Afrolink-Tz Consult Ltd
JF-Expert Member
- Feb 25, 2018
- 424
- 950
- Thread starter
-
- #41
Unaambiwa kwa sababu zifuatazoHapo kwenye kulipa kodi kabla sijaanza biashara,ndio panapoumiza sana kwa nini waniambie nilipe kiasi flani wakati sijajua kama ntauza au sitauza?
Shukrani ndg.Mkuu Mr coffee
1. Ieleweke wazi kuwa malipo ya kodi hayana uhusiano na mtaji wako bali mauzo (kwa biashara ndogo) au faida yako (biashara kubwa)
2. Changamoto kubwa iliyopo ni "lugha ya biashara" kwa tuliowengi hatuwezi au hatuielewi vema. Ipo wazi kabisa kuwa mauzo chini ya mil 4 kwa mwaka hutakiwi kulipa kodi. Tatizo linakuja ktk mahojiano na yule anaekukadiria kodi kwn maswali anayokuuliza juu ya mauzo na ww maelezo unayotoa juu ya biashara yako akifanya hesabu zinazidi zaidi ya mil 4 kimauzo UTAKAPOKUJA ANZA KUFANYA BIASHARA. Hivyo unalipa kama malipo ya awali 'advance payment' ambayo una haki ya kutoa maelezo au kuirekebisha baadae kama mambo hayapo sawa
Iwapo jengo ni la kwako utalipa kodi ya jengo ambayo ulishakadiriwa na manispaa yako husika. Malipo kwa nyumba nyingi za kawaida ni kuanzia elfu Tsh 10,000 kwa mwaka. Hivyo hautalipa kodi ya zuio wala ushuru wa stempuMKUU, Utaratbu wa kulipia hiyo witholding Tax (kodi ya zuio) na ushuru wa stempu, inakuwaje ikiwa jengo ni la kwangu na sikupanga?
Matarajio ni kuwa wengi wetu tutaisoma makala hii na kuelewa vizuri kwani inawezekana kuwa malalamiko mengi hutokana na wafanyabiashara au/na wanaofikiria kufanya biashara kutoelewa vizuri sheria na kanuni.MAKALA: SEHEMU YA KWANZA
Habari zenu wanajukwaa
1. Utangulizi
makala hii inahusu masuala ya kodi kwa wanaoanza biashara lakini vilevile itagusa sheria na biashara kwa ujumla wake. lengo ni kuzidi kuelimishana kwa wasiofahamu na vilevile kukumbushana kwa wenye ufahamu na kuongezeana elimu kwa michango mbalimbali itakayoletwa kutoka kwa wanajukwaa.
2. Biashara na aina zake
Biashara ni kununua na kuuza, kuzalisha mali na kuuza, utaalmu, wito na makubaliano ya kipekee yenye nia ya kupata faida kwa kifupi ili nisiwachoshe.
kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya mwaka 2003 ya kuendeleza wajasiriamali wadogo, wa kati na wakubwa, biashara zimegawanyika katika makundi manne:
1. Biashara ndogo sana
Ina idadi ya waajiriwa kuanzia mmoja hadi wanne, na Mtaji wake ni kuanzia Sh 1 hadi 5mil
2. Biashara ndogo
Ina idadi ya waajiriwa 5 hadi 49, na mtaji wake ni kuanzia mil5 hadi mil 200
3. Biashara za kati
Ina idadi ya waajiriwa 50 hadi 99 na mtaji ni kati ya mil 200 hadi mil 800
4. Biashara Kubwa
Ina idadi ya waajiriwa zaidi ya 100 na mtaji zaidi ya mil 800.
Vingezo vingine vinavyotumika na Mamlaka ya Mapato kuweka madaraja ya walipa kodi ni kulingana na kiasi cha mauzo kwa mwaka au kiasi cha kodi kinacholipwa kwa mwaka
3. SHERIA ZA KODI
Shera hizi zinamgusa anaeanza biashara:
1. Sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004
2. sheria ya kodi ya Ongezeko la thmani (VAT) ya mwaka 2014 kwa anefuzu kusajiliwa
3. Sheria ya ushuru wa stempu ya mwaka 1972
4. sheria ya usimamizi wa kodi ya mwaka 2015
Sheria hizi zinasimamiwa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kupitia kodi za ndani
A: Sheria ya Kodi ya Mapato
Kodi ya mapato hutozwa kwa mtu ambaye mapto yake yanatokana na vyanzo mbalimbali km vilivyoainishwa ktk sheria kama vile
a) Biashara yoyote na kwa muda wowote inapofanyika
b) Ajira yoyote afanyayo mtu
c) Uwekezaji ktk rasilimali. Mfano nyumba, ardhi na hisa
d) Vyanzo vinginevyo vya mapato vya kutozwa kodi ya zuio "Final Withholding Tax. Mf: Kodi ya malipo ya pango, malipo ya gawio kutoka ktk kampuni kwa Mtz, Riba itokanayo na benki na malipo kutokana na maliasili (mrahaba)
B: Mapato yatokanayo na biashara
kwa mujibu wa sheria ya kodi ya mapato ya mwaka 2004 ikarejewa mwaka 2006, Mapato yanayotozwa kodi kutokana na biashara ni Faida au Ziada itokanayo na biashara kwa mwaka wa mapato. Mapato hayo ni pamoja na:
1. Faida kutokana na mauzo ya bidhaa au huduma za biashara
2. Malipo anayolipwa mfanyabiashara kwa masharti ya kufanya au kutofanya biashara kulingana na makubaliano ya upande wa pili
3. Zawadi au Takrima anazolipwa mfanyabiashara kutokana na shughuli zake za biashara
4. Kiasi cha mapatoyanayohusiana na biashara ambayo vinginevo yangekuwa mapato ya uwekezaji ktk rasilimali kwa mtu anayefanya biashara ya kupangisha nyumba`
Inaendelea.......
B: Taratibu za kufuatwa na mtu anaeanza biashara kupata namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN) pamoja na malipo ya kodi na mengineyo:
Mtu anaeanza biashara atatakiwa kuomba TIN kutoka TRA ambapo vielelezo hv vitahitajika
1. Fomu za maombi ya TIN kwa mtu binafsi (zinatolewa TRA)
2. Barua ya utambulisho wa Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa (hutolewa na TRA)
3. Mkataba wa pango kwa aliepanga eneo la biashara au kielelzo cha umiliki wa eneo la biashara kama hati, ofa au karatasi za malipo ya kodi ya majengo
4. Kopi ya kitambulisho cha Taifa, Leseni ya udreva, paspoti ya kusafiria au kitambulisho cha kupigia kura
5. Picha ndogo ya paspoti saizi
Mhusika utaulizwa juu ya biashara yako "business assessment". baada ya hapo utaambiwa kiasi cha kodi utakayostahili kulipa kutokana na mauzo ya biashara unayofanya au unayotarajia kuifanya. baada ya maelezo haya taratibu nyingine zitaendele na hatimaye utapata TIN.
Kwa leo naomba tuishie hapa sehemu ya kwanza kutokana na majukumu. Tutaendelea sehemu ya pili
Nakushauri usome makala imeelezea vema sana suala la EFD usione uvivuMkuu kwaiyo risiti isiyo ya efd inahusisha hadi biashara zenye mauzo ya million 4?
TIN isiyo ya biashara ndo ipoje? Unakua hulipii chochote baada ya kupewa TIN ama?Unaambiwa kwa sababu zifuatazo
1. Maelezo yako ya msingi juu ya mauzo utakuwa umesema mauzo kwa mwaka akifanya hesabu yanazidi mil 4
2. Unatakiwa kulipa kodi kwa awamu nne, awamu ya kwanza utalipa ndani ya siku 90 toka kukadiriwa hvy bhasi km biaahara sio una haki ya kurudi TRA kujaza fomu ya marekebisho lkn ile awamu ya kwanza uilipe
3. Kuanza biashara ni mchakato, hvy bhasi ina maana tyr umeshajipanga. Vinginevyo omba TIN isiyo ya biashara
Fanya kusubscribe kama Mimi nilivyofanyaMakala muhimu sana hii. Tag me plz Afrolink-Tz Consult Ltd
Ni TIN isiyohusiana na masuala ya biashara.TIN isiyo ya biashara ndo ipoje? Unakua hulipii chochote baada ya kupewa TIN ama?
Nimekupata mkuu,ubarikiwe sanaNi TIN isiyohusiana na masuala ya biashara.
Mifano:
1. TIN ya kuombea leseni ya udreva
2. TIN ya kulipia kodi ya jengo
Kwa mfano unapotaka leseni ya udreva, utapata hy Non-Business TIN. Itakusaidia kulipa ze kodi stahiki tu kwa mfano unapoomba au ku- 'renew' leseni ya udreva utalipia. Ukitaka kuanza biashara unatoa taarifa inabadilika inakuwa business TIN hivyo utalipa kodi ya mapato kama kawa!
Asante Mkuu Laki Si Pesaasante kwa somo zuri, naomba ufafanuz jinsi ya kupata TIN TRA kwa kundi la kampuni, taasisi . na hiyo kodi inayokatwa kwa kampuni kutokana na faida inakatwa kwenye gross profit au net profit
Mkuu, Naomba kuhuliza swali, JE kuna uwezekano wa kufuatilia leseni ya biashara kabla ya kupata TIN number kwa maana nilifika TRA kuanza hatua za awali za kupata Hiyo namba ya mlipa kodi lakini baada ya kukinzana kwa hoja kati yangu na bwana mmoja wa TRA ambaye alikuwa akinioji kuhusu biashara yangu,ambaye alilenga kunipa makadirio makubwa. Akaniambia nianze biashara, nitunze kumbukumbu then baada ya mwezi nirejee waangalie biashara yangu.
Je, ni naweza kupata leseni ya biashara?
Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23] Hawa maafisa ovyo sana eti ananidanganya na kuniona lofa sana, kwa kuniambia TRA wanachukua 800 Tsh ikiwa mtu anauza 15000tsh kwa siku ...
harafu aka malizia na neno tu! !!
Mbaya zaidi akajifanya anakorogakoroga mahesabu mengi ili nisimuelewe, mwisho wa siku ni kabakia pale pale ya kuwa makisio yake mengi kwangu.
Sent using Jamii Forums mobile app