asante kwa somo zuri, naomba ufafanuz jinsi ya kupata TIN TRA kwa kundi la kampuni, taasisi . na hiyo kodi inayokatwa kwa kampuni kutokana na faida inakatwa kwenye gross profit au net profit
Asante Mkuu
Laki Si Pesa
Tukirejea katika swali lako la kuhutaji mwongozo wa kupata TIN kwa upande wa kampuni, taasisi nk. Hili limegawanyika kutokana na 'legal entity' ya taasisi/kampuni husika.
A: Kampuni yenye ukomo wa shea ie limited company
Kupata TIN ya kampuni yenye ukomo utaanda vielelezo vifuatavyo:
1. MEMARTS ithibitishe kwa mwanasheria/mahakamani
2. Cheti cha Usajili ie Certificate of Incorporation vema ukithibitisha kwa mwanasheria/mahakama japo kwa sasa mfumo wa usajili wa BRELA na TRA kwa kampuni umeunganishwa hivyo namba ya usajili ya Cheti ndiyo itakuwa namba ya TIN ya kampuni na maelezo yanatumwa TRA pia ukisajili
3. TIN za wanahisa/wamiliki wote wa kampuni
4. Mkataba wa kisheria wa pango
5. Uwepo japo Mkurugenzi mmojawapo wa kampuni hii ni lazima
6. Barua ya utambulisho toka kwa Afisa Mtendaji(barua hii hutolewa na TRA)
7. Fomu za maombi ya kufungua TIN ya kampuni (hutolewa TRA)
8. Fomu za kujaza kwa ajili ya TIN ya kila mwanahisa (hutolewa TRA)
9. Fomu ya makadirio ya kodi kwa ajili ya kampuni (hutolewa TRA)
10. Kama una mshauri wa kodi/mkaguzi wa mahesabu/?mwanasheria(jambo jema hili) andika barua ya kum-'appoint' kwn kadhia zozote watahusika wao kwa niaba ya kampuni yako. Vlvl ndani ya fomu za maombi ya TIN kuna jedwali huonyesha kama unao ujaze maelezo yao kama jina, TIN. Barua hii lazima uliomu'appoint' asaini na mhuri agonge kuonyesha amekubali
11. Passport size ya kila mwanahisa
12. Mnaweza mkaweka na 'Resolution letter' (tafsiri isiyo rasmi barua kuu ya maelezo ya kampuni na kuridhia kwa bodi ya kampuni kufungua TIN. Pia barua hii inasaidia kuweka wazi mnaanza au mnafanya biashara gani kwn MEMARTS huwa na idafi kubwa ya biashara ambazi kampuni inazifanya na inatarajia kuzifanya hapo baadaye)
B: TIN ya ushirikiano "Partnership TIN"
Mahitaji yanafanana na ya mwanzo kwa baadhi ya mambo. Mahitaji yake ni
1. TIN ya kila mshiriki
2. Mkataba wa ushirikiano ie Partnership Deed
3. Mkataba wa kisheria wa pango
4. Fomu za maombi ya TIN kwa ushirikiano
5. Passport size 2 kwa kila mshiriki
6. Fomu ya makadirio ya kodi kwa ushirikiano
7. Na mengine km barua ya appointment ya tax/auditor/lawyer etc
N. K (hii mada ndefu kuweka kila taasisi na mahitaji yake). Naomba uridhike na hizi chache kwanza au uende moja kwa moja kwa taasisi unayotaka.
Tukirejea katika swali la pili juu ya kodi za kampuni:
Ikumbukwe taasisi na makampuni hutakiwa kulipa kodi kubwa 'corporate tax' ya 30% kutoka katika faida ghafi ie Operating Profit.
Faida hii hupatikana baada ya kuandaa mahesabu ya mizania kwa muda ulioona wafaa kwa wakati huo inaweza ikawa ndani ya miezi 6,12,14 lkn si miezi 24 kwa wakati mmoja etc etc kwani statement itaweka wazi hayo mahesabu ni ya muda gani. Hivyo bhasi baada ya kukokotoa mahesabu yako ya faida utatoa 30% ya kodi. Na kama umepata hasara bhasi hutalipa. Suala la namna gani uta'compansate' kodi ya makadirio uliyolipia itaoneshwa ndani ya mahesabu ya mizania