Makadirio mbao kupaua nyumba vyumba 5 na sebule?

papa yna

Member
Joined
Jun 21, 2014
Posts
55
Reaction score
16
wadau wa ujenzi nawaomba munipe makadirio idadi ya mbao za 2*2 na 2*4 za kuweza kupaua mapaa manne nyumba yangu ya vyumba 5 na sebule na korido katikati yaani upana feet 24 na urefu feet 38 nitashukuru sana kwa mchango wenu.
 
mkuu unaweza ukawa na nyumba ya vyumba viwili lakini kubwa zaidi ya nyumba ya vyumba vitano, hakuna standardized size ya ukubwa wa chumba.. kwahio bila kujua actual floor size ni vigumu mtu kujibu chochote
 
mkuu urefu 38ft upana 24ft ukubwa
wa nyumba yangu nipe makadirio mkuu keysersoze
 
mbao za mita nne 2kwa4 = 75, 2kwa2 = 75 na 1kwa8 = 11. Bati za mita tatu = 73 jumla na kofia. misumari (a) ya bati = 15kg (b) 5" =6 kg, 4" = 15kg, 3" = 4 kg, 2.5" = 2 kg na 1,5" = 1 kg. (c) Kenchi waya = 6 kg.

Kwa mawasiliano zaidi email yangu ni komboemmanuel42@gmail.com

Nataka kutengeneza frame za maduka around 5m kwa 20m nataka roof iwe single slope itakuwa kiasi gani full materials and labour cost
 
Ni sawa na kuuliza ubora wa viazi kwenye keypad. Nenda sokoni ndo ujue ubora wa viazi na ununue.
1. Tafuta fundi mpeleke site kama ushaanza kunenga akupe hesabu au 2. weka ramani ya roof " roof plan" yenye vipimo, section ya nyumba kufaham urefu wa paa na aina za mbao zitakazo tumika na floor plan pia ndo wataalam wafanye hesabu otherwise utapata guess-estimate.. Juu/chini sana.
 
kwanza nikushauri tumia 2*3 badala 2*2 zinaleta ufanisi wa kazi ikizingatia 2*2 za siku hizi ni kama 1.5*2.
2*4 kwaajili ya makenchi hazina shida. kwaio kwa vipimo hivyo na kama paa litakua kama ulivyosema kutakuwa na kenchi 3 nzima ambazo zitatumia mbao 8 kwa moja hivyo zitakua 24. kutakua na nusu kench 6 ambazo ni mbao 4 kwa moja.hivyo zitakuwa 24 pia. kutakuwa na mbao za mtamba panya 11. kwa hivyo 24+24+11=59 (2*2).unaweza ukaongeza 4.
na hizo za kushikia bati ziwe 26 unaweza ukaongeza 4 pia kwa hizi.
 
jamani kama haujui kitu nyamaza na uwe mtazamaji tu. sisi mafundi ndio tunatakiwa kusema kama kunamapungufu ktk maelezo yake. kwangu nineona yanajitoshereza.kasema boma lina futi 24x38. futi moja ni sawa na sm. 30.5 hivyo 24x30.5 = 735.sm na futi 38x30.5 = 1159 sm
 
wadau wa ujenzi nawaomba munipe makadirio idadi ya mbao za 2*2 na 2*4 za kuweza kupaua mapaa manne nyumba yangu ya vyumba 5 na sebule na korido katikati yaani upana feet 24 na urefu feet 38 nitashukuru sana kwa mchango wenu.

Kwa wengine hiyo ni sebule tu.
 
kwanza nikushauri tumia 2*3 badala 2*2 zinaleta ufanisi wa kazi ikizingatia 2*2 za siku hizi ni kama 1.5*2.
2*4 kwaajili ya makenchi hazina shida. kwaio kwa vipimo hivyo na kama paa litakua kama ulivyosema kutakuwa na kenchi 3 nzima ambazo zitatumia mbao 8 kwa moja hivyo zitakua 24. kutakua na nusu kench 6 ambazo ni mbao 4 kwa moja.hivyo zitakuwa 24 pia. kutakuwa na mbao za mtamba panya 11. kwa hivyo 24+24+11=59 (2*2).unaweza ukaongeza 4.
na hizo za kushikia bati ziwe 26 unaweza ukaongeza 4 pia kwa hizi.

Pandel ebwana asante sana. Sasa kaka jee unazungumziaje 2X2 za Sao Hill? Hawa jamaa bei yako iko juu lakini nadhani quality yao ipo juu zaidi.
 
kwanza nikushauri tumia 2*3 badala 2*2 zinaleta ufanisi wa kazi ikizingatia 2*2 za siku hizi ni kama 1.5*2.
2*4 kwaajili ya makenchi hazina shida. kwaio kwa vipimo hivyo na kama paa litakua kama ulivyosema kutakuwa na kenchi 3 nzima ambazo zitatumia mbao 8 kwa moja hivyo zitakua 24. kutakua na nusu kench 6 ambazo ni mbao 4 kwa moja.hivyo zitakuwa 24 pia. kutakuwa na mbao za mtamba panya 11. kwa hivyo 24+24+11=59 (2*2).unaweza ukaongeza 4.
na hizo za kushikia bati ziwe 26 unaweza ukaongeza 4 pia kwa hizi.

umesahau mbao za kona
 
Back
Top Bottom