Pre GE2025 Makalla: Lissu ni ndugu yangu yupo mbioni kuja CCM maana CHADEMA wanaendekeza rushwa wakati Lissu hapendi kabisa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwa kabisa kujibu kiu ya Lissu ambapo Lissu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya CHADEMA lakini hawana mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makalla amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lissu akisema CHADEMA sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
---

1723312909499.png
Misenyi. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amemkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu kujiunga na chama hicho akidai tayari chama chake kimeacha misingi yake.

Makalla ameeleza hayo Agosti 9, 2024 kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika katika Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera anakoendelea na ziara ya siku nne.

Ukaribisho huo umetolewa zikiwa zimepita siku chache baada ya Lissu kunukuliwa akisema Chadema si mama yake na kwamba, atakuwa tayari kukihama chama hicho endapo kitakiuka misingi yake.

Hata hivyo, alipotafutwa Lissu amesema, "Mimi nijiunge na chama chao? Yaani niende CCM kwa sababu gani au wana misingi ipi?CCM kuna nini niende kufuata? Tukajenge Taifa kwa... muulizeni Makalla anafikiria mimi nitajiunga na CCM?,’’ amehoji.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Makalla amemkaribisha Lissu kujiunga na CCM akidai tayari chama chake kimepoteza misingi yake, hivyo anakaribishwa kujiunga na CCM ili wafanye kazi pamoja kulijenga Taifa.

Amedai kwa sasa Chadema ni chama kisichofuata misingi ya demokrasia, kinakabiliwa na rushwa, viongozi wake hawana mpango wa kutoka madarakani na hakihubiri umoja wa kitaifa, hivyo Lissu hana sababu ya kuendelea kuwa huko.

"Kwa usomi wake Tundu Lissu, sehemu pekee ya kufanya siasa ni kwenye Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo nimkaribishe ndugu yangu Lissu aje tufanye kazi, tuijenge nchi yetu," amesema Makalla.
 
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwq kabisa kujibu kiu ya Lisu ambapo Lisu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya chadema lakini chadema haina mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makala amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lisu akisema chadema sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
Makalla anasema uongo kama Donald Trump.
 
Amewalisha matango pori wengi nccr nao wanaamini hili!

Lissu huyu huyu au mwingine?
Watahamia wote sio Mheshimiwa Lissu
 
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwq kabisa kujibu kiu ya Lisu ambapo Lisu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya chadema lakini chadema haina mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makala amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lisu akisema chadema sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
Makala atulie tuli , inawezekana kabisa chadema kukawa na arufu ya rushwa ambayo inaweza dhibitiwa ila sio kwa kiwango kile cha ndani ya ccm,

Lissu akiona chadema imepoteza dira na kwa kua chama cha siasa sio baba yake au mama yake bora kuacha siasa kuliko kwenda ccm au chama kingine why nasema hivi.

Kuna weza kuwa na njia ya kuanzisha chama ila sio wakati sahii kwa sasa , na wala hata lissu anaweza Gombea pitia chama kipya hakiwezi leta matokeo chanya.

Ila all in all figisu za ccm zinajulikana tukaribiapo chaguzi, sioni kama chadema kuna mgawanyiko bali ni mambo madogo dogo tu , kwani wamepitia Mangapi? kwa sasa ni nguvu moja tu

ZIMA KIJANI WASHA NYEKUNDU ,NYEUPE ,
 
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwq kabisa kujibu kiu ya Lisu ambapo Lisu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya chadema lakini chadema haina mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makala amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lisu akisema chadema sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
Hiyo Rushwa anayosema Lissu inatokea huko CCM
 
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwq kabisa kujibu kiu ya Lisu ambapo Lisu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya chadema lakini chadema haina mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makala amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lisu akisema chadema sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
Ndoto nyevu ni hatari sana kwa watu wazima
 
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwq kabisa kujibu kiu ya Lisu ambapo Lissu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya chadema lakini chadema haina mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makala amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lisu akisema chadema sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
Ni kweli Lissu hapendi Rushwa ila rushwa hiyo alisema inatoka wapi? siyo CCM! je tushughulike na Supply chain(ccm) au Demand chain(chadema) kuiondoa Rushwa hii? Nipeni suluhisho la kudumu. Lissu yeye kasema kiujumla. Kamaliza.
 
Kwa hilo jibu laini kutoka kwa TAL, nashawishika pasi na shaka kusema kwamba huenda kweli yuko mbioni kujiunga na Sisiemu, kama hajajiunga nao moyoni tayari!
 
Akihutubia wananchi wa mkoa wa Kagera makala amesema chadema wameshindwa kabisa kujibu kiu ya Lissu ambapo Lissu amelalamikia rushwa na kukosekana demokrasia ndani ya CHADEMA lakini hawana mpango wowote kuyashughulikia.

Ndugu Makalla amesema kutokana na ukweli huo alimsikia Lissu akisema CHADEMA sio mama yake ikionyesha kuwa yuko njiani kukihama chama hicho.
---

Misenyi. Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Amos Makalla amemkaribisha Makamu Mwenyekiti wa Chadema (Bara), Tundu Lissu kujiunga na chama hicho akidai tayari chama chake kimeacha misingi yake.

Makalla ameeleza hayo Agosti 9, 2024 kwenye mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM, Dk Emmanuel Nchimbi uliofanyika katika Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera anakoendelea na ziara ya siku nne.

Ukaribisho huo umetolewa zikiwa zimepita siku chache baada ya Lissu kunukuliwa akisema Chadema si mama yake na kwamba, atakuwa tayari kukihama chama hicho endapo kitakiuka misingi yake.

Hata hivyo, alipotafutwa Lissu amesema, "Mimi nijiunge na chama chao? Yaani niende CCM kwa sababu gani au wana misingi ipi?CCM kuna nini niende kufuata? Tukajenge Taifa kwa... muulizeni Makalla anafikiria mimi nitajiunga na CCM?,’’ amehoji.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Makalla amemkaribisha Lissu kujiunga na CCM akidai tayari chama chake kimepoteza misingi yake, hivyo anakaribishwa kujiunga na CCM ili wafanye kazi pamoja kulijenga Taifa.

Amedai kwa sasa Chadema ni chama kisichofuata misingi ya demokrasia, kinakabiliwa na rushwa, viongozi wake hawana mpango wa kutoka madarakani na hakihubiri umoja wa kitaifa, hivyo Lissu hana sababu ya kuendelea kuwa huko.

"Kwa usomi wake Tundu Lissu, sehemu pekee ya kufanya siasa ni kwenye Chama cha Mapinduzi. Kwa hiyo nimkaribishe ndugu yangu Lissu aje tufanye kazi, tuijenge nchi yetu," amesema Makalla.
Sawa.... But ujue atakuja na mkewe tu....
 
Back
Top Bottom