Morogoro ni mkoa mojawapo wenye MAKABILA mengi hapa nchini. Zifuatazo ni wilaya na MAKABILA yake
1. Halmashauri ya Morogoro: hii wilaya maarufu kama Morogoro Vijijini, makabila yanayopatikana ni; Waluguru, Wakwere, Wakutu, na Wazaramo
2. Morogoro Mjini: hapa wenyeji ni Waluguru.
3. Wilaya ya Kilosa: Wenyeji hapa ni Waluguru, Wakaguru, Wasagara, na Wazigua japo sio wengi, Wavidunda,
4. Mvomero: Waluguru, Wazigua (Wazigua wanapatikana kwa wingi hasa Turiani), Wasagara.
5. Kilombero; Wanapatikana Wandamba, Wapogoro, Wambunga, Wabena ( wanapatikana eneo kunaitwa Mbingu Ifakara)
6. Ulanga; Wapogoro
7. Malinyi; wanapatika Wapogoro na Wandamba .
Kama kuna kabila nimelisahau nitashukuru mkinikumbusha...maana morogoro kuna makabila mengi na mengine sio maarufu sana. Ahsanteni