Pre GE2025 Makamba: Hata kama hatumkubali Rais Samia, ni wetu

Pre GE2025 Makamba: Hata kama hatumkubali Rais Samia, ni wetu

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Waziri Januari Makamba amesema hata kama hatumkubali Samia ni wetu hivyo tunatakiwa kuacha siasa hasa kuhusu ziara zake nje ya nchi kwani zimeleta manufaa makubwa kwa nchi.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea

Zaidi sikiliza hii link mpaka mwisho

Makamba unasema hatumkubali Rais wewe na nani ambao hamumkubali rais mimi sijawahi kusikia kiongozi hata mmoja aliyeteuliwa na rais akisema hayo maneno hatakama hatumkubali wewe umejuaje kama wengine hawamkubali? Rais Samia waangalie vizuri hawa vijana wako na hizi kauli zao ni jambo nyuma
 
"Hata kama hatumkubali, Rais Samia ni wetu"

Hii statement ni very "ambiguous" yenye kitu nyuma yake.

Na ieleweke wazi kuwa, ni kweli kabisa kuwa Samia Suluhu Hassan hakubaliki na ni mzigo mzito usio na faida yoyote kwa Wa - Tanganyika

Hata hivyo kwa kauli hii kutolewa na January Makamba waziri mteule wa huyu Rais "asiyekubalika" lakini tulazimike kumkubali hivyo hivyo kwa sababu ni wetu, mtu mwingine anaweza kufikiri hivi:

√ Kwamba, hata yeye January Makamba hamkubali Samia lakini kwa sababu ni wetu basi hana la kufanya inabidi amkubali tu..!

√ Lakini all in all, najiuliza, was it necessary kwa January Makamba kutumia maneno haya kuelezea kilichokukuwa kichwani mwake kiasi cha kusababisha mjadala kumhusu?
Karopokwa bila kujijua anasema nini na kwamba italeta impression gani kwa wajuzi wa dots !
 
Waziri Januari Makamba amesema hata kama hatumkubali Samia ni wetu

By
X dot com / JMakamba


January Yusuf Makamba,

Hakuna sababu ya kuongopa. Taarifa tulizotoa kwa umma zipo wazi kwamba safari ya Mhe Rais Samia Suluhu Hassan nchini Korea ina sehemu mbili: sehemu ya kwanza, Rais wetu amealikwa na Rais wa Jamhuri ya Korea, yeye kama Rais wa Tanzania, kufanya ziara rasmi ya mahusiano ya nchi na nchi (bilateral) nchini Korea; sehemu ya pili, amealikwa pamoja na Marais wenzake wa Afrika kujumuika nao kuhudhuria Mkutano wa Korea-Africa Summit.

Nimeweka picha ya sehemu ya taarifa yangu kuonyesha kwamba tulisema ukweli.Sehemu ya kwanza ya ziara hii imefanyika tarehe 2 Juni 2024, ambapo Rais wetu alikaribishwa na Rais mwenzake Ikulu ya Korea kwa mazungumzo ya uhusiano kati ya nchi mbili, chakula cha heshima cha mchana, na kusaini mikataba, ukiwemo wa dola bilioni 2.5.

Hapa, tofauti na unavyotuhumu, hakukuwa na Rais wa nchi nyingine. Sehemu ya pili ya ziara itakuwa tarehe 4 - 5 Juni, ambapo Rais wetu amealikwa na wenzake wa Afrika kuhudhuria Mkutano wa Kwanza wa Marais wa Afrika na Korea.

Taarifa za Mkutano huu zipo mitandaoni. Katika mkutano huu, Rais wetu atahutubia kwenye Mkutano Mkuu wa Pamoja wa Ufunguzi (plenary) na pia atazungumza kwenye majopo mawili (panels): moja, kuhusu miundombinu na la pili kuhusu usalama wa chakula na madini. Rais wa Korea alionelea amualike Rais wetu kwa ziara yake mwenyewe katika kipindi hiki cha kuelekea Mkutano wa Korea-Africa Summit ili iwe rahisi kufanya mambo mawili katika safari moja: kufanya ziara ya mahusiano ya nchi na nchi na kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Korea na Afrika.

Ukisoma taarifa zetu ndivyo tulivyosema. Kwenye mahusiano ya Kimataifa mambo kama haya ni ya kawaida. Majuzi tu, hata sisi tulialika Marais kadhaa kwenye Sherehe za Kuadhimisha Miaka 60 ya Muungano tarehe 26 Aprili 2024, ikiwemo Rais wa Somalia. Siku iliyofuatia, 27 Aprili, Rais wa Somalia akafanya ziara ya kitaifa (State Visit) nchini na kupewa itifaki stahiki.Katika mipango ya ushirikiano wa Kimataifa, Tanzania ni moja kati ya nchi za Afrika zilizopewa kipaumbele na Korea.

Pia Tanzania ni moja kati ya nchi tatu ambazo Korea imeamua kufanya nazo makubaliano makubwa ya Ushirikiano wa Kiuchumi (Economic Partnership), ambapo leo, mbele ya Marais wawili katikaIkulu ya Korea, tumesaini hilo Tamko. Pia kwa Korea, Tanzania ni nchi ya pili kwa kupokea ODA kubwa zaidi, baada ya Misri.

Kumekuwa na manufaa makubwa katika ushirikiano na Korea. Kwa uchache sana, kuanzia mwaka huu tu pekee, manufaa yanayotarajiwa ni:- hospitali yote ya Muhimbili kujengwa upya kabisa na kuwa kubwa zaidi na ya kisasa zaidi na pia ujenzi wa Chuo Kikubwa Cha Kisasa cha Teknolojia kule Dodoma.

Katika Mkutano kati ya Rais wetu na Rais wa Korea, mambo mapya makubwa ya ushirikiano yameamuliwa ikiwemo ushirikiano mpya kwenye Uchumi wa Kidijitali, Kusambaza Elimu Kidijitali hadi Vijijini, Uchumi wa Bluu, Kuongeza Thamani kwenye Madini Nchini na Ujenzi wa Miundombinu.

Baada ya Korea-Africa Summit kunatarajiwa kutolewa Tamko la Pamoja la Ushirikiano Mpya kati ya Afrika na Korea. Leo Mawaziri wa Mambo ya Nje tumekaa na kupitia Tamko hilo kabla kikao cha Marais tarehe 4 Juni.Nimechukua ushauri wa Fatma Karume kwamba tuwe tunaelezea,hata kama ni kwa urefu kiasi gani, haya mambo ili kusaidia kuelimisha.
 
TOKA MAKTABA
Wazee wa CCM wamkingia kifua kiongozi mkuu wa CCM kufuatia kauli iliyopo ktk waraka wa baadhi wa viongozi ...

2019 20 July

WAZEE WA DAR ES SALAAM WALIVYOCHAFUKWA RAIS KUBEZWA


View: https://m.youtube.com/watch?v=e6s20MCt_zE
Mwenyekiti wa baraza la wazee wa Chama cha Mapinduzi CCM, Mkoa wa Dar es salaam Hemedi Bakari Mkali amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar- es salaam kuhusu waraka uliondikwa na Makatibu wakuu wawili wastaafu Abdurahman Kinana na Mzee Yusuph Makamba ...

Waraka wa Kinana na Makamba wageuka kaa la moto,wabunge ccm wazidi ibuka.​

msekwapic.jpg

Date: July 20, 2019 Author: mtezamedia0
WARAKA uliotolewa na Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Yusuf Makamba na Abdulrahman Kinana wageuka kaa la moto ndivyo unaweza kusema baada ya kuibuka wabunge wa chama hicho kuwapinga wastaafu hao.
Wiki iliyopita Kinana na Makamba waliandika barua kwa Baraza la Wazee wa CCM, wakitaka chama kichukue hatua dhidi ya mtu anayewachafua, huku akijipambanua kuwa mwanaharakati huru anayepambana na wanaomuhujumu Rais Dk. John Magufuli.

Kutokana na hilo, Bashe alisema waraka huo una malengo ya kugawa chama na kuwataka viongozi hao wastaafu wapambane na mtu huyo bila kuingiza chama kwenye vita yao.

Jana, Mbunge wa Simanjiro, James ole Millya, naye alisema yeye si shabiki wa mwanaharakati huyo, lakini Watanzania watafakari kwa kina taarifa ya wastaafu hao.

“Je, mzee Makamba na Kinana wana uhalali gani wa kisiasa (moral authority) ya kukosoa CCM ya Dk. Magufuli iliyorudi kwenye misingi iliyoanzishwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere kinyume na CCM yao waliyohudumu kwenye vipindi tofauti ambayo dhamira yake ilikuwa ni kuhudumia wachache ambao ni matajiri (mafisadi)?” alihoji Millya.



Akihojiwa na kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star Tv jana, Mbunge wa Geita Mjini, Joseph Msukuma, alisema waraka wa wastaafu hao umewafanya waamini wanazo njama kubwa.

“Ule waraka umetufanya tuamini kumbe yule (Cyprian) Musiba sio kichaa, ni mwanaharakati, anaeleza mpango wa kihuni unaofanywa na hawa wazee.
“Jana niliandika kwenye group la Bunge kuwa uvumilivu una mwisho, huwezi kumwita Rais mshamba na amechanganyikiwa.

“Huo waraka ni wa kijinga, hawa wazee wakiendelea tutawapiga na tutasema uozo wao maana kati ya hao wazee wapo waliokuwa wanaingiza makontena kwa wizi, wamwache Rais, na mimi namshauri Rais asiwasikilize,” alisema Msukuma.

Mbunge wa Mtera Livingstone Lusinde, Leo katika Mkutano wake na waandishi amesema kuwa Waraka wa wazee hao wamepotoka kwa kutoa waraka ambao umewaonyesha ni wanasiasa wazoefu lakini musiba amewaendea kwenye jicho wasiloliona na hawakupaswa kuutoa huo waraka
 
Waziri Januari Makamba amesema hata kama hatumkubali Samia ni wetu hivyo tunatakiwa kuacha siasa hasa kuhusu ziara zake nje ya nchi kwani zimeleta manufaa makubwa kwa nchi.

Waziri Makamba ameyasema hayo leo 6.6.2024 akizungumzia ziara ya Rais Samia nchini Korea

Zaidi sikiliza hii link mpaka mwisho

Khee, mbona ana haraka kusema hatumkubali Rais? hiyo hofu anaitoa wapi
 
Back
Top Bottom