Uchawi umekuwa ukisumbua jamii nyingi sana watu hulalamika kulogana ama kutupia mtu jini pale anapopiga hatua, malimbwata ya mapenzi, kutupiana mabusha, kufunga vizazi, wanga wa usiku, n.k.
Pamoja na haya, kuna haya makabila machache nimeona mambo ya uchawi ni adimu (sio kwamba hamna kabisa), ni ngumu kukuta hata waganga wa kuroga katika vijiji vya makabila haya, Mtu wa huku akitaka uchawi itambidi asasafiri kwenda makabila mengine kununua uchawi.
1. Wachaga - Huko kwao ni ngumu kukuta mambo ya uchawi, sehemu ya karibu kuupata uchawi ni kusafiri uende kwa waganga wapare
2. Wakurya - Huko kwao ni ngumu kukuta mambo ya uchawi, sehemu ya karibu kuupata uchawi ni kusafiri uende kwa waganga wajaluo ama wajita.
3. Wamasai - Huko kwao ni ngumu kukuta mambo ya uchawi, sehemu ya karibu kuupata uchawi ni kusafiri uende kwa waganga warangi ama wambulu (wairaqw)