MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

Inaendelea....
MAKALA: SEHEMU YA TATU

Katika makala yetu ya sehemu ya pili tumeangalia mambo mbalimbali kama awamu za malipo ya kodi, viwango vya kodi kwa walipa wa aina tatu tofauti, ukokotoaji kwa walipa kodi kwa wanaoweka kumbukumbu lakini mauzo yao ni chini ya milioni 20 kwa mwaka na mengineyo mengi mazuri ya kutupa elimu zaidi.
Katika makala yetu hii sehemu ya tatu tuangalie masuala yafuatayo:

1. JE UTAFANYAJE KAMA UMEJIKADIRIA/UMEKADIRIWA MAKADIRIO MAKUBWA AU KIDOGO?
Unapoanza au unapoendelea kufanya biashara huwa na matumaini chanya ya biashara kuwa nzuri kwa mwaka husika. Hivyo hata makadirio unayokuwa umekadiriwa unakuwa na uhakika wa kuyalipa kwa awamu zote nne bila tatizo. Lakini kuna nyakati biashara inaweza kustawi sana au kusinyaa sana hadi inafikia hata gharama mbalimbali za kujiendesha biashara yenyewe kushindwa kulipwa au biashara imenawiri. Je utafanya nini kama
a) Umejikadiria kodi kidogo?
Iwapo utagundua kabla ya mwaka wa mapato kuisha, kuwa makadirio yako ya kodi ya awali ni pungufu ukilinganisha na hali halisi unaruhusiwa kisheria kufanya marekebisho yanayostahili ili kuepuka tatizo la kutozwa riba baadaye. riba hutokwa kutokana na viwango vilivyowekwa na Beki Kuu
b) Umejikadiria kodi kubwa?
Ikiwa ukadiriaji wa kodi unayostahili kulipwa ni kubwa kuliko uwezo wako, utaandika barua kwa kamishna wa kodi kutaarifu suala hili na sababu za msingi na kujaza fomu rejea ya makadirio ya kodi kwa kiwango ambacho unaona utaweza kulipa.
c) Malalamiko juu ya makadirio ya kodi
Mojawapo za haki ya Mlipakodi zilizoainishwa katika Mkataba wa Mlipa kodi (Taxpayer's Charter) ni kupinga makadirio ya kodi iwapo anaamini sio sahihi. Fuata taratibu hizi kupinga makadirio ya Kodi (Rejea Sheria ya Usimamizi wa Kodi mwaka 2015):
1. Andika barua kwa kamishna ikielezea sababu za msingi zenye kuonyesha makosa yaliyofanywa ktk ukadiriaji
2. Barua ya kuoina makadirio ni lazima iwasilishwe ndani ya siku 30 toka tarehe ya makadirio ya kodi husika
3. Ili pingamizi la kodi likubalike mlipa kodi anatakiwa alipe 1/3 ya kodi yote kubwa uliyokadiriwa ndani ya siku 30 toka tarehe ya makadirio
Kamishna wa kodi atakutaarifu kupokea malalmiko yako na iwapo baada ya hukumu kutoka kama hujaridhika basi waweza kukata rufaa kwenye Baraza la Rufaa za Kodi au Mahakama Kuu ya Rufaa za Kodi kwa maamuzi ya mwisho

2. SHERIA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT 2014)

VAT ni kodi ya Mlaji inayotozwa na mfanyabiashara aliyesajiliwa kwa miujibu wa sheria kwenye mauzo ya bidhaa au huduma zinazostahili kutozwa VAT. Bidhaa zinazotozwa ni zile zinazozalishwa hapa nchini Tanzania Bara na kutoka nje ya Tanzania
a) Ngazi za utozwaji VAT
Utozwaji hufanywa ktk ngazi ya uzalishaji, uingizaji bidhaa au huduma kutoka nje, uuzaji wa jumla na reja reja mpaka bidhaa inapomfikia mlaji wa mwisho. Mlipaji wa VAT ni mlaji wa mwisho
b) Usajili wa VAT
Sifa hizi zinahusika
1. Awe mfanyabiashara alie na TIN
2. Mauzo yake yawe kuanzia au anatarajia mauzo kuwa zaidi ya mil 100 kwa mwaka
3. Biashara za huduma za kitaaluma kama vile wanasheria, wahandisi, na wahasibu walazaimika kusajili VAT pasipo kuangalia kiwango maalumu cha mauzo kwa mwaka
c) Ulipaji VAT
Ulipaji VAT hufanyika ndani ya siku 20 baada ya mwezi wa malipo husika ie kila tarehe 20 ya mwezi utajaza ritani na kuwasilisha kwa njia ya mtandao
d) Bidhaa zilizosamehewa VAT
kuna bidhaa na huduma zimesamehewa VAT kutokana na sababu mbalimbali za kijamii na kiuchimi zenye tija kwa Taifa.Bidhaa hizo ni kama vile vyakula ambavyo havijasindikwa mfano: mahindi, unga wa mahindi, ngani na unga wake, matunda yasiyosindikwa nk
Bidhaa nyinginezo ni pamoja na madawa ya binadamu yaliyotajwa na Wizara ya Afya, huduma za tiba kama meno na magonjwa mbalimbali, pia magazeti, majarida nk
Vilevi;e usafirishaji wa abiria kwa basi, ndege, treni isipokuwa usafiri wa Taxi, gari za kukodi, boti na ndege za kukodi, huduma za elimu, uuzaji au upangishaji nyumba za kuishi au ardhi nk

3.SHERIA YA USHURU WA STEMPU
Hutumika kuhalalisha miamala ikiwemo hati za kisheria au mikataba mbalimbali. Gharama yake ni 1% ya thamani ya mauzo au sihia kwa maswala ya hati ya kisheria na mikataba hutegemea na viwango maalum vilivyoainishwa kti sheria ya mwaka 1972 na kurejewa mwaka 2006
Muda wa kulipa ushuru wa stempu ni ndani ya siku 30 baada ya kusaini hati au mkataba.

4. KODI YA ZUIO
Utangulizi:

Kodi ya zuio ni kiasi cha kodi kinachozuiwa na mtu anapomlipa mtu mwingine kutokana na bidhaa zilizosambazwa au huduma iliyotolewa na mlipwaji. Mtu anayepokea au anayestahili kupokea malipo ambayo kwayo kodi ya mapato inatakiwa kuzuiwa ni mkatwaji wa kodi ilhali mtu anayepaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika malipo yaliyofanyika kwa mkatwaji anajulikana kama Wakala wa kodi ya zuio.

Malipo yanayostahili kukatwa kodi ya zuio
Kodi ya zuio inatozwa katika malipo husika ikiwa ni pamoja na malipo yanayopaswa kujumuishwa katika kukokotoa mapato ya mwajiriwa yanayostahili kukatwa kutoka kwa mwajiriwa katika ajira, malipo ya mapato ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na magawio, riba, malipo ya maliasili, pango au mrabaha, malipo ya huduma na malipo ya mikataba na malipo ya bidhaa zilizosambazwa serikalini na kwenye taasisi zake.

Taarifa na Muda wa Kulipa Kodi Iliyozuiwa
  • Kila wakala wa kodi ya zuio atalipa kwa Kamishna kodi ya zuio aliyozuia ndani ya siku 7 baada ya kila mwisho wa mwezi wa kalenda.
  • Kila wakala wa kodi ya zuio atapeleka kwa Kamishna ndani ya siku 30 baada ya kipindi cha kila miezi sita ya kalenda taarifa katika fomu maalum iliyoandaliwa inayobainisha malipo yaliyofanywa na wakala katika kipindi husika cha zuio la kodi, jina na anwani ya mzuiwa, kodi ya mapato iliyozuiwa kutoka katika kila malipo yaliyozuiwa; na taarifa nyingine yoyote ambayo Kamishna ataelekeza.
Hati ya Kodi ya Zuio
Wakala wa kodi ya zuio ataandaa na kumtunuku mzuiwa hati ya kodi ya zuio ikionesha kiasi cha malipo alicholipwa mzuiwa na kodi ya mapato iliyozuiwa kutoka katika malipo hayo. Hati ya zuio itahusisha mwezi wa kalenda na itatolewa ndani ya siku 30 baada ya mwisho wa mwezi. Hata hivyo, kwa upande wa kodi inayozuiwa kutoka katika kodi ya ajira hati itahusisha sehemu ya mwaka wa kalenda katika kipindi ambacho mwajiriwa atakuwa amejiriwa na atahudumiwa ifikapo tarehe 30 ya Januari baada ya mwisho wa mwaka au, pale ambapo ajira yake imesitishwa na wakala wa zuio katika mwaka si zaidi ya siku 30 kutoka tarehe ambayo ajira ilisitishwa.

Aina za Kodi za Zuio
Sheria imegawanya kodi ya zuio katika aina kuu mbili, ambazo ni:-
  • Kodi za Zuio za mwisho
  • Kodi za Zuio zisizo za Mwisho
Kodi za Zuio za Mwisho ni kodi ambazo mzuiwa hawezi kudai punguzo lolote la kodi wakati wa kukokotoa kodi ya mapato inayolipwa kwa mwaka wa mapato.
Kodi za Zuio zisizo za Mwisho: ni kodi ambazo mzuiwa anastahili punguzo la kodi kiasi sawa na kodi inayochukuliwa kuwa imelipwa kwa mwaka wa mapato ambamo kiasi hicho kimekokotolewa.

MWISHO
 
Asante sana mkuu kwa kuendelea kutoa elimu hii muhimu sana, lakini pia naomba kuuliza swali.
Vipi kuhusu biashara au huduma za mitandao kama ilivyo Jamiiforums, zoomtanzania, kupatana pamoja na blogs, hawa wanakua katika kundi gani na makadilio yao ya kodi yanakuaje? Maana nadhani wakati ndio wanaanza biashara au kutoa huduma hizo hakuna mapato zaidi ya gharama nyingi za uendeshaji.
ASANTE
 
Asante Mkuu
Tukirejea katika swali lako la msingi:-
Mosi, biashara zote zinapoanza huanza kwa uwekezaji wa mtaji hivyo kuingia gharama mbalimbali. Hivyo basi hasara kwa biashara nyingi kwa 'start up business' haikwepeki kwani ni lazima uwekeze na itakumbuka mauzo huyo yanakuwa chini na mzunguko wa biashara unakuwa sio mzuri sana mwishowe huishia kupata hasara au faida ndogo
Pili, kwa biashara za mitandao nao wanalazimika kwenda TRA kujaza fomu za makadirio ya kodi ya mwaka ambao iwapo kama makadirio yapo juu basi atafuata taratibu zilizoelezwa hapo juu ktk makala.
Kutokana na uzoefu wetu kwa kampuni za kimitandao tulizozisajili, ukiachana na gharama nyinginezo km za TCRA, Leseni ya biashara nk lazima walipe kodi pia. Na mwisho wa mwaka hufanyiwa hesabu za mizania.
Changamoto ilikuwa ktk kutoa risiti za EFD, tuliwapa mwongozo wa kuhakikisha wanatoa risiti pia kwn mteja anapokuja au unapomhudumia online ana physical address, print risiti yake kisha mtumie. Weka na gharama ya kuituma risiti yake kwenye bei yk, ktk invoice aiainishe kuwa gharama hii ni kwa hili na lile
 
Shukran
 
Nyongeza ya jibu nililojibu awali
IMG_20181217_173532.jpeg
 
Duh,
Kwahiyo Mimi mtumiaji wa JAMIIFORUMS risiti ntakua nazo ngapi kwa siku.

Vitu vingine huwa naona Tra wanacomplicate sana
 
Kwani hii huduma ya kuingia kusoma na kuchangia unauziwa?
JF hapa ina maana risiti zitawahusu wale wanaotaka kupata huduma za kulipia mfano kuweka matangazo yao kupitia JF hapa unailipia huduma hii hivyo JF inabidi wakupe risiti yk kwn umefanya malipo the same kama unavyoona ktk luninga au radio, ukipeleka tangazo utalipa na risiti utapewa
 
Asante kwa elimu mkuu, sasa mimi nimefungua ka biashara kadogo ka mtaji wa kama 1.5 m na ninapanga pango ila sijalipia chochote tra wala serikali za mitaa, unanishaurije na je ni kitu kinaweza kunipata kwa jinsi ninavyoendesha haka ka biashara?
 
Hongera kwa kuwa na biashara
1. Kama walipia pango
Hii ina maana biashara yako ipo ktk flemu na waiendesha rasmi. Hivyo basi kwa upande wa TRA utakuwa na haya ya kutekeleza
A: kulipia kodi ya zuio (withholding tax) ya 10% kutokana na mkataba wa pango ulioingia. Angalizo: Hii 10% ya WHT utalipa ikiwa utawasilisha mkataba ndani ya muda wa siku 30 toka kusainiwa kwake. Ikiwa baada ya hapo kuna faini pia utalipa. Ina maana itazidi zaidi ya hy 10%

B: Utalipa 1% ya ushuru wa stempu kwa mwaka kutokana na thamani ya mkataba wako wa pango uliolipia.

C: Hujaainisha mauzo au matarajio yako ya mauzo kwa mwaka itakuwa kiasi gani kwn kwa biashara ndogo kodi hulipwa kutokana na mauzo na si mapato. Waweza kurejea ktk makala jinsi ya ukokotoaji wa kodi. Iwapo mauzo yako yatakuwa chini ya mil 4 kwa mwaka wewe hustahili kulipa kodi bali utapewa TIN ya biashara na utajaziwa fomu za makadirio 0 (sifuri) kwani mauzo chini ya mil 4 hakuna kodi. Iwapo mauzo ni zaidi ya hapo utatakiwa kulipa na kodi.

D: Utaomba cheti cha mlipa kodi msafi "Certificate of Tax Clearance" baada ya kulipa kodi ya zuio na ushuru wa stempu kwn kitakufaa ktk mambo kama kuomba leseni nk

Naogopa hili
Lugha ya biashara ni changamoto kubwa kwa wafanyabiashara hivyo kujikuta anapewa makadirio makubwa kutokana na kushindwa kuelewa anaulizwa nini na yeye anajibu nini!
One day nikijaaliwa nitaleta makala hii
 
Asante sana mkuu kwa maelezo yako mazuri
 
Mkuu, binafs nmeipenda hii makala, JE makadirio ya mtu anayelenga kuanza biashara ambayo mtaji wake ni chini ya 1milion. Makadirio yake yatafanyika vipi ikiwa biashara ajaanza kufanya. Ndio kwanza, yuko katika hatua za awali za biashara. Ndo anaanza taratbu za kupata TIN.

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
 
Hapo kwenye kulipa kodi kabla sijaanza biashara,ndio panapoumiza sana kwa nini waniambie nilipe kiasi flani wakati sijajua kama ntauza au sitauza?
 
Mkuu, binafs nmeipenda hii makala, JE makadirio ya mtu anayelenga kuanza biashara ambayo mtaji wake ni chini ya 1milion. Makadirio yake yatafanyika vipi ikiwa biashara ajaanza kufanya. Ndio kwanza, yuko katika hatua za awali za biashara. Ndo anaanza taratbu za kupata TIN.

Sent from my SM-G900F using JamiiForums mobile app
Mkuu Mr coffee
1. Ieleweke wazi kuwa malipo ya kodi hayana uhusiano na mtaji wako bali mauzo (kwa biashara ndogo) au faida yako (biashara kubwa)

2. Changamoto kubwa iliyopo ni "lugha ya biashara" kwa tuliowengi hatuwezi au hatuielewi vema. Ipo wazi kabisa kuwa mauzo chini ya mil 4 kwa mwaka hutakiwi kulipa kodi. Tatizo linakuja ktk mahojiano na yule anaekukadiria kodi kwn maswali anayokuuliza juu ya mauzo na ww maelezo unayotoa juu ya biashara yako akifanya hesabu zinazidi zaidi ya mil 4 kimauzo UTAKAPOKUJA ANZA KUFANYA BIASHARA. Hivyo unalipa kama malipo ya awali 'advance payment' ambayo una haki ya kutoa maelezo au kuirekebisha baadae kama mambo hayapo sawa
 
Back
Top Bottom