MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

MAKALA: Mambo muhimu ya kuzingatia kuhusu kodi kwa mtu anayeanza biashara

MAKALA: SEHEMU YA KWANZA
Habari zenu wanajukwaa
1. Utangulizi
makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.
2. Biashara na aina zake
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe.
kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:
1. Biashara ndogo sana
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Sh 1 hadi 5mil

2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia mil5 hadi mil 200

3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya mil 200 hadi mil 800

4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya mil 800.

Vingezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka

3. SHERIA ZA KODI
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara:
1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015
Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani

A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)

B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`

Inaendelea.......
B: Taratibu za kufuatwa na mtu anaeanza biashara kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) pamoja na malipo ya kodi na mengineyo:

Mtu anaeanza biashara atatakiwa kuomba TIN kutoka TRA ambapo vielelezo hv vitahitajika
1. Fomu za maombi ya TIN kwa mtu binafsi (zinatolewa TRA)
2. Barua ya utambulisho wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (hutolewa na TRA)
3. Mkataba wa pango kwa aliepanga eneo la biashara au kielelzo cha umiliki wa eneo la biashara kama hati, ofa au karatasi za malipo ya kodi ya majengo
4. Kopi ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya udreva, paspoti ya kusafiria au kitambulisho cha kupigia kura
5. Picha ndogo ya paspoti saizi

Mhusika utaulizwa juu ya biashara yako "business assessment". baada ya hapo utaambiwa kiasi cha kodi utakayostahili kulipa kutokana na mauzo ya biashara unayofanya au unayotarajia kuifanya. baada ya maelezo haya taratibu nyingine zitaendele na hatimaye utapata TIN.
Kwa leo naomba tuishie hapa sehemu ya kwanza kutokana na majukumu. Tutaendelea sehemu ya pili
Asante

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shukrani sana kwa somo nimependa sana kuelimishwa juu ya kodi maana watu hukwepa kulipa kodi kumbe wakati mwingine ni kukosa elimu juu ya ulipaji kodi.
 
Nakushauri usome makala imeelezea vema sana suala la EFD usione uvivu
Ila kwa kifupi tu ni kuwa biashara yyt inayofikisha mauzo ZAIDI YA MIL 14 KWA MWAKA unatakiwa kutoa risiti za kielektroniki ie EFD receipts. Hivyo biashara yenye mauzo chini ya mil 14 hustahili kutoa risiti za kielektroniki bali UTOE RISITI YA KUANDIKWA KWA MKONO ambayo itaonesha TIN yako, Jina lako na bidhaa na bei pia
Mkuu apo umeeleweka vema isipokuwa changamoto zipo njiani ukibeba mzigo wanataka efd receipt ata ukiwaambia mauzo ni chini ya 14 milion hawaelew
 
Mkuu apo umeeleweka vema isipokuwa changamoto zipo njiani ukibeba mzigo wanataka efd receipt ata ukiwaambia mauzo ni chini ya 14 milion hawaelew
Jambo unalotakiwa kufanya ni kuwapeleka kwenye duka ulilonunua mzigo. Na wao wakifika kwa mhusika alietoa risiti ambaye kwa mwaka anauza chini ya mil 14 wataona hali halisi na vlvl watafanya crosschecks zao kujiridhisha.
Lakini tambua mauzo ya mil 14 kwa mwaka ni kama 39,000 kwa siku (360 siku). Ss kwa duka lililopo mjini kidg hii inaleta ukakasi tuwe wakweli jamani. Kuna biashara ambazo hazina mauzo ya kila siku hili lawezekana lkn kwa biashara za mauzo ya kila siku mmh
 
Maswali yangu ni kama ifuatavyo....
1. Unaweza pata TIN ya biashara na makadirio yake kwa biashara ambayo unahitaji kufungua miezi sita ijayo? Nikimaanisha kodi ianze kuhesabiwa baada ya kuanza biashara ingawa TIN imeombwa miezi 6 nyuma?
2. Ili kupata leseni ya biashara halmashauri mfano biashara ya bucha unahitaji viambatanisho gani?
 
Naam Mkuu Trayvess Daniel
Nashukuru kwa maswali yako mazuri. Majibu ni hivi
1. Kulipa kodi wakati huu ili itumike wakati ujao
Unapoomba TIN ya biashara ina maana ya kwanza na inatafsirika umeshaanza biashara hata kama bado hujaianza biashara hiyo kivitendo. Hivyo basi kike kitendo cha wewe kupata TIN ya biashara inahalalisha wewe kulipa kodi kwa wakati husika na haitaweza kutumika tena kwa wakati ujao.
Unachoweza kufanya ni Kuomba TIN lakini isiwe kwa ajili ya biashara bali kwa mambo mengine kwa mfano kuombea leseni ya udereva nk ambapo utakuwa na TIN hy. Ukiona umeanza biashara utaenda kuibadilisha matumizi na kuwa TIN ya biashara ambapo utakadiriwa na kulipa makadirio husika kwa wakati huo ulioanza biashara.

2. Vielelezo vya kupata leseni kwa biashara ya bucha
Kwa biashara hii utatakiwa kuambatanisha vielelezo hivi
1. TIN 2. mkataba wa pango 3. Cheti cha uthibitisho wa kulipa kodi 4. Kujaza fomu ya manispaa ya maombi ya leseni 5. Cheti cha afya na uthibiti cha TFDA 5. Kopi ya kitambulisho chako
 
Kwanza naomba nikupongeze kwa somo zuri unalolitoa kuhusu Kodi na taratibu zake

Kiongozi mimi nina swali japo ntaanza kwa maelezo kidogo

Mwezi wa tisa mwaka 2015 nilifanya mchakato wa kuomba TIN kwa ajili ya biashara yangu ya Library na kuitumia TIN hiyo kupata Leseni ya biashara na kupata line kihalali za Tigo Pesa na M-Pesa maana ndio biashara niliyotaka kufungua.

Japo wakati wa makadirio nilibishana nao pale waliponikadiria kodi kubwa maana mwenyewe najua kabisa biashara yangu ya Library haina uwezo wa kuingiza milioni 4 na zaidi kwa mwaka.
Walikataa kubadilisha makadirio yao ya kodi ya 150,000 kwa mwaka waliyonikadiria nikakubali kishingo upande na baada ya muda nikapewa TIN yangu
Ila kiukweli kabisa mpaka sasa ninavyoandika sijawahi kulipa kodi yao waliyonikadiria maana biashara haizalishi kiasi cha kuweza kulipa kodi.
Kati ya 2016 mpaka 2017 mwishoni nilibanwa sana na majukumu ya chuo na maisha japo biashara yangu ya Library ilikuwa inaendelea kama kawaida
Mwaka jana mwezi wa pili ndio nilienda manispaa kuomba Leseni ya biashara na nikapewa na nikaanza kufatilia line za Tigopesa na M-Pesa

So maswali yangu ni kama ifuatavyo:
1. Je naweza kwenda TRA na kuomba wanikadirie upya??
2. Huku uswahilini serikali za mitaa zinatushinikiza tuchukue kitambulisho cha mjasiriamali na mimi nimechukua je naweza kwenda TRA na kuomba kuisitisha matumizi ya TIN namba yangu?
Ntashukuru nikipata msaada wa kielimu hapo.

Pole sana Mkuu Ramzy Classic kwa changamoto. Anyway maisha lazima yaendelee.
Majibu yako ni
1. Kwa mwaka 2015, TIN na makadirio
Kwa wakati huo baada ya "kulazimishwa" kulipa kiasi ambacho si stahiki kutokana na biashara yako ambayo wewe binafsi umesema mauzo hayakuwa yanazidi mil 4 kwa mwaka, ungeandika barua kwa meneja wa hilo tawi ulilopata huduma juu ya kupinga makadirio hayo.

LAKINI ANGALIZO HILI LIZINGATIWE
Suala la kuandika barua ya kupinga litakuwa sawa kama na kama tu wakati wa mahojiano ulisema kiwango ambacho Afisa wa kodi akifanya hesabu za mauzo kwa mwaka kinakuwa chini ya mil 4. Hivyo basi kama mauzo ulisema mwenyewe yanakuja zaidi ya mil 4 hiyo ni kosa lako mwenyewe, ulitakiwa ulipe

2. Malipo ya kodi toka 2015......2019
Kama hujaenda kutoa taarifa zozote TRA tambua penati itabaki pale pale kwa muda wote huo ambapo ni sh 225,000 kwa kila mwezi unaoongezeka toka mwezi wa malipo ya kodi. Hivyo tarajia ukienda kukutana na faini hii. Sio nakuogopesha usiende laaah bali tatizo hutatuliwa kwa kukabiliana nalo. Nakushauri nenda kaangalie hali halisi naamini utasikilizwa na kusaidiwa kutatua changamoto hii.

3. Kukadiriwa upya mwaka huu 2019
Ndiyo utakadiriwa upya lkn viporo vya madeni yako vipo pia. Kila mwaka makadirio mapya hufanyika.

4. Kitambulisho vya mjasiriamali
Kama biashara yako ni ndogo sana bhasi ni vema ununue hicho kitambulisho na pia uende TRA kutoa taarifa juu ya mabadiliko ya hali ya kibiashara kuwa biashara yako imekuwa ndogo sana. Nenda na kitambulisho hicho kama ushahidi wa biashara yako ni ndogo sana na hapo elezea na hali halisi ya wakati huo wa makadirio makubwa ambayo hayaendani na biashara yako
 
Shukran Kiongozi kwa maelezo yaliyojitosheleza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shule tosha mkuu barikiwa
MAKALA: SEHEMU YA KWANZA
Habari zenu wanajukwaa
1. Utangulizi
makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.
2. Biashara na aina zake
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe.
kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:
1. Biashara ndogo sana
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Sh 1 hadi 5mil

2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia mil5 hadi mil 200

3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya mil 200 hadi mil 800

4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya mil 800.

Vingezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka

3. SHERIA ZA KODI
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara:
1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015
Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani

A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)

B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`

Inaendelea.......
B: Taratibu za kufuatwa na mtu anaeanza biashara kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) pamoja na malipo ya kodi na mengineyo:

Mtu anaeanza biashara atatakiwa kuomba TIN kutoka TRA ambapo vielelezo hv vitahitajika
1. Fomu za maombi ya TIN kwa mtu binafsi (zinatolewa TRA)
2. Barua ya utambulisho wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (hutolewa na TRA)
3. Mkataba wa pango kwa aliepanga eneo la biashara au kielelzo cha umiliki wa eneo la biashara kama hati, ofa au karatasi za malipo ya kodi ya majengo
4. Kopi ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya udreva, paspoti ya kusafiria au kitambulisho cha kupigia kura
5. Picha ndogo ya paspoti saizi

Mhusika utaulizwa juu ya biashara yako "business assessment". baada ya hapo utaambiwa kiasi cha kodi utakayostahili kulipa kutokana na mauzo ya biashara unayofanya au unayotarajia kuifanya. baada ya maelezo haya taratibu nyingine zitaendele na hatimaye utapata TIN.
Kwa leo naomba tuishie hapa sehemu ya kwanza kutokana na majukumu. Tutaendelea sehemu ya pili
 
Inaendelea....
MAKALA: SEHEMU YA TATU

Katika makala yetu ya sehemu ya pili tumeangalia mambo mbalimbali kama awamu za malipo ya kodi, viwango vya kodi kwa walipa wa aina tatu tofauti, ukokotoaji kwa walipa kodi kwa wanaoweka kumbukumbu lakini mauzo yao ni chini ya milioni 20 kwa mwaka na mengineyo mengi mazuri ya kutupa elimu zaidi.
Katika makala yetu hii sehemu ya tatu tuangalie masuala yafuatayo:

1. JE UTAFANYAJE KAMA UMEJIKADIRIA/UMEKADIRIWA MAKADIRIO MAKUBWA AU KIDOGO?
Unapoanza au unapoendelea kufanya biashara huwa na matumaini chanya ya biashara kuwa nzuri kwa mwaka husika. Hivyo hata makadirio unayokuwa umekadiriwa unakuwa na uhakika wa kuyalipa kwa awamu zote nne bila tatizo. Lakini kuna nyakati biashara inaweza kustawi sana au kusinyaa sana hadi inafikia hata gharama mbalimbali za kujiendesha biashara yenyewe kushindwa kulipwa au biashara imenawiri. Je utafanya nini kama
a) Umejikadiria kodi kidogo?
Iwapo utagundua kabla ya mwaka wa mapato kuisha, kuwa makadirio yako ya kodi ya awali ni pungufu ukilinganisha na hali halisi unaruhusiwa kisheria kufanya marekebisho yanayostahili ili kuepuka tatizo la kutozwa riba baadaye. riba hutokwa kutokana na viwango vilivyowekwa na Beki Kuu
b) Umejikadiria kodi kubwa?
Ikiwa ukadiriaji wa kodi unayostahili kulipwa ni kubwa kuliko uwezo wako, utaandika barua kwa kamishna wa kodi kutaarifu suala hili na sababu za msingi na kujaza fomu rejea ya makadirio ya kodi kwa kiwango ambacho unaona utaweza kulipa.
c) Malalamiko juu ya makadirio ya kodi
Mojawapo za haki ya Mlipakodi zilizoainishwa katika Mkataba wa Mlipa kodi (Taxpayer's Charter) ni kupinga makadirio ya kodi iwapo anaamini sio sahihi. Fuata taratibu hizi kupinga makadirio ya Kodi (Rejea Sheria ya Usimamizi wa Kodi mwaka 2015):
1. Andika barua kwa kamishna ikielezea sababu za msingi zenye kuonyesha makosa yaliyofanywa ktk ukadiriaji
2. Barua ya kuoina makadirio ni lazima iwasilishwe ndani ya siku 30 toka tarehe ya makadirio ya kodi husika
3. Ili pingamizi la kodi likubalike mlipa kodi anatakiwa alipe 1/3 ya kodi yote kubwa uliyokadiriwa ndani ya siku 30 toka tarehe ya makadirio
Kamishna wa kodi atakutaarifu kupokea malalmiko yako na iwapo baada ya hukumu kutoka kama hujaridhika basi waweza kukata rufaa kwenye Baraza la Rufaa za Kodi au Mahakama Kuu ya Rufaa za Kodi kwa maamuzi ya mwisho

2. SHERIA YA KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT 2014)

VAT ni kodi ya Mlaji inayotozwa na mfanyabiashara aliyesajiliwa kwa miujibu wa sheria kwenye mauzo ya bidhaa au huduma zinazostahili kutozwa VAT. Bidhaa zinazotozwa ni zile zinazozalishwa hapa nchini Tanzania Bara na kutoka nje ya Tanzania
a) Ngazi za utozwaji VAT
Utozwaji hufanywa ktk ngazi ya uzalishaji, uingizaji bidhaa au huduma kutoka nje, uuzaji wa jumla na reja reja mpaka bidhaa inapomfikia mlaji wa mwisho. Mlipaji wa VAT ni mlaji wa mwisho
b) Usajili wa VAT
Sifa hizi zinahusika
1. Awe mfanyabiashara alie na TIN
2. Mauzo yake yawe kuanzia au anatarajia mauzo kuwa zaidi ya mil 100 kwa mwaka
3. Biashara za huduma za kitaaluma kama vile wanasheria, wahandisi, na wahasibu walazaimika kusajili VAT pasipo kuangalia kiwango maalumu cha mauzo kwa mwaka
c) Ulipaji VAT
Ulipaji VAT hufanyika ndani ya siku 20 baada ya mwezi wa malipo husika ie kila tarehe 20 ya mwezi utajaza ritani na kuwasilisha kwa njia ya mtandao
d) Bidhaa zilizosamehewa VAT
kuna bidhaa na huduma zimesamehewa VAT kutokana na sababu mbalimbali za kijamii na kiuchimi zenye tija kwa Taifa.Bidhaa hizo ni kama vile vyakula ambavyo havijasindikwa mfano: mahindi, unga wa mahindi, ngani na unga wake, matunda yasiyosindikwa nk
Bidhaa nyinginezo ni pamoja na madawa ya binadamu yaliyotajwa na Wizara ya Afya, huduma za tiba kama meno na magonjwa mbalimbali, pia magazeti, majarida nk
Vilevi;e usafirishaji wa abiria kwa basi, ndege, treni isipokuwa usafiri wa Taxi, gari za kukodi, boti na ndege za kukodi, huduma za elimu, uuzaji au upangishaji nyumba za kuishi au ardhi nk

3.SHERIA YA USHURU WA STEMPU
Hutumika kuhalalisha miamala ikiwemo hati za kisheria au mikataba mbalimbali. Gharama yake ni 1% ya thamani ya mauzo au sihia kwa maswala ya hati ya kisheria na mikataba hutegemea na viwango maalum vilivyoainishwa kti sheria ya mwaka 1972 na kurejewa mwaka 2006
Muda wa kulipa ushuru wa stempu ni ndani ya siku 30 baada ya kusaini hati au mkataba.

4. KODI YA ZUIO
Utangulizi:

Kodi ya zuio ni kiasi cha kodi kinachozuiwa na mtu anapomlipa mtu mwingine kutokana na bidhaa zilizosambazwa au huduma iliyotolewa na mlipwaji. Mtu anayepokea au anayestahili kupokea malipo ambayo kwayo kodi ya mapato inatakiwa kuzuiwa ni mkatwaji wa kodi ilhali mtu anayepaswa kuzuia kodi ya mapato kutoka katika malipo yaliyofanyika kwa mkatwaji anajulikana kama Wakala wa kodi ya zuio.

Malipo yanayostahili kukatwa kodi ya zuio
Kodi ya zuio inatozwa katika malipo husika ikiwa ni pamoja na malipo yanayopaswa kujumuishwa katika kukokotoa mapato ya mwajiriwa yanayostahili kukatwa kutoka kwa mwajiriwa katika ajira, malipo ya mapato ya uwekezaji ikiwa ni pamoja na magawio, riba, malipo ya maliasili, pango au mrabaha, malipo ya huduma na malipo ya mikataba na malipo ya bidhaa zilizosambazwa serikalini na kwenye taasisi zake.

Taarifa na Muda wa Kulipa Kodi Iliyozuiwa
  • Kila wakala wa kodi ya zuio atalipa kwa Kamishna kodi ya zuio aliyozuia ndani ya siku 7 baada ya kila mwisho wa mwezi wa kalenda.
  • Kila wakala wa kodi ya zuio atapeleka kwa Kamishna ndani ya siku 30 baada ya kipindi cha kila miezi sita ya kalenda taarifa katika fomu maalum iliyoandaliwa inayobainisha malipo yaliyofanywa na wakala katika kipindi husika cha zuio la kodi, jina na anwani ya mzuiwa, kodi ya mapato iliyozuiwa kutoka katika kila malipo yaliyozuiwa; na taarifa nyingine yoyote ambayo Kamishna ataelekeza.
Hati ya Kodi ya Zuio
Wakala wa kodi ya zuio ataandaa na kumtunuku mzuiwa hati ya kodi ya zuio ikionesha kiasi cha malipo alicholipwa mzuiwa na kodi ya mapato iliyozuiwa kutoka katika malipo hayo. Hati ya zuio itahusisha mwezi wa kalenda na itatolewa ndani ya siku 30 baada ya mwisho wa mwezi. Hata hivyo, kwa upande wa kodi inayozuiwa kutoka katika kodi ya ajira hati itahusisha sehemu ya mwaka wa kalenda katika kipindi ambacho mwajiriwa atakuwa amejiriwa na atahudumiwa ifikapo tarehe 30 ya Januari baada ya mwisho wa mwaka au, pale ambapo ajira yake imesitishwa na wakala wa zuio katika mwaka si zaidi ya siku 30 kutoka tarehe ambayo ajira ilisitishwa.

Aina za Kodi za Zuio
Sheria imegawanya kodi ya zuio katika aina kuu mbili, ambazo ni:-
  • Kodi za Zuio za mwisho
  • Kodi za Zuio zisizo za Mwisho
Kodi za Zuio za Mwisho ni kodi ambazo mzuiwa hawezi kudai punguzo lolote la kodi wakati wa kukokotoa kodi ya mapato inayolipwa kwa mwaka wa mapato.
Kodi za Zuio zisizo za Mwisho: ni kodi ambazo mzuiwa anastahili punguzo la kodi kiasi sawa na kodi inayochukuliwa kuwa imelipwa kwa mwaka wa mapato ambamo kiasi hicho kimekokotolewa.

MWISHO
Tunashukuru sana kwa elimu yako lakini ninaomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye bidhaa zilizosamehewa VAT.
Umeeleza vyakula ambavyo havijasindikwa na ukatoa mfano wa unga wa mahindi,nilitaka kujua kama unga tunaouona ukichakatwa kwenye hivi viwanda vidogovidogo na kufungashwa kwenye viroba kama pale Tandale DSM kama nao upo kwenye msamaha wa VAT.
Thnx
 
Asante kwa kufuatilia mada zetu gimmy's

Mahindi kama mahindi as a raw material hayana VAT. Lkn kama yakibadilishwa ie processed na kuwa unga na muuzaji akawa ana kiwango au anazidi mil 100 ya mauzo yake kwa mwaka bidhaa hii ya unga itachajiwa VAT

NOTE: Niwie radhi kwa mkanganyiko wa mfano uliokuwa haupo sawa ie unga vs mahindi. Samahani sana
 
Wazo tu
Suala la kodi hili naona linahitaji elimu sana kwa watu ili kuelewa na kuepuka kuumizwa. Kama kuna kundi la watu wa masuala ya kodi naomba niunganishwe au liundwe kundi la whatsapp la masuala ya kodi tu. Namba ya ofisi yetu ni hii 0755411455
 
Kweli itapendeza tutapata kujifunza zaidi kuhusu kodi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari!
Tukumbushane kulipa kodi ktk robo ya kwanza ya mwaka
IMG_20190326_092848.jpeg
IMG_20190326_092804.jpeg
 
Umuhimu wa kutunza kumbukumbu kwa wafanyabiashara binafsi katika kodi

Tujitahidi sana kuweka kumbukumbu hata kama biashara yako si kubwa kwani inakusaidia badala ya kukadiliwa utafanyiwwa hesabu na kujulikana wazi watakiwa ulipe kiasi gani. Kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi (kifungu cha 35, utunzaji wa kumbukumbu) kuna namna nzuri na za wazi kabisa katika ukokotoaji wa kodi.
Mfano
Mfanyabiashara A ameuza kwa mwaka mzima mauzo ya mil 4,500,000 na haweki kumbukumbu. Makadirio ya kodi atatakiwa kulipa sh 150,000 kwa mwaka

Mfanyabiashara B ameuza kwa mwaka mil 4.5 kwa mujibu wa kumbukumbu zake ie risiti. Huyu malipo yake ya kodi itakuwa 3% ya mauzo yanayozidi mil 4.
Hii ni kwamba
Kodi=4,500,000-4,000,000
Kodi=500,000*3%
Kodi=15,000
(Rejea ukurasa wa 9, kitabu cha Kodi na Ushuru mbalimbali 2018/19)

Na kuboresha vizuri kumbukumbu zako za mauzo nunua mashine ya kielektroniki ie ELECTRONIC FISCAL DEVICE EFD ambayo kwa sasa bei yake kati ya TZS. 580,000 hadi TZS. 590,000, kila ukiuza toa risiti nawe mnunuzi dai rositi pia. Kwani hii inakusaidia kuwafikishia rekodi za mauzo yako Mamlaka ya mapato kila unapotuma Z-Report.
Naambatanisha kitabu
1. Kodi na Ushuru mbalimbali 2018/2019, toleo la Julai, 2018 TRA
2. Umuhimu wa utunzaji kumbukumbu. Nimekutoa ktk mtandao nimeona ni kizuri kwa kujifunza zaidi juu ya uwekaji sahihi wa kumbukumbu. Afrolink-Tz CL si waandishi wa kitabu hiki
3. Kushauri kununua na kutumia EFD mashine haina maana sisi ni wadau au wauzaji wa mashine hizo laah hasha bali tumeshauri ktk kusaidia kuona njia bora zaidi za kulipa kodi halisi kutokana na mauzo yetu, hivyo tusihusishwe na kulazimisha au kutangaza manunuzi ya mashine hizoView attachment KUTUNZA KUMBUKUMBU ZA BIASHARA.pdfView attachment kodi-na-ushuru-July-18-19 (1).pdf
 
Tunakumbushana tu
Kwa wafanyabuashara wenye sifa za kuwasilisha mahesabu ya mizania, ritani TRA, muda wa uwasilishaji unaisha 30.06.2019 kwa mwaka wa fedha 2018. Je tayari mahesabu yako yameshakadiriwa? Wahi muda kabla ya muda haujakuwahi!
IMG_20190529_041802_734.jpeg
 
Back
Top Bottom