Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,992
Kwanza poleni sana kwa msiba huo mzito, ijapokuwa pole ni pia kwa watanzania wote hasa wale wapenda mabadiliko na wanaoitakia mema nchi hii. Nakupa hongera sana kwa sababu unaweka pamoja na kujumuisha vitu vingi adimu. nia ya kweli ya kuleta mapinduzi, ari ya kusoma na kujiendeleza, kusimama kwenye ukweli, kutumia kichwa na ubongo kutafakari, kufikiri hatua chache mbele zaidi, kuwa tayari kufanyia kazi ndoto zako, kuwa na msimamo usioyumba wala kuyumbishwa, kutokuwa mchumia tumbo - hayo ni baadhi ya mambo adimu kuyakuta yamewekwa pamoja katika mwanasiasa wa Tanzania. kwa kweli namuomba Mungu akujalie udumu hivyo hivyo, usiwe kama wengine wengi ambao jamii iliwaamini, wakaja kuzidiwa na ulevi wa madaraka, au kuingia mkenge kwa kushauriwa vibaya na wasakatonge, na hivyo kuhujumu matumaini ya watanzania. Hongera sana.