Makadirio ya Gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu 3

Makadirio ya Gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vitatu 3

Huu Uzi Jamani
Katika Ujenzi
Ni vyema kuweka miundombinu ya kisasa kama vile umeme, simu (intercom), nyaya za televisheni, Kiyoyozi, na hata Data.

Kwa mjuzi wa haya Mambo waya za data,simu wkt wa wiring zinawekwa/kujengewa sehemu gani pale nyumbani
 
Habarini wakuu, naomba kama kuna mwenye uzoefu anipe makadirio ya gharama ya ujenzi wa nyumba ya vyumba vi 3 (chumba kimoja self na viwili vya kawaida), sitting, dinning, jiko, (choo na bafu public).

Nataka kutumia matofali ya kuchoma ambapo tofali moja linauzwa sh 120.

Msingi utatumia matofali ya block.

Heshima kwenu.
Shilling 200,000,000/-
 
Ukitaka kutafuta gharama halisi au makadirio kwamba ni kiasi gani cha fedha utatumia katika kujenga unaweza usijenge kabisa kama kipato chako ni cha kuungaunga, mambo hayo yanawafaa wenye uhakika wa fedha, au wale wanaochukua mikopo kwa ajili ya ujenzi. Mwanzoni mwa miaka ya 2000 nilipata zari nikapata kiasi cha fedha nikaweza kununua kiwanja maeneo ya Yombo Vituka. baada ya kununua hicho kiwanja sikuwa na pesa nyingi ambayo ingeweza kuanzisha ujenzi. Nikatafakari sana nikaibuka na wazo la kuwa ninaenda site kila Jumamosi hata kama nina fedha ya kununua mfuko mmoja wa simenti na kumlipa fundi wa kufyatua. Nilienda mwendo huo mwaka haukuisha nikawa nimemaliza nyumba. Nilipokuja kujumlisha hesabu sikuamini ni wapi ningeweza kupata kiasi hicho cha pesa kwa mara moja au hata kwa awamu nne!
Mwisho mwa maelekezo yako umeenda vzr Sana, hapo mwanzoni sijui ulikuwa unaandika ukiwaza papuchi?? Haya Mambo yaende taratibu...nimegombana na shemeji it enzi hizo najenga, kwamba tunajenga kwa mshahara wa kila mwezi akabisha. Mzee laki mbili mbili tu ilimaliza nyumba enzi hizooo sio leo. Weka malengo kuwa na subra, ishi kwa urefu wa kamba yako, acha Tamaa ya mijengo Anza taratibu
 
Kama hela ni ya kuunga unga Ujenzi ni mchakato mrefu asee,mi mwenyewe nimebaki nimeduwaa tu nawaza pa kuanzia
 
Kama hela ni ya kuunga unga Ujenzi ni mchakato mrefu asee,mi mwenyewe nimebaki nimeduwaa tu nawaza pa kuanzia
Mkuu nishakusoma kasoro uliyonayo.

Aidha unatamaa
Na umekata Tamaa ya kuishi na maisha

Huna malengo Ila una ndoto.

Kukisaidia.....Anza kubadili tabia. Unajua choo? Fikiria kuanza hata na choo Ni lengo, Anza na chumba kimoja. Angalia vzr Kama una umri wa chini ya 30 au 40 yawezekana huna majukumu laiti ungekuwa na majukumu hata chumba kimoja tu ungeishi ukiwa unajipanga

Kwanza Anza na kiwanja, usiogope kununua ndani ndani ambako watu wanapakimbia, jua hapo ndiyo penyewe.

Watanz hawataki kujiandaa. Jiandae kwa kuishi mbali ili uje upate eneo kubwa la kuishi badala ya kufikiria juu Sana wakati hujaandaa
 
Kuna mdau anataka kuanza ujenzi Nampa big up ila maandalizi yake anasema amefyatua tofali mwenyewe 4000 kwa gharama ya mfuko WA cement 19000,naomba kujua cement hiyo ni Tanzania hii hii au maana mtaani kwetu cement 12000- 13500,swala LA msingi je hizo gharama anapewa tu na fundi then ye anatoa hela? Maana ushauri ukitaka kweli kujenga buildings material inabidi uzunguke maduka kadhaa kufananisha bei vinginevyo utauziwa mfano WA cement 19000 wakati uliyemtuma kalipa 12500,huoni utakuwa unaibiwa kwa uvivu wako au ni contractors company ndio kakupa bei hiyo.
Huku mikoani kama shinyanga, geita, musoma na katavi cement ni Tsh 19,000/=
 
M10 tu inatosha gharama kubwa hapo bati na mbao Labda na fundi tofar flatulsha tanul hata 3 kisha uza mbil tumia moja
 
Kwa makadilio hayo ya m50/zenu watumishi wa umma wasingejenga Mbona manake hata mkopo wa bank haufik
 
M10 tu inatosha gharama kubwa hapo bati na mbao Labda na fundi tofar flatulsha tanul hata 3 kisha uza mbil tumia moja
Kamanda asante kwa mchango wako mi si mwenye uzi ila nimekubali umepanua sana uwanja wa kufikiri
 
Back
Top Bottom