Makala: Buriani Komredi Mawazo, Mpe Hongera Zangu Ken Saro-Wiwa

Makala: Buriani Komredi Mawazo, Mpe Hongera Zangu Ken Saro-Wiwa

Pole sana Ben na asante kwa makala inayoelezea safari ya kisiasa ya Mawazo.....tumejifunza mengi kutoka kwake....

Takriban miaka 23, CCM bado wameshindwa kukumbatia demokrasia ya mfumo wa vyama vingi kwa mikono miwili....Lakini haya maovu yote yanayofanyika dhidi ya wapinzani yana mwisho wake.....

Mawazo ameuawa kikatili... ili kuzuia vitendo vya kulipiza kisasi, Jeshi la polisi iwakamate wote waliohusika ili sheria ifuate mkondo wake, lakini pia ili kurejesha imani ya wananchi na jeshi hilo....Wananchi tunahitaji kuona haki inatendeka.....
 
Mtu aliye kwisha kufa haambiwi buriani ana ambiwa apumzike kwa amani.jifunze vzur kiswahili.
&
Lugha si maudhui ya habari hiyo isitoshe waungwana tumemuelewa,nakuona kama ni mmoja wa wale walio#%* Kazi nzuri Ben S!
 
the reformer,Asante.Si unajua kiswahili chetu ni cha hukohuko.Ila pia nadhani baada ya alama ya nukta sentensi inapaswa kuanza kwa herufi kubwa kama nilivyokoleza rangi nyekundu hapo juu.
Hukohuko wapi?buriani ana ambiwa mtu anaye enda vitani...asante kwa kunisahihisha kuhusu herufi kubwa.
 
Last edited by a moderator:
&
Lugha si maudhui ya habari hiyo isitoshe waungwana tumemuelewa,nakuona kama ni mmoja wa wale walio#%* Kazi nzuri Ben S!

Kumuelewa tu haitoshi.Yeye ni outstanding figure ndani ya Chadema.Anapaswa ku improve umakini wake...Na sisi ndio wa kumusaidia..Kuliko kumuacha tu inakua sio poa.
 
Chadema mkishamzika mawazo mtatumia nini kutafuta umaarufu wa kisiasa? Maana huu msiba kwenu ni sherehe ya kisiasa mnatamani akae mochwari ata mwaka ili nyie mpate kick.

Wewe una akili ya makaburu
 
R i p kamanda mawazo, unaoza wewe ili wengine wachipue, # ua a hero #
 
Umenikumbusha simulizi moja ya Ken Saro-wiwa, AFRICA KILLS HER SUN, humo ndani alitabiri kifo chake. Masikini alikuja uwawa kwasababu ya kupigania jamii yake. Hakika hawatasahaulika
 
Ben Saanane hongera sana hivi ndivyo anatakiwa kuenziwa Mawazo ni pigo kubwa sana!
 
Last edited by a moderator:
Mimi namfananisha Mawazo na Che Guevara wa afrika. Huyu anastahiki kutunukiwa nishani ya juu ya Makamanda Katika ukawa! Buriani Mawazo na ingawa kimwili umetutoka ila jina lako litazidi litanga'aa.

Huwezi kumfananisha che-guevara na marehemu alphonce mawazo... Karudie kusoma historia ya Che-Guevara...
 
Kweli ninyi Maccm hamchoki kumwaga damu za watu, mnamzurumu haki yake na bado mnamuuwa, huu ni ujambazi, yaani uccm ni ushetani, shetani ndio mwenyekazi ya kuua watu.

Na ilaaaniwe CCM, na misinge yake yote kwa kumwaga damu zisizo kuwa na hatia.

Walaaniwe wote waliohusika na mauwaji haya, maisha yao na yawe ya hofu na woga siku zote.

Ilaaniwe kila yeyote aliyehusika na mpango wa mauwaji haya hata kama alisikia na akanyamanza pia.

Walaaniwe pilisi wote, ambao wamepuzia jambo hili na kuzuia haki isitendeke.

CCM, CCM, utaacha lini kuuwa watu, ambao wapo katika haki zao.

Ni CCM ambayo ilimua Daudi Mwangosi kule Iringa, chini ya kamanda Michael Chamuwanda, ni CCM ndio iliuwa wale watu kwa mabomu kule Arusha wakati wa kufunga kampeni za udiwani chini ya uratibu wa Mwiguru Nchemba.

Ni CCM hii hii, iliwauwa watu 21 kwa risasi mwaka 2001, wakiwa katika maandamano ya amani.

Tunajua haya yote yana mwisho, Mungu yupo, ipo siku huu utawala wa kidhalimu unaouwa watu wake utafika mwisho.

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Afrika.

Waliomuua Mawazo ndio walimuua Chacha Wangwe. Acha kumwaga povu bwanamdogo hizi zingine ni zuga tu.
 
Ben Saanane kwanza nikusifu kuandika makala, hii ni hatua nzuri kwa vijana mnaotaka uongozi.

Maudhui ya makala yako ilikua kuomboleza na kukumbuka harakati za mpambanaji Mawazo, japo umeonekana unalaumu polisi au ccm ama ukidhania wao ndio wahusika wakuu wa tukio hilo (pia umewataka polisi kuhakikisha haki inapatikana.......sijui itapatikanaje ilhal unaowatuhumu ndio wachunguzi). Pia unasema wakishindwa nyinyi mtahakikisha haki inapatikana ( japo hujasema how).

Katika makala hii unaonesha ni mara ngapi umeshindwa kufikia malengo yako kupitia chama chako katika ngazi mbali mbali ili kuimarisha demokrasia chamani ( unasema ni sababu za kisiasa bila kueleza kwa undani) tukijumlisha na misuko suko uliyopata 2012.

Upande wa pili umeeleza sababu za kutoimarishwa kwa demokrasia ni uhafidhina walionao viongozi watawala, bila kugusia uhafidhina uliopo chamani mwako ( umesema kuna muda hufunganani na itikadi za vyama).

Sikukosoi ila makala hii ilikua ya kiujumla mno na umeongea mambo mengi huku ukichanganya hili na lile, na uliacha lengo mahususi la makala yako likiwa wazi.

Mtazamo tu
 
Last edited by a moderator:
Nimekusoma mkuu
Kweli wema hawana maisha,ila najiuliza sana na sipati jibu,kabla hujamchukia Mawazo kama mwanasiasa na mwanaharakati hawa waliofanya ushenzi huu walijiuliza ya kuwa Mawazo ni Baba wa familia,ni mume bora kabisa kwa mkewe,ni mjomba,kaka,binamu nk?uvivu huu wa kufikiri ndio uliopelekea unyama wote huu kufanyika,Ben endelea kuishi ndoto zako na unachokiamini,Rombo kuna siku litakuwa jimbo lako,inshallah nitaenda kukupa kura yangu.
 
Makala ni nzuri sana, Pumzika kwa amani kamanda Mawazo. Mungu aitunze familia yako
 
Ben....nimeisoma yote...Am speechless

RIP Mawazo
 
Huwezi kumfananisha che-guevara na marehemu alphonce mawazo... Karudie kusoma historia ya Che-Guevara...


Mawazo alikuwa ni mpigania mabadiliko wa kweli kweli ambayo ndio yaliyopelekea kukatishwa uhai wake na mafashisti wa CCM. Hio ni sawa na Che ni Mabepari na Mabeberu wa Kimagharibi ndio waliokatisha uhai wa El Che. Mkuu una uvivu wa kusoma basi hata wa Uhuru Mawazo unakushinda! Jiangalie utakufa utumwani!
 
Back
Top Bottom