NAGAMAHONGA
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 11,131
- 9,301
Mtanzania akipata unakuwa mwanzo wa choyo. Utakuta yeye na babake waliwahi kufanya hivyo kipindi hajapata kazi na hii simu janja ya kibinafsi.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sukuma gang! Au nasema uwongo ndugu zangu?Umewasahau wasukuma..
#MaendeleoHayanaChama
Wewe utakua msukuma wa mchongo...ila kama ni msukuma.Wasukuma hatuko hivyo hata siku moja ,wasukuma ni watu wa kazi kazi
Watu wa kusini bwana ni balaa , kijana mmoja alitoka kimaisha ukoo pamoja na kijiji kizima kipo kwake wanapishana siku tu za kukaa.Ambao nina uhakika nao kujazana kwa ndugu:
-Wasambaa
-Wazaramo
-Watu wa kusini
Ukioa huko jiandae kisaikolojia [emoji23][emoji23][emoji23]
Bado wanaendelea.Hawajaacha hii tabia mpaka leo?
Wanyakyusa mbona hatuko ivo
🤣🤣🤣🤣🤣🙌ila hii ya ndugu wa mbali tunayo[emoji3] unaelekezwa ndugu mpaka unashangaa[emoji3]
Mpendwa uliyoandika ni ukweli asilimia mia sitasahau wifi yangu tulipo mtembelea kwake akatukaribisha na chai ya moto mchana wa jua la saa saba😬Mhaya dadekii ana roho mbaya yule sikuwahi kuenda tena kwake ni miaka kama 10 .Ila kuna Wahaya jamani[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwanza kitendo cha kuja kwake bila taarifa,umekwishaaa!!!Hawanaga aibu,chakula kwa mhaya kinamuumiza sana ni heri kidogo mhaya wa kijijini anaweza kukuvumilia coz utakula vinavyotoka shambani but jichanganye eti unaenda kwa Mhaya aishie town na hasa Dar! !Ukibahatika sana utakaa 3 dayz tena za kupewa makavu live kila siku,ukiondoka hapo kamwe hutokuja ukanyage pale tena
Hakuna Kama warangi hao ni nambari mojakuna hii tabia inakera sana kuna baadhi ya watu katika makabila flani wakishaona ndugu / kaka / dada yao katoboa ama ndugu yao wa kike / dada yao kaolewa na mtu mwenye maendeleo si haba basi huenda kujazana huko. Wanakula na kulala hapo bila kazi maalum.
Nyuma ya hii tabia hakukosekani visingizio vya oh tuna umoja, oh tunajaliana, oh sisi wakarimu, n.k lakini haibadilishi uhalisia wa hii tabia ya utegemezi. Hapa hatuzungumzii upendo au kujaliana, NO! Tunazungumzia ile tabia ya watu kujazana kwa ndugu, kaka, dada zao bila shughuli rasmi za kimaendeleo za kuwafanya nao wawe na maendeleo.
Kuna makabila kama wachaga, wakinga na wakurya hawa hawawezagi kuvumilia mtu kuja kukaa kwao awe tegemezi na wala si mgonjwa ama mzee. yaani unavyotoka huko kwenu uwe umeshatoa taarifa juu ya ujio wako, shughuli iliyokuleta, ratiba yako ikoje, upo mpaka lini, mipango yako n.k. Kama ni kusalimiana wala hakuna shida lakini sio kuzidi mwezi.
Hali hii ya makabila yanayolimbikiza utegemezi imewafanya hata ndugu zao wanaowalea wamejikuta wanashindwa kupanga maisha yao kwa kuelemewa na gharama za ulezi wa ndugu wasiopenda kujishug. unakuta mtu kakaa hata miaka miwili kwa ndugu na ni kijana mwenye nguvu ila bado hajahama kujitaftia pake na wala hana shughuli za kimaendeleo.
Makabila haya yaayojazana kwa ndugu ni kama
. Watu wa pwani - wazaramo, wasambaa, wadigo
. Wanyakyusa - hawa huwa wanaendeleza undugu hata ule wa mbali. Yaani hata mke wa mjukuu wa baba mdogo wa babu bado anahesabiwa kama ndugu, kawaida sana kukuta mnyakyusa ana ndugu 100
Waha na Wamanyema kutoka Kigoma
. , warangi
(Niliwaweka wabena kimakosa, hawa hawamo )
Amelaaniwa amtegemeae nduguyeMakabila yote ya Bara la Afrika yako hivyo.
Wangapi kila siku mnaomba Connection za kufikia UK, USA na South Afrika kwa Watanzania wenzenu?. Huuu ni utamaduni wa kiafrika kuuacha na kuiga Umagharibi ni suala la muda so tusilasimishe suala hili liiishe mara moja.
Huu ujinga mnaopeana hapa kwamba tusibebane ndio Maaana Watanzania hatupigi hatua Huko Ng'ambo.
Sammata hajavuta mtu EPL wala Ubelgiji, lkn angekuwa Mnigeria angewavuta kina Msuva, Manula nk lkn kwa huu ujinga mnaojazana hapa jamvini anawabania wengine, na hao wengine wanajiskia Vibaya kwenda kufikia kwa sammatta ili watafute maisha.
Hashim Thabit kamvuta nani??
Kikeke yuko BBC kamvuta nani???
Wengine wako WB, IMF Wamevuta kina nani??
Huko BOEING kuna Mnyakyusa kafanya nini kwa watanzania???
Wote hawafanyi kitu kwakuwa vichwani wamejaza UTI wa aina hii mnayodili hapa.
NENDA NIGERIA, nenda GHANA, Nenda CAMEROON akienda Rigobert Song lazima ALEX SONG naye aende na atoboe. Akienda KANU lazima aje OKOCHA.
Nenda SERBIA akienda Simba lazima aje MZUNGU na atatoboa.
Anyway: pale kwangu Kigamboni nina Wazinza kibaoooo kutoka Nkome Mchangani mpaka Kakubilo wako Daaaslam wanasaka Maisha. Wewe na Uzungu wako kazana kushupaza shingo na Umimi wako🙏
Nipo kwenye mchakato wa kuoa Mnyakyusa wa kuzeekea mkuu. Nipe siri angalau mbili tatu kuhusu hawa watu ili nijipange vizuri [emoji16]Nimeoa mnyakyusa huu uzi unanchoma kimyakimya yaani nasoma comments taratibu kujifariji[emoji28]
...Uongo. Wasambaa hawana Tabia hiyo! Yuko radhi akabebe matenga ya nyanya sokoni ajitegemee kuliko kukaa Kwa ndugu. Ni Mtu wa Kazi. Jiulize idadi kubwa ya wabeba mizigo Kariakoo na Wasukuma mikokoteni ni Kabila Gani....!!!wasambaa kwa tabia hizo ndo wenyewe hao ukoo mzima utahamia kwa ndugu au kama mtoto wao kaolewa na mume mwenye unafuu wa maisha basi timu nzima itaweka kambi ya pre season hapo nyumbani