Makamba unampa taarifa za uongo Rais kwa faida ya nani?

Makamba unampa taarifa za uongo Rais kwa faida ya nani?

Mkuu saidoo25, mnyonge mnyongeni, haki yake mpeni, kiukweli kabisa hawa vijana 3, January, Mwigulu na Nape, wanamsaidia sana Samia!.

Kufuatia Magufulification style of working, viongozi wengi wamekuwa na nidhamu ya uoga hivyo walikuwa wanamdanganya JPM, hili la nidhamu ya uoga, nililizungumza Je, Hizi Terorizing za Ziara za Kushtukiza, Hakutajenga Nidhamu ya Woga, Kutasaidia?!. ilifikia kiwango taasisi za umma zinakopa bank kupeleka gawio kwa JPM zionekane zinazalisha faida!.

Kufuatia uoga huu JPM akawa anaogopwa hadi kudanganywa!. January ni mmoja wa mawaziri vijana very bold, ataisema ukweli wa mambo ulivyo na sio kufurahisha watu, kuhusu mradi wa JNHPP, January amesema kila kitu
Enzi za JPM, focus ya mradi huu ilikuwa ni ujenzi tuu wa bwawa, enzi za Samia kupitia January focus sio bwawa tuu bali na miundo mbinu ya kuusambaza umeme huu, mafanikio isiwe kumaliza bwawa au kulijaza maji bali umeme uzalishwe utumike!. Hizo data za mwanzo ni zile January alizozikuta zikimdanganya JPM, sasa anatoa data za ukweli.

P
Mmh,sawa,wakufikirie siku zinayoyoma mno angarau hata.......
 
Mkuu Pascal Mayalla Hotuba tunayoinukuu ni Mwaka wa Fedha 2021/2022 ambayo iliwasilishwa bungeni Mwezi Juni 2021 ambapo JPM alishafariki katikati ya Machi 2021.... Hivyo hiyo Hotuba na hizo takwimu huwezi kuziita za uongo na zililenga kumdanganya Magufuli kwani alikuwa ameshalala mauti.

Swali la Msingi hapa ni kwanini Januari amdangaye Rais kuhusu Asilimia wakati hiyo taarifa ni ya Wizara ya Nishati na sio taarifa ya Familia yake ya WAZURI HAWAFI.

Hii sio mara ya kwanza kwa Januari kumdanganya Rais mbele ya Umma rejea tukio la Geita kuhusu Idadi ya Vijiji vilivyounganishwa na umeme Vs vijiji vilivyoko Mkoa wa Geita.

Rejea majibu yake bungeni kuhusu sababu za kukatika umeme

Mwisho umesikiliza tukio la kujaza maji juzi, umesikia Januari amesema mradi utakamilika lini? na je kuhusu madai ya Serikali ya Trilioni 1.5 kama faini ya kuchelewesha mradi nayo umemsikia amesema nini?

Hakuna mtu anayemchukua Januari personaly, ni mtu muungwana sana na ni kipenzi cha waandishi wa habari na wasanii ila hapa tunazungumzia madaraka ya uwaziri ambao ni mali ya umma.
Best comment of the year
 
Tatizo sio Makamba, hakujipa hicho cheo!

Kama ni lawama zipeleke kwa aliyemuapisha.

Nikukumbushe tu, wakati wa JPM aliyehusika kuuhujumu huu mradi ni Makamba kwa kisingizio cha uharibufu wa mazingira,, sasa fikiria alikokuwa anazitoa hizo "guts" za kumhujumu JPM pamoja na ukali wote ule..

Kipindi Makamba anauhujumu mradi alikuwa wizara ya Muungano na Mazingira ambayo hufanya kazi kwa ukaribu na ofisi ya makamu wa Rais ( Makamu wa Rais kipindi hicho alikuwa Samia)..

Sasa hapo unga dot mwenyewe!

Nb: Rais hadanganywi, mpaka atake mwenyewe. Anavyo vyanzo vyake vya taarifa ambavyo ni vya kuaminika.

Ukiona kadanganywa jua ni mchongo anaoujua.
Correct [emoji817]%
 
Nitajie Waziri yoyote ndani ya serikali ya JPM na Samia, ambaye ni bold enough angeweza kusema ukweli mchungu kama huu?.
Nani angethubutu kuyasema haya?.
P

Mkuu watanzania hasa viongozi wa ccm huwa wana uwezo mdogo wa kufikiri na kila kukicha wao nikusifia watawala wao hata pale wanapokosea kwa leongo yakutengeneza mazingira yao wenyewe na familia zao.. kwani suala la gesi si toka awamu ya JK wimbo huo huo unaimbwa, akaja JPM wimbo huo huo sasa hivi yupo mwingine na mawaziri wake na wimbo ni huohuo...
 
Umejishushia hadhi kwa namna fulani. Sipo kumsifu JPM au kukubali uongo na uoga kwa watendakazi wake lkn . Tukuukulize kama mwana habari nguli na mwanasheria.
1. Ipi tuianini alipokea bwawa likiwa 52% au 37% na pia je aliyesema 22% naye akiwa kiongozi nani mkweli?

2. Umesena JpM alikuwa na ujenzi tu wa Bwawa, je hii ni kweli? Kuwa usalishaji wa hizo megawat zaidi ya 2000 hazikuwa kwenye lengo na wala usambazaji wake. Je hayo maji wangejaza kwa ajili ya uogeleaji au kufugia samaki na kilimo?

Nchi imejaa kujipendekeza ili mtu apewe nafasi ya kula i.e hayupo yanayetumika kwa ajili ya nchi.
hako kajamaa kanaonesha ni kiasi gani kalivyo keupe kichwani na ni type ya wale watu wa kujipendekeza bila kujali ni maumivu kiasi gani wanapitia wananchi kwa sasa
 
Kwa Mujibu wa Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nishati kwa mwaka 2021/2022 nanukuu "Kuendelea na Ujenzi wa Mradi wa Julius Nyerere Hydro Power Project (JNHPP) MW 2,115 ambao hadi kufikia mwezi Mei, 9 2021 utekelezaji wake kwa ujumla umefikia asilimia 52'" mwisho wa kunukuu.

Sasa juzi Januari Makamba akamdanganya tena Mh Rais kwamba 2021 wakati anaingia mradi ulikuwa kwa asilimia 37, Mwigulu naye akihojiwa na Clouds naye akasema wakati Rais anaingia mradi ulikuwa asilimia 22.

Sasa kama Januari akiwa kwenye Umma anamdanganya kwa kiwango hiki Mh Rais swali je wanapokuwa kwenye vikao vya ndani kama Baraza la Mawaziri au vikao vya wao wawili anamdanganya mambo mangapi juu ya uendeshaji wa nchi yetu.

Pascal Mayalla mfuatilie na mkalitazame na hili.
Maza naye washajua udhaifu wake kuwa ni mpenda sifa
 
Mkuu watanzania hasa viongozi wa ccm huwa wana uwezo mdogo wa kufikiri na kila kukicha wao nikusifia watawala wao hata pale wanapokosea kwa leongo yakutengeneza mazingira yao wenyewe na familia zao.. kwani suala la gesi si toka awamu ya JK wimbo huo huo unaimbwa, akaja JPM wimbo huo huo sasa hivi yupo mwingine na mawaziri wake na wimbo ni huohuo...
Hakuna kiongozi mjinga ccm, wote wako smart na akilizao zinafanya kazi vizuri tu,hao wanajitoa akili makusudi Ili mambo yao yaende sawa.
Wanafanya ujingaujinga makusudi kwa sababu wanajua wananchi hawawezikuwafanya chochote.
 
Mm n familia yangu tumemwelewa makamba Jr.
Mama kanyaga twende tumecheleweshwa mnooo kama taifa zaidi ya miaka 7.





Tunachokijua:
 
Pascal Mayalla Makamba alionekana kipanga na ana akili sana kwa sababu alikuwa hajawahi kukabidhiwa jukumu rasmi la kulisimamia yeye kama yeye ndio maana siku zote ilikuwa sio rahisi kuujua uwezo wake ila alipopewa Wizara ya Mazingira na Sasa Nishati ndio watanzania sasa wanaujua rasmi uwezo wake bila kusimuliwa na mtu yoyote.
Uwezo wqke tumeupima na kuuona..
 
Tanzania Coal

Summary Table

TonsGlobal Rank

Coal Reserves

296,521,390 50th in the world

Coal Production

304,238 56th in the world

Coal Consumption

327,861 87th in the world

Yearly Deficit

-23,623

Coal Imports

84,992

Coal Exports

53,522

Net Imports

31,470

(Data shown is for 2016, the latest year with complete data in all categoreies)
Swali. Hitaji la Tanzania ni Megawatt ngapi? Ili tuone kuwa uzalishaji wa Mw 2100 hautoshi
 
Shida yenu mnapenda kusikia habari mnazopenda kuzisikia au mnazoaminishana hata kama za uongo. Lakini huo ndio ukweli kulikuwa na upishi wa data kwa kiwango kikubwa kumdanganya mzee kuwa kazi inafanyika. Hizo taarifa za kuongopa idadi ya vijiji vilivyounganishwa umeme hazikutolewa ili kumuharibia mtu bali ni uhalisia.

Je uliwahi kusikia wakati wa JPM kukisainiwa mkataba wa kujenga miundombinu ya kuutoa umeme huko Rufiji kuja kwenye gridi?

Hii ya Trillioni 1.5 kwanini mnapenda kulishana ujinga? Mikataba haiandaliwi kizembe hivyo. Nani hajui kama kulikuwa na breakdown ya supply ya kila kitu duniani wakati wa Corona. Au wewe unaona mambo yalienda sawa tu wakati wa Corona! Ungekuwa unajihusisha na masuala ya biashara za kimataifa ungejua hali ilivyokuwa wakati wa Corona. Everything just paralyzed, sasa utatumiaje hicho kifungu kwa sababu zilizo nje ya uzembe wake? Kama mna risiti kuwa mkandarasi alilipa hicho kiasi na zikaliwa ziletwe hapa. Msiishi kwa kupenda kuyasikia mtakayo, wakati mwingine yapeni masikio yenu taarifa mbadala.
Swali kwenye mada ni hili 52%, 37% au 22% wakati Makamba anapokea uwaziri?
 
Swali kwenye mada ni hili 52%, 37% au 22% wakati Makamba anapokea uwaziri?
Wakati Makamba anaingia madarakani sijawahi kusikia ikitajwa alichukua ikiwa asilimia ngapi ila wakati Samia anaingia ilikuwa 37%. Hiyo 22% sikuwahi kuiskia labda kama una clip yake niisikilize huenda nikajua ni kitu gani kilichokuwa kinazungumziwa. 52% ni chai za Kalemani tu hizo.
 
Wakati Makamba anaingia madarakani sijawahi kusikia ikitajwa alichukua ikiwa asilimia ngapi ila wakati Samia anaingia ilikuwa 37%. Hiyo 22% sikuwahi kuiskia labda kama una clip yake niisikilize huenda nikajua ni kitu gani kilichokuwa kinazungumziwa. 52% ni chai za Kalemani tu hizo.
Mwigulu anasema Bwawa lilikuwa 12% wakati Rais Samia anaingia madarakani
 
Nitajie Waziri yoyote ndani ya serikali ya JPM na Samia, ambaye ni bold enough angeweza kusema ukweli mchungu kama huu?.
Nani angethubutu kuyasema haya?.
P

Pascal Mayalla naomba nikuthibitishie Januari Makamba ni rafiki sana wa waandishi wa habari na wasanii na anatumia sehemu kubwa ya fedha kujenga mahusiano nao kwa faida hizi unazozisema. Lakini mbele ya macho ya watanzania ni tofauti.
 
Back
Top Bottom