mbenge
JF-Expert Member
- May 15, 2019
- 4,864
- 10,483
Mlundikano wa watu wa kabila ama dini moja katika maeneo ya kazi si jambo la maana hata kidogo kulijadili endapo kama vigezo vilivyotumika katika ajira zao havikuwa na ubaguzi wowote ule. Kama michakato ya kuwapata ilikuwa ni ya haki na haikuwa na upendeleo, na iliyozingatia vigezo vyote viendanavyo na sifa zao za kuajiliwa, sasa hapo kuna kosa gani kama umahiri wao ndiyo umewapa ajira hizo?Hoja ya ukabila haihusiani na kwamba wangapi wamesoma au la.
Kwanini ofisi ikiwa na viongozi labda wangoni au wahehe tusikute wahehe au wangoni wamejazana? Ni kwamba hakuna wahehe au wangoni waliosoma ?
Miaka ya Leo uniambie kuna kabila halina wasomi waliokosa ajira, lipo hilo ?
Sasa tuje kwa makabila hayo yanayojificha kwenye kivuli kwamba wamesoma. mfano ofisini kiongozi akiwa ni mchaga wanajazana wachaga, tukitumia kigezo cha elimu ni kwamba hata hao wengine wahaya, wanyakyusa na wasukuma hawawekwi kwa kuwa hawajasoma au ni ukabila?
Ofisini akiwa mhaya ni Kiongozi makabila yote mengine Hadi hao wengine wasomi unawatafuta kwa tochi, ni kwamba hawana elimu au?
Nadhani kuna shida ya ukabila ambayo haisemwi wazi ila ipo shida ya ukabila na udini nchi hii.
Kwamba unaajiri watu wa usafi wakabila lako mpaka walinzi kwasababu wamesoma mbona hoja inakataa kabisa, zaidi ya ukabila hakuna lingine hapo.
Kuna tasisi mpaka za serikali akiingia mojawapo katika hayo makabila basi unakuta wanaanza kujazana wao kwa wao, kupandishana vyeo, kupeana mikopo, n.k.
Kwa nini malalamiko kama haya hutokea katika maeneo yasiyo hitaji utaalamu wa hali juu!? Ukiangalia kada zenye kuhitaji elimu, utaalamu, weledi, na umahiri wa hali ya utakuta hakuna malalamiko kama haya.
Lazima tukubali kuwa hata vidole hutofautiana kwa urefu na matumizi yake. Lazima tuyape kongole makabila yaliyofanya uwekezaji mkubwa katika elimu, kwa kuwa kile kinachotokea hivi sasa ni matunda ya jitihada zao za muda mrefu.
Mbona ukienda katika mashirika ya kimataifa, unakuta mlundikano wa watu wa kabila ama dini moja lakini wote wameajiliwa kutoka nchi na mamalka tofauti!? Jamani elimu inalipa, kama mtu anakidhi vigezo acha apewe haki yake pasipo kuangalia dini ama kabila lake.