Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 62,101
- 38,487
Habarini za jioni, asubuhi na mchana kwa walio huko mawindoni.
Nimewiwa kuuliza hili swali maana hivi majuzi nilifululiza kuzika ndugu na marafiki.
Katika kuchimba kaburi nimekutana na changamoto nyingi sana. Wakati wa kuchimba, wengine wanakutana na mifupa, wengine wanakutana na mafuvu, lakini marehemu anazikwa tu.
Nimehudhuria makaburi sehemu tatu.
Makaburi mawili yalikuwa mabaya sana.
1. Luventry
Haya yako njiani kuelekea Rainbow ukitokea Tankizima.
Aisee, kona ya pili kulia kuna makaburi. Kule usithubutu kuzika hata mbwa wako.
Kila wanapochimba ni mzigo, kisha wanaufukia na kuendelea. Inasikitisha sana.
Wakati tukisubiri kuzika, walikuja ndugu wakitafuta kaburi la ndugu yao.
Watatu wakasema, "Tumezika hapa," lakini mmoja akasema, "Tuendelee kutafuta."
Kwa bahati nzuri, kulikuwa na mtu anayeyafahamu makaburi ya pale, na marehemu waliokuwa wanamtafuta alikuwa dereva wa bodaboda.
Akasema, "Si mnatafuta Rey?"
Wakasema, "Ndiyo, aliyefariki kwa ajali ya bodaboda."
Akasema, "Basi mpo sehemu sahihi."
Aisee, sijui... mama yake yule alilia hadi akaanguka.
Walipoanza kumsaidia kutambua eneo, wakakuta kaburi jipya ambalo halijafikisha hata mwezi, likiwa juu ya mzigo.
Nashauri makaburi ya aina hii yafungwe.
Watu wanaogopa gharama za kwenda Mbweni kununua eneo la mazishi, lakini ukweli ni kwamba hali hii ni laana na ni kutowastiri marehemu ipasavyo.
Je, kwenu ni makaburi yapi mazuri ambayo hayana tatizo la kuchimba na kukuta mabaki ya mazishi mengine?
Ndiyo maana wengi huomba malipo makubwa kwa kufanya kazi hiyo ya kuchimba makaburi.
Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, na upendo wa Mungu Baba, na ushirika wa Roho Mtakatifu ukae nasi sote sasa na hata milele.
Amina.