Makadirio ya gharama za matumizi yako kwa siku

Makadirio ya gharama za matumizi yako kwa siku

Yofav

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2021
Posts
4,236
Reaction score
7,583
Habari wakuu,

Life limekuwa tight mno wakati huu ila sidhani kama ni kwetu wote, ila kama unavyoona hapo kwenye kichwa cha huu uzi hebu tujuzane gharama za matumizi yetu ya kila siku.

Mfano mimi ni single boy ila Approximately ya matumizi yangu kwa siku huwa haizidi 8000Tsh, hapo nimekula asubuhi, mchana na usiku na pia Bundle la kutosha kuendesha mbanga. (Hapo kwenye kula nakula ninachokitaka, Yaani roho inachotaka sio ninachopata)

Matumizi yangu yanazidi kufika 8k maximum sanasana nikishinda nyumbani ila nikiingia harakati matumizi hupungua na kujikuta natumia 5000Tsh tu. Hii ni kutokana na kazi kuniweka busy kiasi cha kukosa nafasi ya kula asubuhi na mchana.

So nataka kujua na ninyi ndugu zangu Wenye familia na msio na familia vipi makadirio yenu yapo vipi kwenye matumizi ya siku... Nahitahi kujifunza na kujua kama kuna uwezekano wa kupunguza matumizi zaidi au kuongeza pindi nitakapobidi iwapo mfano nikijakuwa na familia inanibidi kuwa na uwezo wa kuacha balance ya shngap mezani.

Twenzetuni
 
Duh how mkuu, Though inawezekana maana kama una kila kitu ndani waweza kujikuta unanunua Dagaa tu... Mboga unayopika mchana unaila na usiku na ahsbh unaamkia na kiporo chake
 
Si una familia?
Sina familia hapo Mimi mwenyewe ila nasomesha, sijaingiza familia ndo maana nikakwambia ikiwa ni siku ya kazini najumlisha chai kule ofisi, chakula cha mchana na usafiri then na emergency naweza kutoka kazini hata saa 7 usiku sasa usafiri mpaka Uber au bolt maana hizi daladala zinasumbua.
 
But unahitaji kujifunza kuhusu nini kutokana na swali lako
Nataka kujua kama mtindo wangu wa budget upo sawa, Either natumia hela vibaya au nipo sawa.... Waweza kukuta mtu unatumia 20k na ungeweza kutumia 10k ukaishi fresh tu... So, ili kujua kwamba hilo linawezekana nitajua kupitia maoni ya wengine
 
Back
Top Bottom