Makabila haya mtu ukifanikiwa jiandae kujaza ndugu tegemezi kwako ama kukuomba misaada kila mara, ukikataa unaonekana huna undugu

Mtanzania akipata unakuwa mwanzo wa choyo. Utakuta yeye na babake waliwahi kufanya hivyo kipindi hajapata kazi na hii simu janja ya kibinafsi.
 
Ambao nina uhakika nao kujazana kwa ndugu:
-Wasambaa
-Wazaramo
-Watu wa kusini

Ukioa huko jiandae kisaikolojia [emoji23][emoji23][emoji23]
Watu wa kusini bwana ni balaa , kijana mmoja alitoka kimaisha ukoo pamoja na kijiji kizima kipo kwake wanapishana siku tu za kukaa.
Yaani hadi mtu aliyeoa binamu yake
 
Hahahahah, eti Warangi..., mbona mnahangaika sana na Warangi.., mara hili mara kile , duuh
 
Mpendwa uliyoandika ni ukweli asilimia mia sitasahau wifi yangu tulipo mtembelea kwake akatukaribisha na chai ya moto mchana wa jua la saa saba😬Mhaya dadekii ana roho mbaya yule sikuwahi kuenda tena kwake ni miaka kama 10 .
 
Hakuna Kama warangi hao ni nambari moja

1. Warangi
2warangi
3.warangi

4 ndo hayo makabila mengine


Kuna watu hawawezi kuona kwa kina mtu flani kwao wako wawili tu na Kila mtu Ana chumba chake ..utasikia mtu anakwambia hivi si umchukue mtoto wa flani mbona hapo kwako Kuna nafasi kubwa tu ,, huku yeye kapanga anakwambia ingekuwa Yeye Ana nyumba angewachukua 😁
 
Amelaaniwa amtegemeae nduguye
 
Mama mkubwa Ana mtoto wa Kaka yake anamsomesha baada ya Kaka yake kufariki

Sasa Kuna likizo moja huyo mtoto wa Kaka ake akaja na mwenzake😁 ma mkubwa akasema alijua kesho yake anasepa kumbe kaja pale likizo nzima 😁 alitoa kauli moja aende kwao au arudi shule
 
Nimeoa mnyakyusa huu uzi unanchoma kimyakimya yaani nasoma comments taratibu kujifariji[emoji28]
Nipo kwenye mchakato wa kuoa Mnyakyusa wa kuzeekea mkuu. Nipe siri angalau mbili tatu kuhusu hawa watu ili nijipange vizuri [emoji16]
 
Wewe kabila gani? Declare your interest first, African traditions are almost similar,we live in communal societies, kusaidiana ni Jambo la kawaida Sana. Hizo selfish ideas Ni maisha ya kibepari. Waafrica tunashirikiana katika Raha na shida, ndiyo maana hatuna makampuni ya kuzikana.
Acha ubinafsi na uchoyo,Nani alikudanganya Kuna kufa kuzuri,ufe masikini au tajiri Bado umekufa tu.
 
Hii Ni tabia ya watz wote kubebana,ama kujuana ,hata ukiwa na jiran anakubebw
 
wasambaa kwa tabia hizo ndo wenyewe hao ukoo mzima utahamia kwa ndugu au kama mtoto wao kaolewa na mume mwenye unafuu wa maisha basi timu nzima itaweka kambi ya pre season hapo nyumbani
...Uongo. Wasambaa hawana Tabia hiyo! Yuko radhi akabebe matenga ya nyanya sokoni ajitegemee kuliko kukaa Kwa ndugu. Ni Mtu wa Kazi. Jiulize idadi kubwa ya wabeba mizigo Kariakoo na Wasukuma mikokoteni ni Kabila Gani....!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…