Makambo na Kisinda wanasubiri nini Yanga?

Makambo na Kisinda wanasubiri nini Yanga?

KAGAMEE

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2013
Posts
4,457
Reaction score
5,454
Mimi siyo wa kulalamika but nimefatilia uchezaji wa MAKAMBO na KISINDA kwa msimu huu hakuna kitu wanaisaidia timu bora wapelekwe hata Simba SC kwa mkopo.

Ni kweli sisi ni unbeaten, Tunaongoza ligi,tunaongoza kuwa na furaha,tuna jezi nzuri Afrika. Lakini nataka kujua hawa watu wana mchango gani kwa timu Mwenye statistics zao za msimu huu alete hapa.

Timu yetu ina utaratibu wa kutoa misaada kwa wenye uhitaji basi MISHAHARA wanayolipwa hawa watu ingepelekwa huko tungepata faida kubwa sana. Watu wanacheza kama hawalipwi (no fighting spirit)Na benchi la ufundi wanawaangalia tu?.

Halafu nyie mnaosema ile siyo PENALTY mlitaka TULIKATAE? Wakati tunalalamika ubovu wa Marefa NBC PREMIER LEAGUE si mlituita MALALAMIKO FC mara kila MTU ASHINDE MECHI ZAKE(Badala ya kuungana na sisi)?.

Mnasema ndio maana kimataifa hatutoboi,tusipotoboa ndo tunakuwa BEATEN?

Kama nyie mnapata raha KIMATAIFA sisi tumechagua kupata raha hapa Nchini tusichaguliane pls.

Kihimbwa kanituma salamu.
 
Back
Top Bottom