Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

My friend huo ni mtihani mkubwa sana kwa serikali yako unataka kuipa.

Yaani inunue mazao ya wakulima mikoa yote itawezea wapi aisee.
Mkuu unawajua hawa wadau ? (NFRA - https://www.nfra.go.tz/) Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula ? Hakuna mtu aliyesema wanunue mazao yote ila wanunue kiasi cha kutosha wakifanya hivyo wanaongeza demand wakati wa supply kubwa....

Mazao hayo wanayoyahifadhi bei zikipanda maradufu wanayaingiza sokoni ili kubalance bei (wanaongeza supply)
Kuhusu mazao kuozea shamban labda mali mbichi hizi nyanya, viazi n.k.

Lakini kwa mazao ya nafaka yakiozea shamban ni vile mkulima kaamua kulingana na tumaini la soko halipo.
Ma ghala yapo nimeyaona yamejengwa sana huku kusini sijajua maeneo mengine.!
Kwamba bei ikiwa ndogo mijini walanguzi wamejaza maghala yao na wanaona hakuna faida ya kuchoma mafuta kwenda vijijini kutafuta mazao na huko kijijini watu hawana capacity ya kutosha kutunza mazao yao mpaka mwaka ujao unadhani yatafanya nini kama sio kuoza...

Ngoja nikupe statistics mojawapo 1/3 of food in the world is wasted; ingawa 1 in every 7 people are hungry (ingawa hili ni janga la kidunia sio Tanzania pekee)
 
Kwa vyovyote vile namuunga mkono waziri kwani wakulima tumeanza kupata faida kwa uhakika huyu waziri anatutetea
 
Mkuu, unamaanisha kuna sehemu wakaulima wanauza au wameuza mahindi kwa bei ya mwaka jana (Aftatu) ?

Suala jingine naona kama una ignore the role of "value chain"....

Sekta ya kilimo (kutoka shambani hadi mezani) ina wahusika (actors) wengi sana hapo katikati na wote wapo kihalali.

Ni kama ilivyo kwenye sekta zote zingine za kiuchumi (madini, utalii, uvuvi, mifugo, usafirishaji, n.k).

Kama mkulima anaendelea kumuuzia mfanyabiashara mahindi kwa bei ya mwaka jana, wakati gharama za uzalishaji zimepanda na pia bei ambayo mfanyabiashara anaenda kuuza hayo mahindi imepanda, huo ni uzembe wa mkulima.
Mkuu unaongelea wakulima / Farmers wakati majority ya ndugu zetu huko kijijini ni peasants..., ni kwamba wengi wana gunia mbili au tatu wengine hata moja...., kwahio kinachofanyika dealers / traders wanakusanya kidogo kidogo kutoka kwenye kila kaya / watu ili mzigo ukiwa mkubwa wanaleta usafiri na kufikisha mzigo sokoni...

Hapo utaona kwamba they are necessary (sababu bila wao huenda hata mzigo usingefika sokoni) ila utaona kwa jicho jingine ni kufeli kwa wizara kwa kutokuhakikisha soko linawafuata wakulima (kupunguza middlemen) ili mkulima anufaike zaidi....

Kwanza haya mambo ya kila mtu kulima teknolojia ya sasa watu wachache / vikundi vichache / mashine chache zinaweza kulisha Nchi nzima (automation) na kwa kutumia precision farming eneo dogo tu linaweza kutoa mazao maradufu (ila ndio hivyo tena Sera mbovu za Nchi)
 
Sasa wewe ndo umeelewa somo una akili.

Sasa baada ya wengi kuingia kulima mpaka wasio na Kazi rasmi na kupelekea mahindi kutapakaa kama unavyosema,
By the way unadhani kulima huku kwa kutegemea mvua ni kutupia tu mbegu na mazao hayo unavuna ?, unajua mambo ya ukame, unajua risk ya wadudu n.k. unajua kwamba mtu unaweza ukawekeza hata mbegu ulizoweka zisirudi ? Issue ni kwamba kwa miundombinu huu hata bei ikiwa vipi bado ni bahati nasibu (storage zenyewe za kusuasua unaweza ukahifadhi mahindi ukakuta molds wameshafanya yao.....
jambo la msingi Serikali ifungue mipaka yote na kusiwe na longo longo mipakani Kama kipindi cha mwendazake lkn pia serikali kitengo cha (nation food) kinunue mahindi mengi kwa bei nzur ili bei zilizopo zisishuke zaidi ya nusu ya bei ya sasa.
Umeelewa.!??
Kwahio wanunue kwa bei elekezi ambayo ili huyu mkulima awauzie itakuwa sawa na hio wanayopata kutoka nje ? Wakishanunua wayatunze ili kuja kuuza wapi na kwa bei ipi ?

Issue ya maana ni kuongeza supply ya kutosha na kutafuta masoko na kupata masoko inabidi tuache ujanja ujanja na ku-maintain quality..., haya mambo ya kusema kwamba Magereza sijui wasilime ili watu binafsi ndio walime ni myopic thinking......
 
Kwa vyovyote vile namuunga mkono waziri kwani wakulima tumeanza kupata faida kwa uhakika huyu waziri anatutetea
Ni kama kumshukuru mtu kwa kukubakizia makombo....
  • Kuruhusiwa kuuza mazao ya nguvu kazi yako popote kwa bei kubwa iwezekanavyo ni haki yako wala tofauti na hapo ni unyangayi....
  • Kukosekana kwa vitendea kazi au gharama za uendeshaji kuongezeka ni uzembe wa wizara
  • Mfumuko wa bei kutokana na supply kutotosheleza ndani na kubaki ya kuuza nje bado ni uzembe.
  • Kushindwa kununua mzigo wakati bei ipo chini ili ku-balance wakati bei inapanda na kuepuka mfumoko wa bei bado ni uzembe...
Mwisho wa siku unasahau kwamba hata wewe mkulima bado ni mlaji na knock on effect kupanda kwa chakula kutapelekea kila kitu kupanda bei (hii ni necessity need na sio want) watu lazima wale...
 
Unasema issue ni kuongeza supply,kwani umeambiwa nchi haina chakula watu wanakufa????

Chakula kipo mzee, hapa tunazungumzia bei ambayo kwa mkulima anachekelea na mlaji analalamika.

Ndo maana tukasema wizara iseti standard price kama ili kwenye mafuta ya petrol, diesel. N.k
Bei hiyo imnufaishe mkulima ili ivutie wengi kuwekeza huko lkn pia bei ya kununua iwe rafiki kwa mlaji.!
KeyserSoze
 
Ni nini kinafanya bei ishuke wakati wa mavuno na kupanda muda ukipita baada ya mavuno... Je hujasikia watu wanasema mwaka huu mahindi machache huenda kukawa na njaa..., kama soko la nje ni infinity si ukiongeza supply ya kuuza nje ukatosheleza bado mzigo utabaki wa kutosha ndani na bei bado zikawa ahueni ?

Kwanini Bei imepanda nini kimetokea ?

Huwezi uka-set bei efficient way ni kuacha market ijiseti (binadamu hatuna uwezo wa kupanga bei we are not that efficient) njoo tu kwenye bundle za simu serikali ilijaribu kupanga bei matokeo yake bundle zimekuwa gharama zaidi...

Serikali inachoweza kufanya ni kununua bei inapokuwa ndogo zaidi kuongeza demand na kipindi cha bei kupanda kuachia mzigo sokoni (tofauti ya private sectors wanaomaximize profit kwa kuuza as much as they can get au kuficha mzigo mpaka bei zipande sana) serikali itaachia mzigo kwa reasonable prices...

Unaongelea Serikali isikupangie pa kuuza ila unasema ikupangie bei ya kuuza ? Je ukiambiwa debe lisizidi 1500/- wakati wewe labda mbegu yako ni premium na ina ingredients tofauti kama yale maji ya Mwamposa ?!!!
 
Sasa wewe ndo umeelewa somo una akili.

Sasa baada ya wengi kuingia kulima mpaka wasio na Kazi rasmi na kupelekea mahindi kutapakaa kama unavyosema, jambo la msingi Serikali ifungue mipaka yote na kusiwe na longo longo mipakani Kama kipindi cha mwendazake lkn pia serikali kitengo cha (nation food) kinunue mahindi mengi kwa bei nzur ili bei zilizopo zisishuke zaidi ya nusu ya bei ya sasa.
Umeelewa.!??
Naona akili yako imegota, kama unayo kweli!

Wewe unadhani hao watakaokimbila kilimo kwa sababu tu msimu mmoja bei ilikuwa juu sana utawategemea kuwa wakulima hao? Hizo gharama za kulima tu kwanza, na madeni chungu nzima juu yake (ikiwa pesa ya serikali inayotupwa shimoni); yote haya hayaingii akilini mwako!

Halafu eti unajiona umeeleza kitu cha kuuliza mtu kama ameelewa? Nielewe kitu gani ulichoeleza hapo!
 
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima.

Lakini ukiangalia kwa marefu na mapana hawa walaji sio kwamba wanasema mkulima apangiwe bei au pa kuuza bali wanalalamila bei zimepanda kuliko uwezo wao, kwahio nadhani Waziri atakuwa na myopic thinking kwa kudhani njia pekee ya kuzuia mfumuko ni kuzuia wakulima wasipate faida kubwa iwezekanavyo (ingawa nadhani hata hio faida wanapata walanguzi/ middle men na sio peasants ambao anajifanya kuwatetea)...

Kwa ufupi ukiangalia hili suala kwa ujumla wake ni kwamba amekosea/ tumekosea sehemu sababu kupata soko la nje sio vibaya bali ni baraka (kupata faida na watu kukuza uchumi wao) lakini kwa kuwa na demand kubwa kuliko supply kunaonyesha lack of long term planning kwa Wizara, na hapo ashutumiwe kwa kutokuwa na production ya kutosha kuweza kuuza nje na bado kubaki na mzigo wa kutosha ndani..., Mambo ya ukame tunayajua na yanatabirika kwahio ununuzi ungefanyika kabla na kuweka stock ya kutosha ili supply ikipungua waachie mzigo.

Na huko wanakotembeza bakuli hawashindwi kununua mahindi in volumes na kwa bei ya chini ili kuja kupunguza makali kwa kuongeza supply.

In short ni mengi ya kufanya kuliko kuendelea na mipasho (jambo ambalo sidhani kama ni moja ya majukumu yake)..., wananchi wanahitaji results na results ni bei ya chakula kuwa rafiki kulingana na kipato chao; kama wanashindwa kufanya hayo mimi kama mlipa kodi na bosi wao sioni umuhimu wa uwepo wao (tutaendelea kuuza nje na kulima na kulishana na hali itaendelea kuwa ngumu hivi hivi hata wasipokuwepo)
Njaa na ukame vinakuja mbele yetu,

Nazishauri mamlaka kuhakikisha WAZIRI BASHE anaondolewa au anakalishwa chini kuelimishwa Ili kujipanga na baa la njaa lijalo.

Nchi inatakiwa kuja na mkakati mkubwa kuhakikisha tunazalisha chakula Kwa umwagiliaji pembeni mwa maziwa makuu,

Yajengwe maghala makubwa kuhifadhi chakula.

Tuendelee pia kuomba maombi ya TOBA na REHEMA Kwa Nchi yetu Ili kuiponya Nchi na upanga na tauni juu ya nchi.

Aaamen
 
Naona akili yako imegota, kama unayo kweli!

Wewe unadhani hao watakaokimbila kilimo kwa sababu tu msimu mmoja bei ilikuwa juu sana utawategemea kuwa wakulima hao? Hizo gharama za kulima tu kwanza, na madeni chungu nzima juu yake (ikiwa pesa ya serikali inayotupwa shimoni); yote haya hayaingii akilini mwako!

Halafu eti unajiona umeeleza kitu cha kuuliza mtu kama ameelewa? Nielewe kitu gani ulichoeleza hapo!

Wewe unauona msimu mmoja, sisi tunazungumzia mapinduzi ya kudumu kwenye sekta ya kilimo.
Fungua ubongo wako.

Kama unaogopa gharama za kulima, tulia uuziwe kilo ya unga elfu 3.
 
Sasa una unavyojichanganya hapa.
Unakwenda kuzoa bodaboda na kuwapeleka kwenye kilimo kwa kutumia matokeo ya msimu mmoja, hicho ndiyo kilimo chenye manufaa?
 
Ni nini kinafanya bei ishuke wakati wa mavuno na kupanda muda ukipita baada ya mavuno... Je hujasikia watu wanasema mwaka huu mahindi machache huenda kukawa na njaa..., kama soko la nje ni infinity si ukiongeza supply ya kuuza nje ukatosheleza bado mzigo utabaki wa kutosha ndani na bei bado zikawa ahueni ?

Kwanini Bei imepanda nini kimetokea ?

Huwezi uka-set bei efficient way ni kuacha market ijiseti (binadamu hatuna uwezo wa kupanga bei we are not that efficient) njoo tu kwenye bundle za simu serikali ilijaribu kupanga bei matokeo yake bundle zimekuwa gharama zaidi...

Serikali inachoweza kufanya ni kununua bei inapokuwa ndogo zaidi kuongeza demand na kipindi cha bei kupanda kuachia mzigo sokoni (tofauti ya private sectors wanaomaximize profit kwa kuuza as much as they can get au kuficha mzigo mpaka bei zipande sana) serikali itaachia mzigo kwa reasonable prices...

Unaongelea Serikali isikupangie pa kuuza ila unasema ikupangie bei ya kuuza ? Je ukiambiwa debe lisizidi 1500/- wakati wewe labda mbegu yako ni premium na ina ingredients tofauti kama yale maji ya Mwamposa ?!!!
Kama umesoma vzr nilisema, ifanyike analysis ya input cost kwa ekar, harvest quantity ndipo utajua at least uuze kuanzia bei gani.
Ulichokisema nafikir ni sahihi lkn kumbuka serikali haiwez kuwa na pesa kununua kiasi kikubwa cha mavuno na hapa tunazungumzia mahindi tu lkn kumbuk kuna mpunga, maharagwa n.k

Kwa mara chache walipojarib kufanya hivyo miaka ya nyuma walinunua kwa wakulima wachache still wakulima wengi walibakiwa na mazao na kuyauza kwa bei ndogo sana.

Nafikir jambo la msingi tuongeze supply wakati serikal ikimaintain price kwa kufungua mipaka bei inapoonekana ndogo ( huge supply) na kufunga inapoonekana kuna viashiria vya mazao kupungua ( low supply).

Jambo la msingi bei ya mazao ivutie vijana kutambua kilimo ni ajira na biashara.
 
Imetokea kasumba mbovu ambayo mwisho wa siku ninaiita cheap politics na divide and rule..., Waziri amekuwa akijinasibu mtetezi wa wakulima kwamba hawapangii Bei na kuonyesha kana kwamba walaji ni wanyonyaji ambao wanataka kunyonya jasho la mkulima.

Lakini ukiangalia kwa marefu na mapana hawa walaji sio kwamba wanasema mkulima apangiwe bei au pa kuuza bali wanalalamila bei zimepanda kuliko uwezo wao, kwahio nadhani Waziri atakuwa na myopic thinking kwa kudhani njia pekee ya kuzuia mfumuko ni kuzuia wakulima wasipate faida kubwa iwezekanavyo (ingawa nadhani hata hio faida wanapata walanguzi/ middle men na sio peasants ambao anajifanya kuwatetea)...

Kwa ufupi ukiangalia hili suala kwa ujumla wake ni kwamba amekosea/ tumekosea sehemu sababu kupata soko la nje sio vibaya bali ni baraka (kupata faida na watu kukuza uchumi wao) lakini kwa kuwa na demand kubwa kuliko supply kunaonyesha lack of long term planning kwa Wizara, na hapo ashutumiwe kwa kutokuwa na production ya kutosha kuweza kuuza nje na bado kubaki na mzigo wa kutosha ndani..., Mambo ya ukame tunayajua na yanatabirika kwahio ununuzi ungefanyika kabla na kuweka stock ya kutosha ili supply ikipungua waachie mzigo.

Na huko wanakotembeza bakuli hawashindwi kununua mahindi in volumes na kwa bei ya chini ili kuja kupunguza makali kwa kuongeza supply.

In short ni mengi ya kufanya kuliko kuendelea na mipasho (jambo ambalo sidhani kama ni moja ya majukumu yake)..., wananchi wanahitaji results na results ni bei ya chakula kuwa rafiki kulingana na kipato chao; kama wanashindwa kufanya hayo mimi kama mlipa kodi na bosi wao sioni umuhimu wa uwepo wao (tutaendelea kuuza nje na kulima na kulishana na hali itaendelea kuwa ngumu hivi hivi hata wasipokuwepo)
Bashe yupo sawa, ngoja nguvu ya soko iamue. Watu wengi wanalima kwenye mitandao ya kijamii Sio kufanya Kwa vitendo. Wanasema Bei ya vyakula ni ndogo hebu watuambie kuwa kilmoja ya mahindi, maharage, mpunga ni sh ngapi. Nimekuwa mtafiti Kwa umri wa miaka 31, niwaambie mkulima hapati faida kubwa Kwa kile anachozalisha!
 
Umesoma nilochoandika hapa ?

Wapi nimesema mkulima apangiwe bei au pa kuuza ?

Kwanini mwaka huu bei ipo juu kuliko mwaka jana ? Kama nguvu ya soko imeamua sababu ni supply ndogo na sisi shida yetu bei iwe kubwa kwanini tusipunguze supply maradufu ? Utaona kwamba kuwa na supply ndogo hence bei kupanda ni uzembe wa wizara husika, na kinachofanyika sasa hivi ni kupiga siasa badala ya kufanya basics ambazo ni kazi / shughuli yake
 
Kama umesoma vzr nilisema, ifanyike analysis ya input cost kwa ekar, harvest quantity ndipo utajua at least uuze kuanzia bei gani.
production cost ya hapa na pale ni tofauti, quality inaweza kuwa tofauti mimi naweza kuwa na njaa kuliko wewe na nataka mzigo uishe haraka kwahio nikauza bei nusu na wewe...., Yaani mambo ya kupangia bei ni non-starter....

Mimi naweza nika-brand mzigo wangu na kuwapiga watu porojo kwamba mahindi yangu ni bora kuliko yeye, kuna issue za usafiri huenda mimi mbolea nilitengeneza mwenyewe sikununua na wala sihitaji dawa sababu nafanya crop rotation hence uzalishaji wangu ni wa chini na nina uwezo wa kuuza bei ya chini...
Ulichokisema nafikir ni sahihi lkn kumbuka serikali haiwez kuwa na pesa kununua kiasi kikubwa cha mavuno na hapa tunazungumzia mahindi tu lkn kumbuk kuna mpunga, maharagwa n.k
Serikali haina pesa, hizo pesa ni tozo zetu na kodi zetu kwahio inabidi wasifanyie mambo ya maana; pili kama wewe mwenyewe unasema kilimo kinalipa kwahio wakinunua wakati bei ni za ajabu na ni guarantee bei zitapanda kwahio wana uhakika hata wa kutengeneze tshs 100/= kwa kilo
Kwa mara chache walipojarib kufanya hivyo miaka ya nyuma walinunua kwa wakulima wachache still wakulima wengi walibakiwa na mazao na kuyauza kwa bei ndogo sana.
Hawakufanya kazi yao ipasavyo sababu kama masoko yapo na huko nje yapo kwanini hawakuwasaidia wakulima kupata soko;
Nafikir jambo la msingi tuongeze supply wakati serikal ikimaintain price kwa kufungua mipaka bei inapoonekana ndogo ( huge supply) na kufunga inapoonekana kuna viashiria vya mazao kupungua ( low supply).

Jambo la msingi bei ya mazao ivutie vijana kutambua kilimo ni ajira na biashara.
Sasa huoni hapo unasema kile ambacho hautaki Bashe akifanye (na mimi sioni kama ni jambo la maana sababu mwisho wa siku huko ndio kumpangia mkulima Bei) mimi nachosema waache watu wauze popote wanapotaka wakati wowote na ili ku-maintain bei za ndani wahakikishe stock ya chakula ya Taifa ni ya kutosha ili supply ikipungua waachie mzigo sokoni na kuhakikisha kwenye hio stock yao ni kwa ajili ya soko la ndani na sio la nje (yaani sio walanguzi kununua haya mahindi ya stock ya Taifa na kuyapeleka nje kwa magendo)
 
production cost ya hapa na pale ni tofauti, quality inaweza kuwa tofauti mimi naweza kuwa na njaa kuliko wewe na nataka mzigo uishe haraka kwahio nikauza bei nusu na wewe...., Yaani mambo ya kupangia bei ni non-starter....

Mimi naweza nika-brand mzigo wangu na kuwapiga watu porojo kwamba mahindi yangu ni bora kuliko yeye, kuna issue za usafiri huenda mimi mbolea nilitengeneza mwenyewe sikununua na wala sihitaji dawa sababu nafanya crop rotation hence uzalishaji wangu ni wa chini na nina uwezo wa kuuza bei ya chini...

Serikali haina pesa, hizo pesa ni tozo zetu na kodi zetu kwahio inabidi wasifanyie mambo ya maana; pili kama wewe mwenyewe unasema kilimo kinalipa kwahio wakinunua wakati bei ni za ajabu na ni guarantee bei zitapanda kwahio wana uhakika hata wa kutengeneze tshs 100/= kwa kilo

Hawakufanya kazi yao ipasavyo sababu kama masoko yapo na huko nje yapo kwanini hawakuwasaidia wakulima kupata soko;

Sasa huoni hapo unasema kile ambacho hautaki Bashe akifanye (na mimi sioni kama ni jambo la maana sababu mwisho wa siku huko ndio kumpangia mkulima Bei) mimi nachosema waache watu wauze popote wanapotaka wakati wowote na ili ku-maintain bei za ndani wahakikishe stock ya chakula ya Taifa ni ya kutosha ili supply ikipungua waachie mzigo sokoni na kuhakikisha kwenye hio stock yao ni kwa ajili ya soko la ndani na sio la nje (yaani sio walanguzi kununua haya mahindi ya stock ya Taifa na kuyapeleka nje kwa magendo)
Biashara na serikali wap na wapi!?

Refer korosho zilisumbua sana.!

Changamoto sidhani serikali kama ina pesa ya kutosha kununua mahindi mengi kiasi hicho. Jambo la 2 upigaji mwingi lazima serikali iingiliwe.
Serikali inamudu kununua mahindi ya tahadhali tu ikitokea mikoa 2 au 3 tu imekumbw na njaa ndo inaweza ika supply.
 
Biashara na serikali wap na wapi!?
Aisee naona tunazunguka tu...., Issue hapa sio Biashara (as much profit as possible) bali issue ni safety net ya kuepuka mabaa ya njaa ambayo huwa yanatokea; tunajua kabisa supply inapanda na kushuka sasa kwanini kusiwe na stock ya kutosha ya Taifa ? Kama unajua lazima within 12 months kuna uwezekano wa chakula kupanda kuna ubaya gani kununua wakati bei ni za kutupa na kuyauza bei zinapokuwa za juu sana ? kama within two years bei zipo za kawaida unaachia hata mzigo huo nchi jirani au kuwashauri wakulima kwamba kwa sasa stock ya mpunga ni kubwa sana kwanini msijikite zaidi kwenye mahindi.... Wewe unaongelea biashara mimi naongelea well being ya jamii (na bila chakula hakuna jamii) Hizi sio perfume ambazo mtu ataamua kukaa na kunuka kikwapa ni chakula ambacho kama hana atakuibia au kuchukua chako....
Refer korosho zilisumbua sana.!
Hivi unajua korosho ni cash crop ? sasa ununue korosho ikiwa chini ili mwisho wa siku uuze wapi wakati soko ni hilo hilo la nje hapo unaweza kuwafungulia wigo watu ili mwenye nguvu more money apate mzigo ni tofauti na unapoongelea staple food
Changamoto sidhani serikali kama ina pesa ya kutosha kununua mahindi mengi kiasi hicho. Jambo la 2 upigaji mwingi lazima serikali iingiliwe.
Serikali inamudu kununua mahindi ya tahadhali tu ikitokea mikoa 2 au 3 tu imekumbw na njaa ndo inaweza ika supply.
Nani kasema wanunue yote nimekwambia wanafanya balancing hata wakinunua ya mkoa mmoja tu ni kwamba zile gunia ambazo zingekwenda kariakoo na kushusha bei sasa hivi zitapungua kwenda Kariakoo na zitatunzwa hence supply itapungua..., na kipindi supply ikiwa ndogo kama zikishushwa gunia elfu kumi nchini huoni kwamba zitaongeza supply
 
Aisee naona tunazunguka tu...., Issue hapa sio Biashara (as much profit as possible) bali issue ni safety net ya kuepuka mabaa ya njaa ambayo huwa yanatokea; tunajua kabisa supply inapanda na kushuka sasa kwanini kusiwe na stock ya kutosha ya Taifa ? Kama unajua lazima within 12 months kuna uwezekano wa chakula kupanda kuna ubaya gani kununua wakati bei ni za kutupa na kuyauza bei zinapokuwa za juu sana ? kama within two years bei zipo za kawaida unaachia hata mzigo huo nchi jirani au kuwashauri wakulima kwamba kwa sasa stock ya mpunga ni kubwa sana kwanini msijikite zaidi kwenye mahindi.... Wewe unaongelea biashara mimi naongelea well being ya jamii (na bila chakula hakuna jamii) Hizi sio perfume ambazo mtu ataamua kukaa na kunuka kikwapa ni chakula ambacho kama hana atakuibia au kuchukua chako....

Hivi unajua korosho ni cash crop ? sasa ununue korosho ikiwa chini ili mwisho wa siku uuze wapi wakati soko ni hilo hilo la nje hapo unaweza kuwafungulia wigo watu ili mwenye nguvu more money apate mzigo ni tofauti na unapoongelea staple food

Nani kasema wanunue yote nimekwambia wanafanya balancing hata wakinunua ya mkoa mmoja tu ni kwamba zile gunia ambazo zingekwenda kariakoo na kushusha bei sasa hivi zitapungua kwenda Kariakoo na zitatunzwa hence supply itapungua..., na kipindi supply ikiwa ndogo kama zikishushwa gunia elfu kumi nchini huoni kwamba zitaongeza supply
Impact yake naona ni very minute.!
 
Impact yake naona ni very minute.!
Impact gani ?

Hivi unaweza ukaniambia matumizi ya nafaka kwa mwezi kwa nchi ni kama tani ngapi ? Na kama kutoka store bei zikianza kupanda wakiachia 0.005 ya mzigo sokoni hautaleta tofauti ? na wale ambao wanangoja bei ifike ili watoe mzigo store wakijua kwamba haitafika zaidi ya mara mbili si wataendelea kuuza tu au ?
 
wacha wakulima wapate,ukiona bei ya vyakula iko juu nenda shamba kalime uuze kwa bei ya juu na wewe
Haya mawazo ya kumtaka kila anayehoji kupanda Kwa bei ya chakula naye aende akalime ni ufinyu wa kufikiri. Mfano Walimu, maaskari, marubani, madaktari na wote walioajiriwa Ili wawahudumie hao wakulima Kwa namna moja au nyingine wote waende kulima? Chakula chenu lazima kiuzwe Kwa bei wanayoweza kuiweza, vinginevyo ni sawa na kusema hao wakulima wasitusumbue kuleta wagonjwa wao mahospitalini Ili siye pia tupate muda wa kulima kama mnafikiri hiyo ndiyo solution. Vivyo hivyo muwe na shule, magereza, vyombo vyenu vya usafiri wenyewe nk. Issue hapa ni kwamba lazima serikali itafute namna iliyo Bora na isiwe issue ya kutishana ati kila anayelalamika akalime. Familia Bora inapimwa Kwa utoshelevu wa vitu vya mhimu Cha kwanza ni chakula, ni sawa sawa na nchi.
 
Back
Top Bottom