Makamba unampa taarifa za uongo Rais kwa faida ya nani?

Pascal Mayalla Makamba alionekana kipanga na ana akili sana kwa sababu alikuwa hajawahi kukabidhiwa jukumu rasmi la kulisimamia yeye kama yeye ndio maana siku zote ilikuwa sio rahisi kuujua uwezo wake ila alipopewa Wizara ya Mazingira na Sasa Nishati ndio watanzania sasa wanaujua rasmi uwezo wake bila kusimuliwa na mtu yoyote.
 
Aaah brother! Yani enzi za JPM project ilikuwa uzalishwe umeme ila usimbazwe! Ila enzi za Samia ndo wakawaza ilo baada ya kushika kijiti Makamba! Hapa umetudanganya Pascal.

Wote wamefanya kwa mwaka 1 na miezi 9 iyo project! Ila kusema ukweli ata wahariri wa vyombo vya habari walikuwa wanaenda Rufiju kujionea, tbc walikuwa na kipindi kila weekend kuonesha maendeleo ya mradi! Kimsingi hakuna tofauti kubwa tangia kile kipindi cha tbc kife mwez May 2021 na yale tuliyoyaona jana.
 
Tatizo sio Makamba, hakujipa hicho cheo!

Kama ni lawama zipeleke kwa aliyemuapisha.

Nikukumbushe tu, wakati wa JPM aliyehusika kuuhujumu huu mradi ni Makamba kwa kisingizio cha uharibufu wa mazingira,, sasa fikiria alikokuwa anazitoa hizo "guts" za kumhujumu JPM pamoja na ukali wote ule..

Kipindi Makamba anauhujumu mradi alikuwa wizara ya Muungano na Mazingira ambayo hufanya kazi kwa ukaribu na ofisi ya makamu wa Rais ( Makamu wa Rais kipindi hicho alikuwa Samia)..

Sasa hapo unga dot mwenyewe!

Nb: Rais hadanganywi, mpaka atake mwenyewe. Anavyo vyanzo vyake vya taarifa ambavyo ni vya kuaminika.

Ukiona kadanganywa jua ni mchongo anaoujua.
 
Hakuna lolote lile kutoka kwa uyo January
 
ukawe na sikukuu njema ya majilio mkuu pascal.
uongo na vitisho vilivyokuwepo kipindi kile chini ya JPM wengi waliamini kwamba ndiyo ukweli wa mambo ulivyo.
shirika kama TCCL lilitoa wapi pesa za kurudisha gawio wakati lilishajifia?
 
Ukweli wako Ni upi?
 
Aliyesema Bungeni umefika 52% ni nani? Sio kipara?
 
"zilongwa mbali zitendwa mbali" by aka Mkwere wa Msoga.

Tuishi kwa kiasi
 
KUNA MSEMO UNAOSEMA UKIWA MUONGO USIWE NA UGONJWA WA KUSAHAU
 
Vitu vingine ni kama ganda la mua la jana, kwako hana lolote, kwa wegine he is everything!.
P
Ganda la Muwa ni ganda la muwa tu..iwe kwao au kwa mtu mwingine...

Sijawahi Elewa hua unaona nn kwa huyu jamaa unless bado una matumaini kua siku moja atakua prezidaa and atalipa fadhila

...Ushawahi kujiuliza huyu dogo angekua sio mtoto wa kigogo angekua nani by now?maana ht shule alifail...He is nobody if you remove his Father's name.

But even with his Father's name he is no longer popular as he used to be, kismati kimekataa, na wajumbe wameonesha kua kwao Bashungwa or Musukuma are better off pamoja na hawa jamaa kutokua na ma God Fathers..

Even Juzi kwenye uzinduzi wa Bwawa, waalikwa walimuonesha kua the deadman is still powerfull than he is, infact the deadman was popular than meza kuu yote, hakuhitaji Mc kuomba makofi everytime jina lake likitajwa like the rest of them pamoja na wao kujitahidi sana kutolitaja jina lake, mind u si Maharage or jamaa yako aliedhubutu ku acknowledge or kulitaja jina la marehemu popote bt he the deadman was still the man of the show.
 
Sasa kama Januari akiwa kwenye Umma anamdanganya kwa kiwango hiki Mh Rais swali je wanapokuwa kwenye vikao vya ndani kama Baraza la Mawaziri au vikao vya wao wawili anamdanganya mambo mangapi juu ya uendeshaji wa nchi yetu.
Hapo ndipo mdanganywa anavaa udanganyika
 
Kiiini Cha tatizo hili ni mfumo

Hii Katiba yetu ndiyo "kimeo" kikuu😎

wewe uliona wapi katika nchi za wenzetu, Rais wa nchi anateua maelfu ya watendaji wake, bila kuhojiwa ametumia vigezo gani kuwateia hao wateule wake???

Dawa ya huu upuuzi wote huu ni kupata Katiba mpya, itakayoendana na mfumo wa vyama vingi tulionao

Lakini Kwa Katiba tuliyo nayo hivi Sasa, ambayo imempa madaraka makubwa mno, mithili ya ki-mungu, hatuwezi kutoboa maisha yetu yote, watanzania.

Badala yake Taifa letu litaendelea kuwa miongoni ya mataifa masikini Sana Duniani (licha ya malliasili nyingi ssna tulizo nazo)
 
Kwani rais ni rahisi hivi kiasi cha kushindwa kutofautisha uongo na ukweli?
 
Hapa si bure kuna namna .kuna msemo wa unasema tumikia kafiri ili upate umradi wako naona hicho ndicho ulichokifanya hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…