Lucas Mwashambwa
JF-Expert Member
- Jul 28, 2022
- 28,722
- 20,610
- Thread starter
- #101
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais.Huyu mama ,atakuja kufungwa.
Ni mhujumu uchumi
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais.Huyu mama ,atakuja kufungwa.
Ni mhujumu uchumi
Nimesema huyu mama. Sijasema mheshimiwa Rais.Uwe na adabu kwa Mheshimiwa Rais.
Acha utoto wako.Nimesema huyu mama. Sijasema mheshimiwa Rais.
Wa kusamehewa ni wewe maana hujitambui.Wewe nakusamehe bure kabisa maana akili yako inafahamika vyema.
Wewe hujitambui hata kidogoWa kusamehewa ni wewe maana hujitambui.
Kuna msemo unasema mtu akiwa mjinga hawezi kujijua kama ni mjinga na haumii bali wanaomzunguka ndio huona ujinga wake na ndio wanaoumia.
Safi sana Lucas MwamshambaNdugu zangu Watanzania,
Hii ni makala yangu ya wazi kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan Shujaa wa Afrika,Nuru ya wanyonge,Nyota ya Matumaini na jasiri Muongoza njia.Ni makala Ya kumtia moyo,kumpa faraja,kumpa pole kwa kazi nzito afanyayo pamoja na kumuombea afya njema na nguvu za kuendelea kuliongoza Taifa letu.
Mama yangu,mama yetu ,Rais wangu ,Rais wetu nipende kusema na kuanza kwa kusema Shikamoo Mama. Rais wetu, Mamillioni ya Watanzania wanaendelea kukuombea dua njema,kukuunga mkono wewe binafsi na serikali yako. Hii ni kwa kuwa kwa mikono yako umegusa maisha ya wengi,umewafuta machozi wengi,kuwapa matumaini mamilioni ya watanzania,kuwainua wengi ,kuwapa faraja waliokuwa wamekata tamaa,kuwashika mkono waliokuwa wameanguka na kuishiwa nguvu.
Kwa macho yako ya huruma ,kwa maamuzi yako,kwa sera zako ,kwa vipaombele vyako,kwa hatua zako,ajenda zako,kwa maoni yako,kwa ucha Mungu wako,kwa utu,upendo,huruma na unyenyekevu wako umewapa nuru mamilioni ya watanzania waliokuwa gizani, umesaidia wengi kutimiza ndoto zao,umewaondoa wengi katika dimbwi la umaskini,umewaamsha na kuwapa matumaini wagonjwa wengi waliokuwa wamelala Vitandani wakiwa wamekata tamaa kutokana na hali ya umaskini na kukosa pesa za kupata matibabu,lakini wewe uliwapelekea madaktari bingwa huko huko waliko.
Kwa ulimi wako umeliunganisha Taifa,umewaleta watu pamoja waliokuwa maadui na wakaweza kuzungumza lugha moja,kwa ulimi wako na matendo yako ya haki na huruma na hofu yako kwa Mungu umewapa imani waliokuwa wamekosa Imani ya kuishi na kurejea hapa Nchini,umewahakikishia usalama wao.
Lakini Mama yangu na Rais wangu Mpendwa pamoja na hayo mazuri na mengi Mema uliyoyatenda kwa Taifa letu.Bado kuna watu kwa kukosa uungwana na shukurani,kwa chuki binafsi,kwa maslahi yao binafsi,kwa kutumiwa na kutumika na watu wenye nia ovu wamekuwa wakikushambulia kwa lugha za matusi , udhalilishaji,ubaguzi,chuki na kutweza utu wako. Wamekwenda mbali zaidi kwa kuanza kudhalilisha na kushambulia familia yako na kuihusisha na kila aina ya ubaya kwa lengo la kukuchafua na kukuchonganisha na wananchi wako wenye imani kubwa na wewe.
Lengo lao ni moja tu Rais wangu kwako. Nalo ni kwamba wanataka kukuvunja moyo,kukukatisha tamaa,kukudhoofisha,kukupunguza kasi,kukuondoa kwenye reli,kukuhamisha na kukupa ajenda zao ndio uwe mjadala wa kitaifa kwa maslahi yao.wanataka kukunyong'onyesha na kukuvuruga hasa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu. Wanataka wakuchosha akili na kukutikisa,kutetemesha,kukutetelesha pamoja na kukupa hofu na uoga.
Ndio sababu ya kuona wakitunga kila aina ya uzushi usio na ushahidi,kutumia lugha kali kali na mbaya pamoja na kuishambulia familia yako hasa mwanao wa kiume.
Lakini Mheshimiwa Rais Wangu Napenda kukuambia ya kuwa usiogope,usiteteleke,usiteteleshwe,usikate tamaa,usikatishwe tamaa wala kuvunjwa au kuvunjika moyo,usiumie Rais wangu maana tayari umeshaogelea katika bahari ya siasa yenye kila aina ya Mawimbi mpaka hapo ulipofika umri huo .Najuwa umepitia mengi na umekomaa na kuiva na hakuna geni kwako la kuweza kukuondoa katika reli ya kuwatumikia watanzania wenye imani kubwa na uongozi wako.
Rais wangu Mpendwa Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hasssan,Uwe Hodari na Moyo wa Ushujaa . USIOGOPE kwa kuwa Mungu aliyekuinua kwa mkono wake Hodari yupo bado na wewe.Uso wake upo na wewe na mkono wake upo juu yako na yeye yupo ndani yako.
Narudia tena kusema Mama Yangu USIOGOPE. Uwe HODARI na Moyo wa USHUJAA. MUNGU yupo pamoja na wewe.
Kikubwa nakuomba uhakikishe unaendelea kulinda Taifa letu kuendelea kuwa na amani na umoja wa kitaifa. Linda kwa uzalendo ,Wivu ,jasho na Damu kila kitu kilicho mali ya watanzania ndani na nje ya Taifa letu. Usibabaishwe na yeyote. Tumekukabidhi kila kitu mikononi mwako kikatiba. Tumekupa na kukuwekea Vyombo vyote vya ulinzi na usalama vyenye uzalendo uliotukuka na wa mfano kuwa chini yako. Vitumie na saidiana navyo kupigania na kulinda maslahi ya Taifa letu.
Ni mimi Lucas Hebel Mwashambwa. Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa.
Safi sana Lucas Mwamshamba
Asante NashukuruSafi sana Lucas Mwamshamba
Wamepoteana!Nafasi ya uteuzi inavyowatesa Uvccm.
Uchawa utakupeleka pabaya....Yaani mtu anateua marehemu kuongoza waliokwisha kufa bado unampa mavyeo yote haya?Kwani uchawa upo wapi hapa ndugu yangu mtanzania.
Mimi ni msema kweli na siyo chawa.Uchawa utakupeleka pabaya....Yaani mtu anateua marehemu kuongoza waliokwisha kufa bado unampa mavyeo yote haya?
Mimi Sitafuti uteuzi hapa jukwaaniChawa Kashiba Damu Anabwata Tu Hana Cha Kupoteza Anangoja Teuzi
Kwani Ungesemaje ?Mimi Sitafuti uteuzi hapa jukwaani
Nasema kwamba mimi sipo hapa na siandiki kwa ajili ya kutafuta uteuzi ndugu yangu.Kwani Ungesemaje ?
Watanzania Siyo Wajinga Wanajua, Wanaona
Nitakujibu vizuri nikitulia maana umeorodhesha mambo mengi na mchanganyiko. Ila hongera sana maana inaonyesha umekula chumvi nyingi.maana uliposema umesoma na Mtoto wa Nyerere nikaona kwa hakika umetoka mbali na nchi yetu na unaweza kueleza baadhi ya matukio ya kihistoria kwa Taifa letu pasipo kusoma kitabuni. Asante lakini kwa mawazo yako na mchango wako ambao nitakujibu vyema baadaye.Mwashamba uko vizuri katika kutetea Chama chako lakini,; mama antakiwa asaidiwe kujua hali halisi, kwenye mikutano yetu ya kijani wote tunapiga kelele mitano tena lakini hii mitatu ya kwanza mambo ni mengi ya kufikilisha, deni la Taifa limepaa ukilinganisha na uwiano wa muda na uwezo kulipa mikopo hiyo kwa muda, leo hii wakandalasi za ujenzi wa miundombinu ilikadiliwa kuwa Tilion 11 wakandalasi wamesimama kazi karibu 80 asilimia ya miradi imesimama, hali ngumu bei ya mafua juu maana kodi nyingi zimejazwa hapo hata pa kupumulia hakuna, mafisdi wanatanua bila woga mama anakusanya watu wanameza, kazi ya Urais si rahisi sana na ukishaweka ushoga, undugu , urafiki, upenzi, uewano uzazi, uana, ukanda nk nk watu wanatumia mwanya huo huo, nilisoma na mtoto wa Nyerere sekondari alipanga foreni ya chakula kama sisi alilala kwenye bweni kama sisi tena kwa baadhi ya watu ilikuwa si rahisi kujua huyu ni mtoto wa Rais, hizi mbwembwe zinatoka wapI? unakwenda ziara ya kiserikali na wazazi wako!! ili iweje watanue wakusifie tumezaa mtoto!! unabeba wasanii ziara ya kiserikali mmmh ili iweje wajifunze usanii, wapeleko kivyao waende wakae na wenzao muda wa kutosha wajifunze. ukweli tunampenda Samia lakini vitu vingine mmmmh vinatia ukakasi. amefungua milango na madilisha yote kila kitu hakina kizuizi impact yake tutaiona baadae, inawezekana asiwepo madarakani lakini tutaumia sana.
Kuandika kwa ufupi, na ujumbe ufike ulivyokusudiwa, inahitaji akili na uwezo mzuri.Mleta mada Siku ingibe ukiandika chochote Kwa Raisi kisizidi sentensi 10
Ana kazi nyingi za kufanya Sio kusoma mangonhera Yako marefu hayo
Nikufundishe unapoandika Kwa mtu wa Chini ikiwa raia wa kawaida unaandika kirefu unapoandika Kwa bosi aliye juu unatakiwa kuandika kifupi na direct to the pointi
Acha uvivu wako.Kuandika kwa ufupi, na ujumbe ufike ulivyokusudiwa, inahitaji akili na uwezo mzuri.
Umbu hacha uchawa ongea basi ukweli tukupongeze ila kwa haya unayoyaandika ndugu yangu unajipaka kinyesi..Mimi ni msema kweli na siyo chawa.
Salamu zangu za pole zikufikie popote ulipo kwa maana hapa tumepigwa na kitu kizitoNdugu zangu Watanzania,
Hii ni makala yangu ya wazi kwa Rais wetu mpendwa na Jemedari wetu kipenzi cha watanzania Mheshimiwa Daktari Samia Suluhu Hasssan Shujaa wa Afrika,Nuru ya wanyonge,Nyota ya Matumaini na jasiri Muongoza njia.Ni makala Ya ko. Vitumie na saidiana navyo kupigania na kulinda maslahi ya Taifa letu.
Ni mimi Lucas Hebel Mwashambwa. Naweka kalamu yangu chini na kuishia hapa.