutafuta mahindi kitaa debe moja la lita 20 wananunua kwa 18,000.

Hakuna mkulima aliye chukizwa na bei za mwaka huu, tena asikwambie mtu watu wamelima na Mungu bariki mvua inanyesha we subiri uletewe Dar mahindi kwa elfu 2 kg ya unga.
Sasa amesema uongo gani mkuu, amekwambia wakulima waliuza mahindi tangu yakiwa shambani, so hawafaidiki na ongezeko lolote la bei la sasa. Hata kwa Mbeya kuna maeneno wana tabia ya kuuza mahindi tangu yakiwa shambani.
 
Huenda unaishi mjini, mimi naongea kulingana na uzoefu maana ni mtoto wa mkulima lkn pia mahangaiko yng yapo jirani na wakulima wadogo.

Wakulima wengi huuza mahindi kidogo kidogo mpaka kulingana na shida yake kwa wakati huo, na wengi pia wanauza lkn wanabakisha wanauza december na january kwa ajili ya kununulia pembejea kuhudumia msimu mpya.
Kwa hiyo tusijumuishe kwamba mkulima ameuzia mazao shamban sio kweli labda mwenye dharura kubwa.
Mpaka sasa bado vijijini kuna vituo vinakusanya mahindi na kusafirisha.
 
Kumbe wakati tunasema tuuze nje tulikuwa tunakataza kununua nje ? (Hili ndio Soko Huria)!!!

By the way tungewekeza na kuhakikisha tunazalisha vya kutosha na kwa gharama nafuu nadhani kungekuwa hakuna haja ya kuagiza nje ?

Na tunaagiza kwa kiasi gani per kg na kwanini huko tunapoagiza bei ni ndogo kuliko hapa kwetu ?

Hilo inabidi lisitazamwe tu bali lifanyiwe kazi...
 
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima.

Lakini ukiangalia kwa marefu na mapana hawa walaji sio kwamba wanasema mkulima apangiwe bei au pa kuuza bali wanalalamila bei zimepanda kuliko uwezo wao, kwahio nadhani Waziri atakuwa na myopic thinking kwa kudhani njia pekee ya kuzuia mfumuko ni kuzuia wakulima wasipate faida kubwa iwezekanavyo (ingawa nadhani hata hio faida wanapata walanguzi/ middle men na sio peasants ambao anajifanya kuwatetea)...

Kwa ufupi ukiangalia hili suala kwa ujumla wake ni kwamba amekosea/ tumekosea sehemu sababu kupata soko la nje sio vibaya bali ni baraka (kupata faida na watu kukuza uchumi wao) lakini kwa kuwa na demand kubwa kuliko supply kunaonyesha lack of long term planning kwa Wizara, na hapo ashutumiwe kwa kutokuwa na production ya kutosha kuweza kuuza nje na bado kubaki na mzigo wa kutosha ndani..., Mambo ya ukame tunayajua na yanatabirika kwahio ununuzi ungefanyika kabla na kuweka stock ya kutosha ili supply ikipungua waachie mzigo.

Na huko wanakotembeza bakuli hawashindwi kununua mahindi in volumes na kwa bei ya chini ili kuja kupunguza makali kwa kuongeza supply.

In short ni mengi ya kufanya kuliko kuendelea na mipasho (jambo ambalo sidhani kama ni moja ya majukumu yake)..., wananchi wanahitaji results na results ni bei ya chakula kuwa rafiki kulingana na kipato chao; kama wanashindwa kufanya hayo mimi kama mlipa kodi na bosi wao sioni umuhimu wa uwepo wao (tutaendelea kuuza nje na kulima na kulishana na hali itaendelea kuwa ngumu hivi hivi hata wasipokuwepo)
Mengi ya kufanya kama yapi? Mbona una bwabwaja bila majibu? Mjinga typical blaa blaa as usual za Mtanzania
 
Mengi ya kufanya kama yapi? Mbona una bwabwaja bila majibu? Mjinga typical blaa blaa as usual za Mtanzania
Aisee hata kusoma haujui ?!!!!

Moja kwenye post ya kwanza nimesema kwanini kama production imekuwa ndogo short term wasingetoa chakula nje (jambo ambalo naona wamefanya when its too late watu wameshaumia)

Mbili badala ya kuhangaika na kuwa reactive kununua chakula wangewasaidia wakulima wakati bei zipo chini kununua au kuhakikisha pembejeo zina gharama rafiki hence kupunguza gharama za uendeshaji...

Tatu kuhakikisha production inakuwa kubwa kila wakati hapo kutakuwa hakuna haja ya kuongelea kufunga mipaka kila mtu atauza anavyotaka popote anapotaka.

Kuhakikisha tuna storage ya nafaka kulisha nchi walau kwa mwaka mmoja hapo bei zinaposhoot wanaachia mzigo hence ku-balance bei
 
Acha uongo, nipo Iringa hapa wilaya ndani chobi, boda boda zinapishana kutafuta mahindi kitaa debe moja la lita 20 wananunua kwa 18,000.

Hakuna mkulima aliye chukizwa na bei za mwaka huu, tena asikwambie mtu watu wamelima na Mungu bariki mvua inanyesha we subiri uletewe Dar mahindi kwa elfu 2 kg ya unga.
Ndio maana nimekuambia katika hao watu wenye akili ndogo na wewe upo

Sasa kama wakulima wangekuwa na mahindi hao bodaboda wangeangaika kutafuta debe debe Kwa wakulima?

Hizo bodaboda unazoziona hao sio wafanya biashara hao tunawaita wachuuzi

Wafanya biashara walishanunua mahindi tokea yapo shamba wakayavuna na kujaza katika maghala Yao Sasa hivi wanapiga pesa

Yani nyinyi Bashe amewajaza ujinga sana Kwa kujifucha katika mgongo wa wakulima kumbe mwenzenu anawanufaisha wafanya biashara aka mafisadi
 
Sawa.
 
Vipi unasemaje kuhusu kuruhusu mzigo kuagizwa kutoka nje ? Hapa bado anawatetea au anawaonea ?

Naomba maoni yako....
Tumelalamika mno imembidi aruhusu chakul/mchele kuingia Tz.

Kimsingi hiyo ni short team solution lkn tungevumilia tunge solve uhaba huu kwa long term stratergic ambazo zingetusaidia kwa kiwango kikubwa.

Kuna msemo mara nyingi unatumika naomba niutumie kurahisisha maana ya hii hali.

Wanasema "ukiwa hauna samaki, usiombe samaki bali omba zana na ujuzi wa kuvua samaki"

Tungetafuta namna ya ku incounter hii shortage ingesaidia kuwa stable kwa miaka mingi katika uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa manufaa ya mkulima na mlaji.

KeyserSoze
 
Tumelalamika mno imembidi aruhusu chakul/mchele kuingia Tz.
Unajua kwamba chakula ni basic need ? Unajua kwamba chakula ndio nishati ya binadamu ili afanye kazi nyingine sasa kama hata una tractor lako halina mafuta ya kutosha unategemea litalima ?

Wala watu hawakupaswa kulalamika ndio wafanye wangehakikisha hata hayo malalamiko hayatokei na kama ni bahati mbaya majanga yametokea wangekuwa tayari wana stock / suluhisho la kufanyika kama majanga yatatokea na last resort ndio hii kuagiza kutoka nje...

Wewe usilazimishwe kuuza sehemu moja (uza hata nje) ila na usiwanyime watu chakula cha bei wanayomudu eti tusinunue nje wakati wewe bei unayotoa haiendani na buying power yao / income
Kimsingi hiyo ni short team solution lkn tungevumilia tunge solve uhaba huu kwa long term stratergic ambazo zingetusaidia kwa kiwango kikubwa.
Kwanini hizo long term strategies hazikufanyika tangia miaka mitatu huko nyuma ? kwanini kama hao wa nje wanaweza kuuza mzigo kwa bei ya chini na wewe unapofika nchini na wewe usiige wanachofanya ili uwauzie ?
Kuna msemo mara nyingi unatumika naomba niutumie kurahisisha maana ya hii hali.

Wanasema "ukiwa hauna samaki, usiombe samaki bali omba zana na ujuzi wa kuvua samaki"
Nani ni mvuvi na nani ameomba samaki ? Mvuvi ni wewe (mkulima) na Serikali yako ingebidi ikupe ujuzi huo tangia miaka ya huko nyuma ili leo uweze kuvua samaki ya kulisha familia yako (walaji) sasa wewe umeshindwa kulisha familia alafu unataka hata kwa jirani tusichukue kwa bei nafuu (unataka tufe)? Kwahio hapo kosa la nani ? Mlaji au Wizara ?
Tungetafuta namna ya ku incounter hii shortage ingesaidia kuwa stable kwa miaka mingi katika uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa manufaa ya mkulima na mlaji.

KeyserSoze
Shortage ni kuongeza supply na storage ili ikitokea issue kama hii kubalance bei isifumuke..., wala pia na mimi sikubaliani mkulima apangiwe sehemu ya kuuza vilevile sikubali kabisa kwamba ninunue mazao bei mbaya hapa ndani wakati kuna kodi zangu zishakusanywa na zinaweza kuleta mazao ambayo yatapunguza bei (ingawa hio pia ni kufuja pesa kwa nchi yenye ardhi kubwa) best scenario ni kuhakikisha kuna supply ya kutosha hadi kubaki for storage ya kutosha atleast mwaka mzima
 
Muendelezo wa Divide and Rule....; Sasa hivi ni kosa la Wafanyabiashara kwa kuuza Sukari bei juu
 
Kupanda kwa bei ya chakula ni jambo zuri kwa uchumi wetu. Zuri sana. Na hao 'walanguzi' walitokea sababu ya kuzuia kuuza mazao nje. Mpango huu wa Bashe utawamaliza
Vipi kupanda kwa Sukari ?
 
Vipi kupanda kwa Sukari ?
Inategemea na sababu ya kupanda. Kama kupanda ni sababu amepatikana mteja aliye tayari kununua kwa bei nzuri ni jambo zuri sana. Lakini kama bei imepanda sababu ya hila chafu za cartels na monopoly mbovu basi ni jambo baya.
 
Inategemea na sababu ya kupanda. Kama kupanda ni sababu amepatikana mteja aliye tayari kununua kwa bei nzuri ni jambo zuri sana.
Sasa kama wateja wanapatikana wa kununua kwa Bei kubwa wakati kuna Bei ndogo si watakuwa wajinga kununua kwa bei kubwa ? Hapo utaona kwamba supply imepungua (demand ni kubwa zaidi)
Lakini kama bei imepanda sababu ya hila chafu za cartels na monopoly mbovu basi ni jambo baya.
Hizo ni Siasa za wanasiasa always blaming the other guys, for their incompetent. Kama hao so called wafanyabiashara waliamua kuchukua risk ya kununua sukari wakati bei chee kwa ku-bet kwamba itapanda na ikapanda fair to them..., Sababu isingepanda wangekula hasara wala hakuna ambaye angewasaidia....

In short Price Setting (Kupanga Bei) does not and has never worked
 
Back
Top Bottom