Makabila yanayosifika kwa kutokuwa na ubinafsi

WANYAKYUSA - Ni watu wakarimu ila kwao kabila kwanza mengine badae, sehemu iwe na mwajiri, uongozi, mtoa michongo, n.k. mnyakyusa utajua tu, kweli kuna mambo ya kupeana pasi lakini kwa wanyakyusa ni wazi zaidi na kwa kiwango kikubwa kupitiliza bila
Miaka ya nyuma kulikuwa na boss mmoja alikuwa Murugenzi wa Shirika la Bima NIC, aliitwa Gibbons Mwaikambo, alijaza watu wa kabila lake kwenye Shirika hilo.
Tukuyu na Kyela ilihamia hapo.

Pia Bodi ya Biashara ya nje, ( Board of External Trade) ilipokuwa chini ya Mbaruku Mwandoro, naye alijaza wadigo wenzake kutoka Mkinga.

TANESCO ilipokuwa chini ya Salvatori Mosha ilitia fora.
Kila mtanzania alifurahia kufanya kazi na bosi Mosha.
Mosha hakubagua mfanyakazi, uwezo wako ndiyo utakubeba.
 
Halafu nashangaa watu wanasema wachaga wabaguzi si kweli
 
Sio zamani tu ni mpaka leo, Meneja au HR awe mnyakyusa na kuna sheria hazimbani basi atajaza wenzake, hatukatai kuna mambo ya kuwekana lakini hawa wamepitiliza.

Halafu kwenye ajira tumeenda mbali, niliwahi kusoma humu Jamiiforums kuna jamaa aliweka kisa chake huko shuleni kwao kiranja au headboy akiwa Mnyakyusa basi ni upendeleo wa wazi kabisa kwa wenzake, basi kukiwa na uchaguzi watu wakawa wanaogopa kuchagua mnyakyusa πŸ˜‚ ni hivyo hiyyo hata ukifuatilia kwenye makanisa yao.
 
Nafanya nao biashara adi nikawowa uko ulichosema ni sahihi kabisa...

Uzuri salamu zao ni zile za kunong'ona na kujirudiarudi huwa naenda nao hvyohvyo
 
Cooments kibao wameishi nao vizuri labda ulikutana na wale wa Simiyu au ulitaka uanze kuleta vijisheria vyako vya huko kwenu ulikotoka
 
Wasukuma ni watu poa sana hasa wa shinyanga lakini hawa wa kizazi cha leo. Nilifanya kazi huko miaka ya 90 wakivuna mazao unaletewa zawadi kila siku karanga,maziwa,viazi,mahindi. Halafu sio washindani hata ukifungua biashara na sio kabila lao hupati shida.
 
Mimi ni Msukuma πŸ’― Miaka 25 iliyopita niliwahi kuishi Kwa Wasukuma wenzangu na Kwa bahati nzuri Kwa kuwa nilizaliwa na kukulia mjini, na pia mazingira ya shule nilizosoma, lafudhi yangu sio ya Kisukuma japo najua kuongea Kisukuma vizuri sana.
Sasa nilipokuwa nafanya shughuli zangu huko kwenye Vijiji vya Mkoa wa Geita nilijifanya sijui kabisa Kisukuma. Sometimes waliweza kunisema Kwa lugha ya Kisukuma wakijua kuwa Mimi sisikii.
Nikifanya hivi kama sehemu ya kujua ustaarabu wa Wasukuma Kwa makabila mengine..
Pamoja na hayo, nilioneshwa ukarimu wa hali ya juu sana na sikujiona mpweke.
Ukweli, Wasukuma ni wakarimu sana n Mimi huwa ni mkarimu sana na ninapenda sana utani. Ukikutana na Mimi nakuuliza kabila lako Kwa lengo la utani zaidi. Muda huo naanza kukutania as if tumefahamiana kitambo.
Hata sehemu yangu ya kazi, Kwa bahati nzuri ni kiongozi, ila utani Kwa subordinates wangu upo kama sehemu nje ya kazi.

Bhasukuma bhanho bha bhiza nu.
 
Ishi na wasukuma hujui hicho kisukuma chao uone hizo fursa kama utapata.
Hii ni kweli. Nakumbuka panel ya kuajiri mradi wa SGR walikuwa wasukuma wengi kuliko makabila mengine; automatically nafasi nyingi walikuwa wanapewa wa kabila hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…