Majukumu ya Waziri wa Kilimo ni yapi?

Kupanda kwa bei ya chakula ni jambo zuri kwa uchumi wetu. Zuri sana. Na hao 'walanguzi' walitokea sababu ya kuzuia kuuza mazao nje. Mpango huu wa Bashe utawamaliza
 
Familia iwe chakula na chakula cha kutosha kwani umeambiwa chakula hakipooo.!?

Aliye kwambia manesi au wakalime ni wapi hapo ebu quote?

Wadau wamesema wasio na kazi maalumu ndo wakalime mfano, ukienda mijini utakutana na vyombo vya usafir mdogo mdogo utitili.
Well wamejiajir baada ya kutoka vyuo lkn kwa nyongeza tupendekeza serikal iweke mazira ya kilimo kuwa biashara inayolipa pia ajira kwa wasio na ajira rasmi.

Issue ya walimu, askari hao ni wateja wetu tunawapigania mishahara waongezewe daima ili mzunguko kwa mkulima na wafanyabiashar wengine wanufaike kupitia wao.
 
Mkuu umesema kweli kabisa, nilishangaa nilikwenda fanya kazi mkoa fulani, nikakuta wakulima wameshauza mahindi yaliyoko shambani. Nilipodadisi wakaniambia ni kawaida ingawa huko nyuma haikuwa hivyo kwa kiwango hiki. Wenye mahindi kwa sasa ni wafanyabiashara wenye warehouses, au wanaokodi warehouses, na wametengeneza pesa nzuri tu.
 
Sasa amesema uongo gani mkuu, amekwambia wakulima waliuza mahindi tangu yakiwa shambani, so hawafaidiki na ongezeko lolote la bei la sasa. Hata kwa Mbeya kuna maeneno wana tabia ya kuuza mahindi tangu yakiwa shambani.
 
Sasa amesema uongo gani mkuu, amekwambia wakulima waliuza mahindi tangu yakiwa shambani, so hawafaidiki na ongezeko lolote la bei la sasa. Hata kwa Mbeya kuna maeneno wana tabia ya kuuza mahindi tangu yakiwa shambani.
Huenda unaishi mjini, mimi naongea kulingana na uzoefu maana ni mtoto wa mkulima lkn pia mahangaiko yng yapo jirani na wakulima wadogo.

Wakulima wengi huuza mahindi kidogo kidogo mpaka kulingana na shida yake kwa wakati huo, na wengi pia wanauza lkn wanabakisha wanauza december na january kwa ajili ya kununulia pembejea kuhudumia msimu mpya.
Kwa hiyo tusijumuishe kwamba mkulima ameuzia mazao shamban sio kweli labda mwenye dharura kubwa.
Mpaka sasa bado vijijini kuna vituo vinakusanya mahindi na kusafirisha.
 
Bashe afukuzwe uwaziri na uraia wake uhojiwe
 
Kumbe wakati tunasema tuuze nje tulikuwa tunakataza kununua nje ? (Hili ndio Soko Huria)!!!

By the way tungewekeza na kuhakikisha tunazalisha vya kutosha na kwa gharama nafuu nadhani kungekuwa hakuna haja ya kuagiza nje ?

Na tunaagiza kwa kiasi gani per kg na kwanini huko tunapoagiza bei ni ndogo kuliko hapa kwetu ?

Hilo inabidi lisitazamwe tu bali lifanyiwe kazi...
 
Mengi ya kufanya kama yapi? Mbona una bwabwaja bila majibu? Mjinga typical blaa blaa as usual za Mtanzania
 
Mengi ya kufanya kama yapi? Mbona una bwabwaja bila majibu? Mjinga typical blaa blaa as usual za Mtanzania
Aisee hata kusoma haujui ?!!!!

Moja kwenye post ya kwanza nimesema kwanini kama production imekuwa ndogo short term wasingetoa chakula nje (jambo ambalo naona wamefanya when its too late watu wameshaumia)

Mbili badala ya kuhangaika na kuwa reactive kununua chakula wangewasaidia wakulima wakati bei zipo chini kununua au kuhakikisha pembejeo zina gharama rafiki hence kupunguza gharama za uendeshaji...

Tatu kuhakikisha production inakuwa kubwa kila wakati hapo kutakuwa hakuna haja ya kuongelea kufunga mipaka kila mtu atauza anavyotaka popote anapotaka.

Kuhakikisha tuna storage ya nafaka kulisha nchi walau kwa mwaka mmoja hapo bei zinaposhoot wanaachia mzigo hence ku-balance bei
 
Ndio maana nimekuambia katika hao watu wenye akili ndogo na wewe upo

Sasa kama wakulima wangekuwa na mahindi hao bodaboda wangeangaika kutafuta debe debe Kwa wakulima?

Hizo bodaboda unazoziona hao sio wafanya biashara hao tunawaita wachuuzi

Wafanya biashara walishanunua mahindi tokea yapo shamba wakayavuna na kujaza katika maghala Yao Sasa hivi wanapiga pesa

Yani nyinyi Bashe amewajaza ujinga sana Kwa kujifucha katika mgongo wa wakulima kumbe mwenzenu anawanufaisha wafanya biashara aka mafisadi
 
Sawa.
 
Vipi unasemaje kuhusu kuruhusu mzigo kuagizwa kutoka nje ? Hapa bado anawatetea au anawaonea ?

Naomba maoni yako....
Tumelalamika mno imembidi aruhusu chakul/mchele kuingia Tz.

Kimsingi hiyo ni short team solution lkn tungevumilia tunge solve uhaba huu kwa long term stratergic ambazo zingetusaidia kwa kiwango kikubwa.

Kuna msemo mara nyingi unatumika naomba niutumie kurahisisha maana ya hii hali.

Wanasema "ukiwa hauna samaki, usiombe samaki bali omba zana na ujuzi wa kuvua samaki"

Tungetafuta namna ya ku incounter hii shortage ingesaidia kuwa stable kwa miaka mingi katika uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa manufaa ya mkulima na mlaji.

KeyserSoze
 
Tumelalamika mno imembidi aruhusu chakul/mchele kuingia Tz.
Unajua kwamba chakula ni basic need ? Unajua kwamba chakula ndio nishati ya binadamu ili afanye kazi nyingine sasa kama hata una tractor lako halina mafuta ya kutosha unategemea litalima ?

Wala watu hawakupaswa kulalamika ndio wafanye wangehakikisha hata hayo malalamiko hayatokei na kama ni bahati mbaya majanga yametokea wangekuwa tayari wana stock / suluhisho la kufanyika kama majanga yatatokea na last resort ndio hii kuagiza kutoka nje...

Wewe usilazimishwe kuuza sehemu moja (uza hata nje) ila na usiwanyime watu chakula cha bei wanayomudu eti tusinunue nje wakati wewe bei unayotoa haiendani na buying power yao / income
Kimsingi hiyo ni short team solution lkn tungevumilia tunge solve uhaba huu kwa long term stratergic ambazo zingetusaidia kwa kiwango kikubwa.
Kwanini hizo long term strategies hazikufanyika tangia miaka mitatu huko nyuma ? kwanini kama hao wa nje wanaweza kuuza mzigo kwa bei ya chini na wewe unapofika nchini na wewe usiige wanachofanya ili uwauzie ?
Kuna msemo mara nyingi unatumika naomba niutumie kurahisisha maana ya hii hali.

Wanasema "ukiwa hauna samaki, usiombe samaki bali omba zana na ujuzi wa kuvua samaki"
Nani ni mvuvi na nani ameomba samaki ? Mvuvi ni wewe (mkulima) na Serikali yako ingebidi ikupe ujuzi huo tangia miaka ya huko nyuma ili leo uweze kuvua samaki ya kulisha familia yako (walaji) sasa wewe umeshindwa kulisha familia alafu unataka hata kwa jirani tusichukue kwa bei nafuu (unataka tufe)? Kwahio hapo kosa la nani ? Mlaji au Wizara ?
Tungetafuta namna ya ku incounter hii shortage ingesaidia kuwa stable kwa miaka mingi katika uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa manufaa ya mkulima na mlaji.

KeyserSoze
Shortage ni kuongeza supply na storage ili ikitokea issue kama hii kubalance bei isifumuke..., wala pia na mimi sikubaliani mkulima apangiwe sehemu ya kuuza vilevile sikubali kabisa kwamba ninunue mazao bei mbaya hapa ndani wakati kuna kodi zangu zishakusanywa na zinaweza kuleta mazao ambayo yatapunguza bei (ingawa hio pia ni kufuja pesa kwa nchi yenye ardhi kubwa) best scenario ni kuhakikisha kuna supply ya kutosha hadi kubaki for storage ya kutosha atleast mwaka mzima
 
Muendelezo wa Divide and Rule....; Sasa hivi ni kosa la Wafanyabiashara kwa kuuza Sukari bei juu
 
Kupanda kwa bei ya chakula ni jambo zuri kwa uchumi wetu. Zuri sana. Na hao 'walanguzi' walitokea sababu ya kuzuia kuuza mazao nje. Mpango huu wa Bashe utawamaliza
Vipi kupanda kwa Sukari ?
 
Vipi kupanda kwa Sukari ?
Inategemea na sababu ya kupanda. Kama kupanda ni sababu amepatikana mteja aliye tayari kununua kwa bei nzuri ni jambo zuri sana. Lakini kama bei imepanda sababu ya hila chafu za cartels na monopoly mbovu basi ni jambo baya.
 
Inategemea na sababu ya kupanda. Kama kupanda ni sababu amepatikana mteja aliye tayari kununua kwa bei nzuri ni jambo zuri sana.
Sasa kama wateja wanapatikana wa kununua kwa Bei kubwa wakati kuna Bei ndogo si watakuwa wajinga kununua kwa bei kubwa ? Hapo utaona kwamba supply imepungua (demand ni kubwa zaidi)
Lakini kama bei imepanda sababu ya hila chafu za cartels na monopoly mbovu basi ni jambo baya.
Hizo ni Siasa za wanasiasa always blaming the other guys, for their incompetent. Kama hao so called wafanyabiashara waliamua kuchukua risk ya kununua sukari wakati bei chee kwa ku-bet kwamba itapanda na ikapanda fair to them..., Sababu isingepanda wangekula hasara wala hakuna ambaye angewasaidia....

In short Price Setting (Kupanga Bei) does not and has never worked
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…