Makabila yanayopatikana Morogoro na wilaya yanakopatikana

Bwana Banzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 14, 2014
Posts
397
Reaction score
196
Morogoro ni mkoa mojawapo wenye MAKABILA mengi hapa nchini. Zifuatazo ni wilaya na MAKABILA yake

1. Halmashauri ya Morogoro: Hii wilaya maarufu kama Morogoro Vijijini, makabila yanayopatikana ni; Waluguru, Wakwere, Wakutu, na Wazaramo

2. Morogoro Mjini: Hapa wenyeji ni Waluguru.

3. Wilaya ya Kilosa: Wenyeji hapa ni Waluguru, Wakaguru, Wasagara, na Wazigua japo sio wengi, Wavidunda,

Pia soma: Wizara ya Utamaduni na Utalii: Nimeandika makala nzuri ya Morogoro, nimepigiwa simu na makampuni tisa ya utalii Arusha wakiuliza namna ya kufika

4. Mvomero: Waluguru, Wazigua (Wazigua wanapatikana kwa wingi hasa Turiani), Wasagara.

5. Kilombero; Wanapatikana Wandamba, Wapogoro, Wambunga, Wabena ( wanapatikana eneo kunaitwa Mbingu Ifakara)

6. Ulanga; Wapogoro

7. Malinyi; wanapatika Wapogoro na Wandamba .

Kama kuna kabila nimelisahau nitashukuru mkinikumbusha... maana Morogoro kuna makabila mengi na mengine sio maarufu sana. Ahsanteni
 
Kilosa wenyeji hasa ni wasagara, wakaguru na wavidunda ambao wanapatikana hasa pale KIDODI
Kwa waluguru kuwa ni wenyeji wa kilosa hapo umetuokota waluguru wanapatikana hasa wilaya yao mama yenye asili yao Huko MOROGORO VIJIJINI. matombo , kolelo nk
 
Wavidunda hatari Sana hao watu. Waligoma kuhama kupisha ujenzi wa bwawa la Kidatu wakahamia milimani wakafanya yao Hadi serikali kupitia Tanesco ikaingia nao mkataba. Inawasafirisha mara 2 Kila wiki kwenda mjini kupeleka mazao Yao Sokoni na kuwarudisha jioni, matibabu bure.
 
Alafu makaburi miaka ile walikuwa wanazika sebuleni enzi zile
 
Wavidunda hatari Sana hao watu. Waligoma kuhama kupisha ujenzi wa bwawa la Kidatu wakahamia milimani wakafanya yao Hadi serikali kupitia Tanesco ikaingia nao mkataba. Inawasafirisha mara 2 Kila wiki kwenda mjini kupeleka mazao Yao Sokoni na kuwarudisha jioni, matibabu bure.
Ha ha haa kweli Wavidunda kiboko
 
Back
Top Bottom