Makabila haya yanaongoza kwa ulevi Tanzania, yanaongoza kwa akili pia

Makabila haya yanaongoza kwa ulevi Tanzania, yanaongoza kwa akili pia

Na huo utabak kuwa ukweli,mm sitoki mikoa hiyo lakini nimekaa nao sana. Bila watu wa mikoani Dar ingekuwa kama bagamoyo tu
Ndio ukweli wenyewe sasa, [emoji419][emoji419][emoji419]
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Kuna rafiki yangu mngoni akiona mwanamke mzuri barabarani hata kama alikuwa akitoa stori ya maana kiasi gani husahau story yote hadi akumbushwe alichokuwa akisema! 😀
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] jamani nimecheka mbavu sina lol. Wangoni on the truck.
 
1. Wachagga: hivi kuna mchaga asiye kunywa pombe? Nahisi atakuwa anatumia dawa, ila hakuna asiejua wachaga kwenye utafutaji,akili na maendeleo pia.

2. Wanyakyusa: kwanza kabisa Mbeya hakujawahi kutokea njaa na mkoa wa Mbeya ukiacha kulima Tanzania kutakuwa na baa la njaa. Hawa watu wanapiga pombe sio masihara, pamoja na utumiaji huo wa kileo lakini Mbeya kuna maendeleo.

3. Wahaya: nani asiyejua wahaya darasani, vyuoni na maofisini? Kwa takwimu zisizo rasmi wanaongoza kwa kuwa na maprofesa wengi. Pamoja na usomi wao lakini kwenye pombe, sio watu wabana pesa. Inasemekana mwisho wa mwaka pombe za ghali kama Hennessy, Hennessy, Jack Daniels n.k ziliishajini Bukoba.

Bonus: Wahehe, kwanza ni wasomi wazuri tu, ni majasiri toka zamani lakini mitingi wanapiga sana. Sijui mengi kuhusu Iringa.

Sasa swali kwa msiokunywa pombe mbona maendeleo yenu ya kawaida kuliko wanaokunywa? Je, dhana ya pombe inasababisha umasikini ni kweli ama si kweli?
Hii haina tofauti na ile dhana ya ulaji wa samaki kupelekea kua na akili

Binafsi naona haya mambo hayana uhusiano wowote,hivi hao watu wa Israel ambao tunaaminishwa kua wana akili zaidi duniani hao wanapenda pombe ama ni walaji wazuri wa samaki?

Kua na akili ni kipaji kama vile kuwa na uwezo wa kuongoza,uwezo wa kuimba,uwezo wa kucheza mpira na mengine mengi
 
1. Wachagga: hivi kuna mchaga asiye kunywa pombe? Nahisi atakuwa anatumia dawa, ila hakuna asiejua wachaga kwenye utafutaji,akili na maendeleo pia.

2. Wanyakyusa: kwanza kabisa Mbeya hakujawahi kutokea njaa na mkoa wa Mbeya ukiacha kulima Tanzania kutakuwa na baa la njaa. Hawa watu wanapiga pombe sio masihara, pamoja na utumiaji huo wa kileo lakini Mbeya kuna maendeleo.

3. Wahaya: nani asiyejua wahaya darasani, vyuoni na maofisini? Kwa takwimu zisizo rasmi wanaongoza kwa kuwa na maprofesa wengi. Pamoja na usomi wao lakini kwenye pombe, sio watu wabana pesa. Inasemekana mwisho wa mwaka pombe za ghali kama Hennessy, Hennessy, Jack Daniels n.k ziliishajini Bukoba.

Bonus: Wahehe, kwanza ni wasomi wazuri tu, ni majasiri toka zamani lakini mitingi wanapiga sana. Sijui mengi kuhusu Iringa.

Sasa swali kwa msiokunywa pombe mbona maendeleo yenu ya kawaida kuliko wanaokunywa? Je, dhana ya pombe inasababisha umasikini ni kweli ama si kweli?
Wachaga wanakunywa pombe kwa akili wala siyo wote wanaokunywa pombe idadi kubwa ni ya wale wasiokunywa ila kuna kabila la wangoni, wamasai wote walevi hadi wanawake
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mtuache wangoni bhana, Kwan hamjui Ngono tamuuuuh? Hahahah
Miss u madame
Hahahaa ila mmezidi jamani. Chaaaa.

Miss u pia. Nipo mzima wa afya mie.
 
Kuna myahudi mmoja ni jamii ya Ashkenazi. Kuna mmoja alimuuliza katika jamii yote makundi manne ya wayahudi ninyi mna akili sana, hii imekuwaje?

Akajibu hakuna jamii iliyo na akili kusema kuizidi jamii nyengine yaani in nature iwe hivyo akasema hakuna. Isipokuwa sisi jamii ya Ashkenazi kwetu elimu imepewa kipaombele zaidi na tunahimizana na ni msimamo umewekwa tujikite kwenye elimu kuanzia utotoni mpaka tunafikia elimu za juu.

Ndiyo maana katika Ashkenaz kwa wilo tumewazidi wayahudi wenzetu na kwetu hili suala lilianza mda na machoni na akilini mwa watu ikajengeka kuwa; kwa kuwa sisi ni wayahudi basi kwa ujumla ikajengwa wayahudi ni jamii yenye akili sana.

Tukija kwenye mada yako napinga bandiko la Uzi wako kuwa hayo ni makabila yenye akili sana. Hakuna! Isipokuwa hayo makabila yalitangulia kupata elimu kuliko makabila mengine na wakaweka jitihada na kuhimizana kuhusu suala la elimu kuanzia ngazi ya familia mpaka ukoo ndiyo ikawa ni sababu zikajengeka nadharia kichwani kuwa ni makabila yenye akili.

Laiti serikali ingefanya jitihada za makusudi kwenye makabila mengine matunda yangeonekana. Jamii zilizo nyuma kielimu bado ni jamii ileile! Inahitajika nguvu ya nje uwasukume ili wafanye mabadiliko na kwa hilo serikali ikiamua linatokea ndani ya muda mfupi tu.

Hivyo, hakuna kabila lenye akili kuliko lengine. Hakuna jamii yenye akili kuliko jamii nyengine. Isipokuwa ni mikakati tu na kuisimamia hiyo mikakati.

Kingine cha ziada: Hayo makabila ya juu uliyoyataja kwa hapa Tanzania ukiangalia sehemu nyingi walizopewa wadhifa wa uongozi ili waongoze wanakuwa na matatizo sana. Mara nyingi kuendelea kwa hiyo Taasisi inakuwa ni issue ijapokuwa wengi wao wamesoma na wakapatiwa uwadhifa na uwingi huo huo wa waliyosoma ndiyo uwingi unaofanya uharibifu.

Kwa hapa ndipo ninapo amini akili ni kuondoa yale yote uliyoyasoma! Kilichobaki kichwani ndiyo akili.
 
Hivi unajua makabila haya wanyakyusa, wachaga na wahaya ndio wanaoendesha nchi kwa utajiri, usomi na maendeleo kidogo na wakinga pekua utajua
Hakuna mbantu anayeendesha hii nchi kwa muktadha unaouleta. Hii nchi inaendeshwa na watanzania wenye asili ya asia.

Wabantu tutabakia kwa kujiita wasomi na uchumi wa kati wa kutambia mbele ya wabantu wenzetu kuwa sisi ni matajiri.
 
Na huo utabak kuwa ukweli,mm sitoki mikoa hiyo lakini nimekaa nao sana. Bila watu wa mikoani Dar ingekuwa kama bagamoyo tu
Kabla ya uhuru na baada ya uhuru Dar ilikuwaje? Unafahamu kuwa wabantu wa mbali na hayo makabila walikuwa na majengo makubwa tu kariakoo na kufanya biashara na kujiwekeza kwa aina tofauti?

Ikiwa Dar bila watu wa mikoani ingekuwa kama Bagamoyo vipi hao waliyotoka mikoani imekuwaje mikoa yao haikuendelelea kabla ya Dar?
 
Germany ni kati ya nchi zinazoongoza kwa unywaji wa pombe na ni kati ya nchi yenye watu wenye akili sana na maendeleo makubwa kisayansi na kiuchumi. Somalia hakuna baa hata moja ila hali zao mnazijua
Miongoni mwa tamaduni ya wajerumani ni kufanya kazi na kusoma. Wanafahamu elimu ni nini na imewasaidiaje! Ndiyo maana elimu kwao haikufanywa ghali kama mataifa mengine.

Kunywa pombe nako ni utamaduni. Hakuna uhusiano baina ya pombe na akili. Kwa sababu makabila mengi ya kibantu unywaji wa pombe upo! Ikiwa pombe ni akili inakuwaje kwa makabila mengine ni tofauti na kichwa cha habari cha Uzi?

Naishia hapa kwanza.
 
Hivi unajua makabila haya wanyakyusa, wachaga na wahaya ndio wanaoendesha nchi kwa utajiri, usomi na maendeleo kidogo na wakinga pekua utajua
Unatudanganya mkuu, top ten ya billionaires ni wahindi na waarabu hakuna mbongo hata mmoja walikuwepo Mengi na Ali Mufuruki ambao they are no more.
 
Jibu unalo mwenyewe,kwanin wanywaji ndio wenye akili na maendeleo?
Na huo utabak kuwa ukweli,mm sitoki mikoa hiyo lakini nimekaa nao sana. Bila watu wa mikoani Dar ingekuwa kama bagamoyo tu
Mbona ukienda Mbeya , Kagera na Kilimanjaro maskini kibao tu,

Hapa dar kule temeke kuna mahali wanaita kwa wahaya ndio hao unasema wanaendesha uchumi wa Dar ?
 
Back
Top Bottom